Nawafundishaje walimu ili waje kufundisha?

Nawafundishaje walimu ili waje kufundisha?

Kuna tofauti ya umuhimu wa hicho unachowafundisha hapo awali na sasa? Je huko nyuma walikuwa wanafaulu kwa urahisi? Wakati mwingine wanafunzi hupuuzia vitu ambavyo wanahisi havina umuhimu sana au kwa mazingira yaliyopo wanaona watafaulu tu.

Lakini mbona haya matatizo nakumbana nayo sasa na siyo enzi zile?

Mbona sisi tulifundishwa hivi hivi tukaelewa na wanafunzi wetu wa awali sasa ni maprofesa wazuri.

Hawa wa sasa ndiyo wamekuwaje? Au sisi ndiyo tumepitwa na time?
 
Mkuu ushauri ulioupata kutoka kwa wadau ni positive, hapo unatakiwa tu uchanganye na zako maana wewe unajua mazingira ya shule unayofundisha, wanafunzi wako na hilo somo linalokupa taabu, kuna msemo mmoja uliwahi kunukuliwa kutoka kwa mmoja wa matajiri wakubwa duniani kwamba ukitaka jambo lako lifanywe haraka na kwa ufanisi basi jambo hilo mpe mtu mvivu. Hebu tafuta mwanafunzi mmoja mvivu halafu mpe hiyo task anaweza kukusaidia kupata majibu muafaka.

Mzee mwenzangu, hvi huu uzi umewaalika kina Nyani Ngabu, Kaizer, Kiranga, EMT, Gaijin, gfsonwin, snowhite, Ruttashobolwa, BAK, Ntuzu na Kaunga ?
 
wambie wanafunzi kila mmoja aandike mawazo yake kwenye kikaratasi bila ya kuandika jina lake, ukweli watakueleza wanafunzi hawana khiyana kwa mwalimu kilaza
 
Khaaaaaaaaaaaaaaaaaa,

Nijibu nini swahiba wangu?

Just take any example, si kila kitu kina vitu ambavyo ndiyo vinakifanya kisimame? Mfano, nia na mtaji katika biashara!

......Mnh! Swahiba!

Hiyo reference uliyoitoa, 'si kila kitu kina vitu ambavyo vinakifanya kisimame' wanafunzi watakukimbia!
 
Mkuu ushauri ulioupata kutoka kwa wadau ni positive, hapo unatakiwa tu uchanganye na zako maana wewe unajua mazingira ya shule unayofundisha, wanafunzi wako na hilo somo linalokupa taabu, kuna msemo mmoja uliwahi kunukuliwa kutoka kwa mmoja wa matajiri wakubwa duniani kwamba ukitaka jambo lako lifanywe haraka na kwa ufanisi basi jambo hilo mpe mtu mvivu. Hebu tafuta mwanafunzi mmoja mvivu halafu mpe hiyo task anaweza kukusaidia kupata majibu muafaka.

Mzee mwenzangu, hvi huu uzi umewaalika kina Nyani Ngabu, Kaizer, Kiranga, EMT, Gaijin, gfsonwin, snowhite, Ruttashobolwa, BAK, Ntuzu na Kaunga ?

Mimi tena nikose? Hahahaa haiwezekani
 
Tafuta mwalimu mwengine anayefundisha somo hilo akusaidie, mueleze tatizo pengine material unayo lakini uwezo wa kuyadeliver kwa unowafundisha ili wakuelewe ndo shida. Omba msaada kwa walimu wengine

Babu kwani umehamia kwenye fani ya snowhite, mimi na gfsonwin?

Mwalimu nimewamisi sana! Hi kwa Ma Mkwe na Mwalimu!

cc Kaizer
 
Last edited by a moderator:
Babu DC longtime no see!

Wacha nijifanye mwanafunzi then nikujibu.

Nahisi mwlm asipokijua anachokifundisha ndio tatizo no 1!
Kuna wlm hawafanyi research na proof reading ya yale wanayokwenda kuyafundisha. Wanasomesha kwa mazoea and/or ufaulu wake kipindi anasoma, may be alipata 1st class.

