Nawajua mashoga 5, wote walianza kwa kufanyiwa dhuluma ya kingono utotoni

IslamTZ

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
309
Reaction score
182
3 10.21.56.jpeg

Abuu Kauthar

Nianze kwa kuelezea uzoefu wangu katika maisha wa kukutana na kuwajua mashoga. Nianze kwa kuomba msamaha kwa jina hilo kwani sina hakika kama ni rasmi na linakubalika kwao.

Nimepata kujuana na mashoga watano. Najua kuna makundi mengi katika hao wanaojitambulisha kama jamii ya LGBT, lakini nikizungumzia mashoga ninakusudia wanaume wanaofanyiwa mapenzi kupitia tundu la nyuma, ambalo limezoeleka kama ni kwa ajili ya kutolea mavi.

Watu hao watano ninaowajua wana jambo moja linalofanana. Wote waliingia kwenye tabia hiyo utotoni baada ya kunyanyaswa kwa muda mrefu, kingono. Mmoja wapo, nilimjua katika taasisi moja ya elimu, alinambia alifanyiwa mambo hayo na baba yake mdogo, mwingine ambaye ni mdogo wangu wa mama mdogo alinyanyaswa utotoni na jirani.

Mwingine ni kijana wa Kiarabu kule Dodoma ambaye alikuwa rafiki wa mjomba angu, akisoma shule ya Mazengo. Mara kadhaa alimfuata mjomba kumuomba amuombee dua aache tabia hiyo na kukiri kuwa ina uraibu mkubwa, kama wa sigara kwa liayezoea kufanyiwa. Kijana huyo naye alianzishwa mambo hayo utotoni na watu wazima katika familia yake. Katika hao watano, kila mmoja alikuwa na hadithi yake.

Sina sababu ya kutowaamini kwa sababu hayakuwa mazungumzo ya kipolisi au ya kuwahukumu bali ya kirafiki kabisa.

Kule Zanzibar na hata baadhi ya maeneo mengine, tunaambiwa, vitendo vya ulawiti wa watoto ni vingi mno. Baadhi vinang’amuliwa maopema, baadhi ya vitendo hivyo havijulikani na vinaendelea na kutengeneza mashoga.

Swali langu kwa watetezi wa LGBT, hawa nao waliingia huku kwa hiari?

Sina tatizo na mtu mzima, walau kwa uchache miaka 18 na zaidi, anayejitambua tayari, kuamua kuingiliwa kinyume akaifanya ni starehe yake lakini kuingizwa huko kupitia unyanyasaji haikubaliki.

Kwa hiyo, wakati wakina Mishy Singano, Fatma Karume na wenzao wanaowatetea mashoga wakiendeleza harakati zao, wachungulie takwimu na kuona hali mbaya ya ongezeko la vitendo vya ulawiti kwa watoto wa kiume na kike, wachunguze mchango wake katika kuzalisha mashoga (bila hiari) na wajishughulishe na mapambano hayo.

Katika habari moja niliyoiona imechapwa katika tovuti ya Shirika la Habari la Ujerumani, Deutche Welle (DW) Jeshi la Polisi limenukuliwa kuwa visa vya ukatili na dhuluma ya kingono dhidi ya watoto mwaka wa 2020 ilifikia 7263 ikiwa ni ongezeko la asilimia 26 ikilinganishwa na mwaka 2015 ambapo vilirikodiwa visa 5803, hii ikiwa ni sawa na visa 615 kwa mwezi jambo ambalo linatajwa kuwa linahatarisha mustakabali wa ustawi kwa watoto nchini humo. Dhuluma hizi za kingono ndio zinazalisha uraibu wa kupenda kuingiliwa kinyume.

Hawa vijana walioingizwa katika ushoga bila kutaka kwa kubakwa mfululizo utotoni wanapitia mateso makubwa mno. Wakienda kufanyiwa vipimo, hukutwa na hali mbaya ya kiafya, wameharibika. Starehe gani hii ya kuvunja haki za watu wengine ya kuwa na afya nzuri, eti kwa kizingizio kuwa ameridhia wakati kumbe wengi wanalazimishwa kwa kuanza kubakwa?

