Nawafafanulia vipi wanangu kwamba Israel inalindwa na Teknolojia huku Africa tunamuomba Mungu wa Israel atulinde

Nawafafanulia vipi wanangu kwamba Israel inalindwa na Teknolojia huku Africa tunamuomba Mungu wa Israel atulinde

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Israel inajilinda na umasikini kwa kuwekeza kwenye elimu ya ubunifu wa teknolojia, hawana madini ardhi yao sehemu kubwa ni jangwa lakini kupitia Teknolojia wana uchumi wa dola bilioni 500 (Trilioni elf 1 na 500) kusanya nchi zote za Afrika Mashariki hatufikii. Kampuni yenye teknolojia kubwa ya umwagiliaji duniani ipo Israel, Kampuni nyingi zimeweka ofisi za ubunifu Israel, n.k.

Hizi ni nchi zenye uchumi mkubwa zaidi Mashariki ya Kati, Chanzo ni Wikipedia kwa kutumia takwimu za IMF shirika la fedha la kimataifa.

Soma Pia: Afrika tunaomba Mungu wa Israel atulinde. Israel inalindwa na mitambo ya teknolojia ya hali ya juu kuzuia mashambulizi ya anga

1728328936702.png

Israel inarushiwa makombora hawakimbilii kanisani kusema ni mipango ya Mungu kungoja kiama, wameumiza vichwa kubuni mitambo maalum ya kutungua makombora mengi (sio yote) kabla hayajatua,

1728329015604.png

Nawaelezeaje wanangu kwamba Africa inalindwa na Mungu wa Israel kwenye Umasikini, Ujinga na maradhi wakati Israel inategemea zaidi Teknolojia kupunguza makali ?

1728329113737.png
 
Wachane tu laivu kama ulivyoandika kwenye kichwa.

Wazungu wana msemo ELI5 (wazungu wa reddit) na nionavyo mimi kichwa cha habari kinaeleweka kabisa hata kwa kijana wa miaka mitano.
 
Israel inajilinda na umasikini kwa kuchapa kazi kwenye biashara na ubunifu wa teknolojia, Kampuuni nyingi zina ofisi za uvumbuzi Israel, Israel ina kampuni inayoongozea kwenye teknolojia ya umwaguliaji duniani....
Nchi ya pili kwa uchumi mashariki ya kati kwa data za wapi mkuu, maana imf leo imetoa report ya nchi kumi duniani zenye uchumi mkubwa mbilo kutoka middle east ambayo ni qatar na uae ,israel haipo
 
Wachane tu laivu kama ulivyoandika kwenye kichwa.

Wazungu wana msemo ELI5 (wazungu wa reddit) na nionavyo mimi kichwa cha habari kinaeleweka kabisa hata kwa kijana wa miaka mitano.
Explaining Like am Five uwongo?

Yeah kweli mwambie ajue ABC akikua zaidi ataelewa XYZ
 
Nchi ya pili kwa uchumi mashariki ya kati kwa data za wapi mkuu, maana imf leo imetoa report ya nchi kumi duniani zenye uchumi mkubwa mbilo kutoka middle east ambayo ni qatar na uae ,israel haipo
Chanzo ni wikipedia, Pia nitoe ufafanuzi wa Ziada pato la nchi kama saudi arabia ni mara mbili ya Israel lakini Saudi Arabia ina eneo kubwa zaidi ya mara 100 kuzidi Israel na watu wengi zaidi kuliko Israel, kwahio inabidi utilie maanani size ya nchi na population

1728326884875.png

Israel inajilinda na umasikini kwa kuwekeza kwenye elimu ya ubunifu wa teknolojia, hawana madini ardhi yao sehemu kubwa ni jangwa lakini kupitia Teknolojia wana uchumi wa dola bilioni 500...
Weka current data kutoka imf ndio kazi yao hiyo mkuu haya kamata hiyo hapo ipo ya sita huko acheni kudanganya watu
 
Attachments

  • Screenshot_20241007-212813_Chrome.jpg
    Screenshot_20241007-212813_Chrome.jpg
    208.2 KB · Views: 2
Huna hoja ndio maana unatukana ,mtu mwenye akili huwa hatukani huwa anaweka hoja, kutukana ni kjidhalilisha na kuwadhaliliaha waliokulea
 
Chanzo ni wikipedia, Pia nitoe ufafanuzi wa Ziada pato la nchi kama saudi arabia ni mara mbili ya Israel lakini Saudi Arabia ina eneo kubwa zaidi ya mara 100 kuzidi Israel na watu wengi zaidi kuliko Israel, kwahio inabidi utilie maanani size ya nchi na population

View attachment 3118146
Kwenye hii list hawa wote wakiungana Bado watapigwa na Israel
 
Chanzo ni wikipedia, Pia nitoe ufafanuzi wa Ziada pato la nchi kama saudi arabia ni mara mbili ya Israel lakini Saudi Arabia ina eneo kubwa zaidi ya mara 100 kuzidi Israel na watu wengi zaidi kuliko Israel, kwahio inabidi utilie maanani size ya nchi na population

View attachment 3118146
Yaani israel iwe na pato kubwa kushinda saudi arabia? Huu ni uongo uliodhahiri kabisa
 
Nawaelezeaje kwamba Africa inalindwa na Mungu wa Israel kwenye Umasikini, Ujinga na maradhi
Huko kushindwa kwako kuwafafanulia ni moja ya mipango ya Mungu ili usiwapotoshe hao malaika
Ni kama vile tu alivyokwamisha ujenzi wa mnara wa Babeli
 
Unaambiwa ukuta wa yeriko uliangushwa Kwa nyimbo tu. Lkn Israel Ina makombola Kila kona. Walokole ni wajinga mnoo hakuna mfano.
Mwamposa akiugua huyo hospital mbio mbio kutibiwa halafu Hawa kondoo wananunua udongo na mafuta
 
Huna hoja ndio maana unatukana ,mtu mwenye akili huwa hatukani huwa anaweka hoja, kutukana ni kjidhalilisha na kuwadhaliliaha waliokulea
Ukiwa ngedere lazima tukutukane maana unaandika pumba tupu humu🤣🤣🤣🤣🤣
 
Weka current data kutoka imf ndio kazi yao hiyo mkuu haya kamata hiyo hapo ipo ya sita huko acheni kudanganya watu
Nimekuwekea chanzo cha uhakika cha wikipedia kinachochukua data Imf

Hicho chanzo chako hakina uaminifu, hakina reference ya sehemu walipochua data, ni website ya mtu binafsi si ajabu kajitungia.
 
Back
Top Bottom