Nawafundishaje walimu ili waje kufundisha?

Nawafundishaje walimu ili waje kufundisha?

Dark City

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2008
Posts
16,253
Reaction score
11,626
Ndugu zangu wana MMU,

Naomba mnisaidie jambo ambalo limenikwaza kidogo. Ngoja nijaribu kueleza mambo yalivyonibana.

Tuchukulie kwamba wewe ni mwalimu ambaye unafundisha wanafunzi ambao ni walimu watarajiwa (mwalimu wa walimu).

Bahati mbaya somo lako linawapa taabu sana na hawaonekani kuelewa vitu vya msingi. Muda unaenda na wanatakiwa kufanya mtihani wa kumaliza masomo. Wewe mwenyewe ndiye unautunga na kusahihisha. Kwa vile muda wa kufanya mtihani bado kidogo, utawasaidiaje vijana wako ili walaulu?

Na si kufaulu tu, ila huko mbele ya safari waweze kufundisha wanafunzi wao vizuri?

Je, utawapitisha hivyo hivyo liwalo na liwe?

Au utabanana nao hadi kieleweke?

Kwamba hata wakifeli wote, potelea mbali kuliko kupeleka makapi uraiani?

Wenu katika kizungumkuti.

Babu DC

cc: Asprin, Kaizer, Fixed Point, King'asti, Mtambuzi, snowhite, gfsonwin, Mbu, Paloma, CHUAKACHARA, Mwanyasi, KOKUTONA, YNNAH, Arabela (sitakunyaka mdogo wangu), MwanajamiiOne, watu8..
 
hii thread kwa nin umeileta jukwaa hili? Btw we fuata principles za kufundisha zinasemaje si ulijifunza ethics za teaching mkuu?
 
kuna mawili hueleweki au unaowafundisha hawaelewi
 
Tafuta njia mbadala ya ufundishaji inayoendana na mada husika ikiwezekana wabadilishie mazingira inakuwa ngumu kutoa ushauri pasipo kujua mada husika.
 
Unatakiwa utafute mwalimu mwingine awafundishe hilo somo hata kwa extra time ili wapate uelewa mzuri eneo hilo kisha urudi ukasome mbînu za ufundishaji!

Hahahahahahahaha,

Nitaweza kurudi class Filipo kweli....

Mbona unanimaliza hivyo?

Mkuu wape nafasi ya kukuasses binafsi kupitia dondoo mbalimbali..... Hlf uangalie unapungukiwa wapi.
Wape mtihani, watakaoshindwa wabebeshe supp.
Dah!yalishanikuta hayo, kufundisha ni tabu.

Bora wewe umenielewa...lol!

kuna mawili hueleweki au unaowafundisha hawaelewi

Kuna pia la tatu....wote hatusomeki...au unasemaje?

Tafuta njia mbadala ya ufundishaji inayoendana na mada husika ikiwezekana wabadilishie mazingira inakuwa ngumu kutoa ushauri pasipo kujua mada husika.

Mbona mada ni hii hii The secretary...au hutaki kumwokoa Babu?
 
Last edited by a moderator:
Hahahahahahahaha,

Nitaweza kurudi class Filipo kweli....

Mbona unanimaliza hivyo?



Bora wewe umenielewa...lol!



Kuna pia la tatu....wote hatusomeki...au unasemaje?



Mbona mada ni hii hii The secretary...au hutaki kumwokoa Babu?

kweli kabisa inawezekana ni pipa na mfuniko
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo nichape supp za kutosha na wengine wakariri mwaka?

Ungekuwa wewe ndiye denti ungejisikiaje??

Nimechanganywa mkuu ujue?
Babu kwani hawaelewi topic zote kwenye hilo somo?
Kwa nijuavyo mimi siyo lazima kutunga mtihani kwenye topic zote kwenye syllabus......... waweza tumia hiyo loophole.....
Ila kama hiyo topic ni nyeti sana basi komaa nao kwa kuwapa maswali mengi uwezavyo, wanaweza wakapata kitu through questions.........
Ni mawazo yangu tu kama mwanafunzi, sijui walimu wanawazaje?
 
Wakifeli ina maana hawajafaa basi kama hawajafaa hawatokaa wawe Walimu. As long as umetimiza wajibu wako na umetumia tekniki zote mujarabu sioni shida, unless uwe umewatunuku kiasi cha kuuza roho yako wawe "walimu"
 
Kwanza huwa sikubali wanafunzi wasielewe....! Wasipoelewa hujiona mimi ndio tatizo..!!

Hujitahidi sanaa kulifanya somo langu mpaka lieleweke....!

Ikitokea kuna baadhi hawaelewi kwa kweli huwa nakula vichwa tuu..!

Weee kula vichwa tuuu hakuna kufaulisha watu wasio na sifa...!!
 
Back
Top Bottom