Kuna tofauti ya umuhimu wa hicho unachowafundisha hapo awali na sasa? Je huko nyuma walikuwa wanafaulu kwa urahisi? Wakati mwingine wanafunzi hupuuzia vitu ambavyo wanahisi havina umuhimu sana au kwa mazingira yaliyopo wanaona watafaulu tu.
Khaaaaaaaaaaaaaaaaaa,
Nijibu nini swahiba wangu?
Just take any example, si kila kitu kina vitu ambavyo ndiyo vinakifanya kisimame? Mfano, nia na mtaji katika biashara!
Mkuu ushauri ulioupata kutoka kwa wadau ni positive, hapo unatakiwa tu uchanganye na zako maana wewe unajua mazingira ya shule unayofundisha, wanafunzi wako na hilo somo linalokupa taabu, kuna msemo mmoja uliwahi kunukuliwa kutoka kwa mmoja wa matajiri wakubwa duniani kwamba ukitaka jambo lako lifanywe haraka na kwa ufanisi basi jambo hilo mpe mtu mvivu. Hebu tafuta mwanafunzi mmoja mvivu halafu mpe hiyo task anaweza kukusaidia kupata majibu muafaka.
Mzee mwenzangu, hvi huu uzi umewaalika kina Nyani Ngabu, Kaizer, Kiranga, EMT, Gaijin, gfsonwin, snowhite, Ruttashobolwa, BAK, Ntuzu na Kaunga ?
Ndugu zangu wana MMU,
Naomba mnisaidie jambo ambalo limenikwaza kidogo. Ngoja nijaribu kueleza mambo yalivyonibana.
Tuchukulie kwamba wewe ni mwalimu ambaye unafundisha wanafunzi ambao ni walimu watarajiwa (mwalimu wa walimu).
Bahati mbaya somo lako linawapa taabu sana na hawaonekani kuelewa vitu vya msingi. Muda unaenda na wanatakiwa kufanya mtihani wa kumaliza masomo. Wewe mwenyewe ndiye unautunga na kusahihisha. Kwa vile muda wa kufanya mtihani bado kidogo, utawasaidiaje vijana wako ili walaulu?
Na si kufaulu tu, ila huko mbele ya safari waweze kufundisha wanafunzi wao vizuri?
Je, utawapitisha hivyo hivyo liwalo na liwe?
Au utabanana nao hadi kieleweke?
Kwamba hata wakifeli wote, potelea mbali kuliko kupeleka makapi uraiani?
Wenu katika kizungumkuti.
Babu DC
cc: Asprin, Kaizer, Fixed Point, King'asti, Mtambuzi, snowhite, gfsonwin, Mbu, Paloma, CHUAKACHARA, Mwanyasi, KOKUTONA, YNNAH, Arabela (sitakunyaka mdogo wangu), MwanajamiiOne, watu8..
wambie wanafunzi kila mmoja aandike mawazo yake kwenye kikaratasi bila ya kuandika jina lake, ukweli watakueleza wanafunzi hawana khiyana kwa mwalimu kilaza
Babu DC longtime no see!
Wacha nijifanye mwanafunzi then nikujibu.
Nahisi mwlm asipokijua anachokifundisha ndio tatizo no 1!
Kuna wlm hawafanyi research na proof reading ya yale wanayokwenda kuyafundisha. Wanasomesha kwa mazoea and/or ufaulu wake kipindi anasoma, may be alipata 1st class.
Uwezo wa kuelezea. Hili ni tatizo no 2.
Wanafunzi wanaelewa tofauti, wengine ni wepesi na wengine ni wazito kuelewa.
Usidhani kila anaesoma chuo ni brave, uzame deep kwa mifano, mifano ni muhimu sana kwa sisi vichwa ngumu.
Toa hata out line ya mada na kuelezea lengo la mada hiyo kwa wfunzi huku ukiwakumbusha maeneo muhimu wasiopashwa kuyasahau ktk mada hiyo.
Wape maswali kila baada ya hatua moja ambayo unahisi kuna swali, simamia vizuri presentations hakikisha wanapresent na sio unawaachia wasome manotes waliokusanya.
Eds
teaching methods and techique. How to socialize with your students, hupaswi kuappear kama mwalimu tu, sometimes uwatokee kirafiki, haina maana kwamba ukae maskani zao and/or uende nao klabu.
hamna sio wewe kilaza ila wanafunzi wana sifa za kipekee, unaweza kuwasomesha vipindi vyote na wasikufahamu ila akaenda mwanafunzi mwenzao akatumia muda mchache tu wakafahamuInawezekana kabisa kwamba kweli mimi ndiye kilaza...
ivi babu nina nini mimi na wewe lkn??
muda wangu bado haujafika tafadhali.
Mmmhh ulikua unatafutwa wewe ulijificha wapii
Tuchukulie kwamba wewe ni mwalimu ambaye unafundisha wanafunzi ambao ni walimu watarajiwa (mwalimu wa walimu). Bahati mbaya somo lako linawapa taabu sana na hawaonekani kuelewa vitu vya msingi.
Muda unaenda na wanatakiwa kufanya mtihani wa kumaliza masomo. Wewe mwenyewe ndiye unautunga na kusahihisha. Kwa vile muda wa kufanya mtihani bado kidogo, utawasaidiaje vijana wako ili walaulu?
Na si kufaulu tu, ila huko mbele ya safari waweze kufundisha wanafunzi wao vizuri? Je, utawapitisha hivyo hivyo liwalo na liwe? Au utabanana nao hadi kieleweke? Kwamba hata wakifeli wote, potelea mbali kuliko kupeleka makapi uraiani?