Uwezo wa kuelezea. Hili ni tatizo no 2.
Wanafunzi wanaelewa tofauti, wengine ni wepesi na wengine ni wazito kuelewa.

Usidhani kila anaesoma chuo ni brave, uzame deep kwa mifano, mifano ni muhimu sana kwa sisi vichwa ngumu.

Toa hata out line ya mada na kuelezea lengo la mada hiyo kwa wfunzi huku ukiwakumbusha maeneo muhimu wasiopashwa kuyasahau ktk mada hiyo.
Wape maswali kila baada ya hatua moja ambayo unahisi kuna swali, simamia vizuri presentations hakikisha wanapresent na sio unawaachia wasome manotes waliokusanya.

Eds
teaching methods and techique. How to socialize with your students, hupaswi kuappear kama mwalimu tu, sometimes uwatokee kirafiki, haina maana kwamba ukae maskani zao and/or uende nao klabu.
 
watengenezee tutorial questions yenye suggestive answers ili wakalili then wambie mtihani wangu nitatoa humohumo
 
Ndugu zangu wana MMU,

Naomba mnisaidie jambo ambalo limenikwaza kidogo. Ngoja nijaribu kueleza mambo yalivyonibana.

Tuchukulie kwamba wewe ni mwalimu ambaye unafundisha wanafunzi ambao ni walimu watarajiwa (mwalimu wa walimu).

Bahati mbaya somo lako linawapa taabu sana na hawaonekani kuelewa vitu vya msingi. Muda unaenda na wanatakiwa kufanya mtihani wa kumaliza masomo. Wewe mwenyewe ndiye unautunga na kusahihisha. Kwa vile muda wa kufanya mtihani bado kidogo, utawasaidiaje vijana wako ili walaulu?

Na si kufaulu tu, ila huko mbele ya safari waweze kufundisha wanafunzi wao vizuri?

Je, utawapitisha hivyo hivyo liwalo na liwe?

Au utabanana nao hadi kieleweke?

Kwamba hata wakifeli wote, potelea mbali kuliko kupeleka makapi uraiani?

Wenu katika kizungumkuti.

Babu DC

cc: Asprin, Kaizer, Fixed Point, King'asti, Mtambuzi, snowhite, gfsonwin, Mbu, Paloma, CHUAKACHARA, Mwanyasi, KOKUTONA, YNNAH, Arabela (sitakunyaka mdogo wangu), MwanajamiiOne, watu8..

Chunguza vizuri tatizo litakua kwako katika mbinu za kufundisha hao ndugu,labda kama darasa hilo ni watu watundu na sio wasikivu,ikiwa hivyo tu toa taarifa kwa mkufunzi mkuu ili mshauluane namna ya kuwasaidia
 
Je masomo mengine wanaelewa?
Kama wanaelewa basi katika somo lako kuna tatizo la aidha hao wanafunzi hawakuwa na vigezo vya kusoma somo hilo, ama mwalimu wa somo hilo (ambaye ni wewe) hana vigezo vya kufundisha somo hilo ama ufundishaji wake ni mbaya.

Trainers huwa wanatumia feedback forms....huwapa trainees wao wajaze kutoa mrejesho wa mapungufu ya trainer na training program yenyewe inavyofanyika....jaribu kutengeneza fomu ya hivyo uwape pengine kuna jambo dogo tu mnatofautiana, utalijua.
 
wambie wanafunzi kila mmoja aandike mawazo yake kwenye kikaratasi bila ya kuandika jina lake, ukweli watakueleza wanafunzi hawana khiyana kwa mwalimu kilaza

Inawezekana kabisa kwamba kweli mimi ndiye kilaza...

Babu DC longtime no see!

Wacha nijifanye mwanafunzi then nikujibu.

Nahisi mwlm asipokijua anachokifundisha ndio tatizo no 1!
Kuna wlm hawafanyi research na proof reading ya yale wanayokwenda kuyafundisha. Wanasomesha kwa mazoea and/or ufaulu wake kipindi anasoma, may be alipata 1st class.

Uwezo wa kuelezea. Hili ni tatizo no 2.
Wanafunzi wanaelewa tofauti, wengine ni wepesi na wengine ni wazito kuelewa.

