Ndugu zangu wana MMU,
Naomba mnisaidie jambo ambalo limenikwaza kidogo. Ngoja nijaribu kueleza mambo yalivyonibana,
Tuchukulie kwamba wewe ni mwalimu ambaye unafundisha wanafunzi ambao ni walimu watarajiwa (mwalimu wa walimu). Bahati mbaya somo lako linawapa taabu sana na hawaonekani kuelewa vitu vya msingi. Muda unaenda na wanatakiwa kufanya mtihani wa kumaliza masomo. Wewe mwenyewe ndiye unautunga na kusahihisha. Kwa vile muda wa kufanya mtihani bado kidogo, utawasaidiaje vijana wako ili walaulu? Na si kufaulu tu, ila huko mbele ya safari waweze kufundisha wanafunzi wao vizuri?
Je, utawapitisha hivyo hivyo....liwalo na liwe? Au utabanana nao hadi kieleweke? Kwamba hata wakifeli wote, potelea mbali kuliko kupeleka makapi uraiani?
Wenu katika kizungumkuti,
Babu DC!!
cc:
Asprin,
Kaizer,
Fixed Point,
King'asti,
Mtambuzi,
snowhite,
gfsonwin,
Mbu,
Paloma,
CHUAKACHARA,
Mwanyasi,
KOKUTONA,
YNNAH,
Arabela (sitakunyaka mdogo wangu),
MwanajamiiOne,
watu8..