Usidhani kila anaesoma chuo ni brave, uzame deep kwa mifano, mifano ni muhimu sana kwa sisi vichwa ngumu.

Toa hata out line ya mada na kuelezea lengo la mada hiyo kwa wfunzi huku ukiwakumbusha maeneo muhimu wasiopashwa kuyasahau ktk mada hiyo.
Wape maswali kila baada ya hatua moja ambayo unahisi kuna swali, simamia vizuri presentations hakikisha wanapresent na sio unawaachia wasome manotes waliokusanya.

Eds
teaching methods and techique. How to socialize with your students, hupaswi kuappear kama mwalimu tu, sometimes uwatokee kirafiki, haina maana kwamba ukae maskani zao and/or uende nao klabu.

Tatizo langu kubwa ni kwamba hili tatizo linaongezeka siku za karibuni?

Ina maana wale wanafunzi tuliokuwa nao enzi za utumishi wetu (I am retired) walikuwa super humans?
 
Inawezekana kabisa kwamba kweli mimi ndiye kilaza...
hamna sio wewe kilaza ila wanafunzi wana sifa za kipekee, unaweza kuwasomesha vipindi vyote na wasikufahamu ila akaenda mwanafunzi mwenzao akatumia muda mchache tu wakafahamu
 
ivi babu nina nini mimi na wewe lkn??
muda wangu bado haujafika tafadhali.
 
Ukiwapitisha hivyo hivyo utakuwa unawatengenezea tatizo ulilotengenezewa wewe - la kupitishwa hivyohivyo wakati unasoma!
 
Tuchukulie kwamba wewe ni mwalimu ambaye unafundisha wanafunzi ambao ni walimu watarajiwa (mwalimu wa walimu). Bahati mbaya somo lako linawapa taabu sana na hawaonekani kuelewa vitu vya msingi.

Ni somo lako tuu ndilo linawapa taabu au ni pamoja na baadhi ya masomo mengine au yote? Kama ni masomo yote, then hapo tatizo linaweza kuwa pana zaidi. Lakini kama ni somo lako tuu, then tatizo linaweza kuwa wewe au labda hilo somo ni gumu zaidi kupita masomo mengine.

Ila nakumbuka baadhi ya walimu ambao wanafundisha masomo ambayo ni compusory huwa wanajidai sana halafu wananoko sana kwa sababu wanajua whatever the case, wanafunzi hawezi kulikimbia somo.

Muda unaenda na wanatakiwa kufanya mtihani wa kumaliza masomo. Wewe mwenyewe ndiye unautunga na kusahihisha. Kwa vile muda wa kufanya mtihani bado kidogo, utawasaidiaje vijana wako ili walaulu?

Obvious lazima shule/chuo kitakuwa na standards za ku-set mitihani ambazo kama mwalimu unatakiwa uzifuate. Kama ni mwalimu unayeamini kwenye standards na quality, huwezi kupanua goli ili tuu wanafunzi wengi wafunge magoli. Bali utawafundisha skills za kufunga magoli kama Messi.

Na si kufaulu tu, ila huko mbele ya safari waweze kufundisha wanafunzi wao vizuri? Je, utawapitisha hivyo hivyo liwalo na liwe? Au utabanana nao hadi kieleweke? Kwamba hata wakifeli wote, potelea mbali kuliko kupeleka makapi uraiani?

Prevention is always better than protection. Quality is always better than quantity. Mfano angalia sasa jinsi tunavyohangaika na elimu yetu iliyoshuka.

Nisisahahu huwa pia kuna mtindo wa wanafunzi kwa sababu fulani kuamua kumchukia mwalimu na automatically kuchukia hata somo analofundisha. Nakumbuka form one na two nilikuwa napenda sana biology na nilikuwa napasua, lakini kuanzia form three nililichukia hilo somo kisa mwalimu. The same happened nilipokuwa elimu ya juu; module moja niliipenda sana lakini nilipohudhuria lectures tatu tuu nikaona lecturer mzinguaji nika-switch kwenye module nyingine ambayo sikuipenda saaana lakini jinsi mwali alivyokuwa anafundisha mpaka leo nazikumbuka lectures zake. Major topics zimenikaa kichwani mpaka leo.
 
Back
Top Bottom