Jambo la pili ambalo nataka kuligusia kidogo ni hii tabia ya kutumia nguvu nyingi kupromote ushoga, jambo ambalo kusema ukweli linaathiri jamii ya LGBT kuliko kuwasaidia.

Jamii ya LGBT ilikuwepo miaka na miaka na ndio maana jambo la kuingiliana kinyume wanaume kwa wanaume au hata kwa wanaume kwa wanawake limetajwa kama dhambi kwenye dini nyingi kubwa. Zamani, hasa huku Afrika, walikuwepo walivumiliwa, kama walivyovumiliwa wengine wenye tabia zisizokubalika katika jamii.

Siku hizi upinzani dhidi yao umekuwa mkubwa kwa sababu wajiitao wanaharakati (ambao wenyewe wanapambana watoto wao wa kuwazaa wasiingie huko) wanatumia nguvu nyingi kulazimisha jamii ipende na ikumbatia tabia hizi.

Mi nadhani kwanza, wanaharakati wa LGBT waanze kuchunguza vijana wengi waliingiaje huko na wana maoni gani kwa hivi sasa? Je wangependa kusaidiwa kutoka (naamini hivyo) kwa sababu wengi wanafanya kwa uraibu, kama ilivyo kwa dawa za kulevya, sio kupenda?

Lakini, nina hakika wanaharakati wa LGBT hawawezi kufanya jambo lolote litakalopunguza idadi ya mashoga, ambao wamewafanya mradi wao wakichuma mabilioni kutoka kwa wafadhili. Wanaharakati wanapenda kutuaminisha kuwa mashoga wote wamekuwa hivyo kwa sababu ya kimaumbil.e.. sijui homoni na kadhalika.

Jamani! hivi ukiwa na homoni za kike ndio uingiliwe kinyume? Kwani kwa hao wanawake huko nyuma ni rasmi kama eneo la starehe? Mi nina hakika wanaharakati nguli wa LGBT, wakina nanihii hawajawahi kutoa ‘tigo’ kwani wanajua madhara yake ila wanahimiza watoto wa kiume wa wanawake wenzao wafyokolewe nyuma! Disgusting!

Wazazi wenzangu nawashauri tuwe waangalifu. Sibishi kuwa huenda homoni fulani huchangia kumsukuma mtu kwenye ushoga, lakini tusisahau sababu kubwa ya watoto wetu kuingia huko ni unyanyasaji wa kingono.

Wazazi, tuwachunge watoto sio tu dhidi ya manyang’au watu wazima wanaowamendea kutaka kuwabaka, lakini tuwalinde watoto wasifanyiane wao kwa wao na kuzoesha na tabia hiyo chafu.

Mwenyezi Mungu atuhifadhi na tabia asizoziridhia! Aaamiin
 
Nikuulize ivi amanibaraka baada ya hao members wa familia yako kufanya ufezuli huo, je nyie Kama familia mliwapeleka ktk vyombo vya dola ?
Members wa familian yangu ipi tena? Katika hao watano, ni mmoja tu ambaye ni ndugu yangu, mtoto wa mama mdogo, ambaye alifanyiziwa na jirani. Hapo wakati ana admit hivyo ni miaka 20 baadae, tunaanzia wapi wakati wamekuwa wakihama hama na hata hawajui hata mhusika yapo wapi kwa sasa?
 
Wewe una visa[emoji16][emoji16]
 
Kuna uthibitisho wa picha za miaka ya 1900s wanawake kwa wanawake wakioana.

Sidhani kama kuna uhusiano wa moja kwa moja wa kua shoga na kulawitiwa kwa lazima. Hii ni kwakua hata katika video za juzi tumeona jamaa akiwekwa ila alikua amedindisha.

Pia hatuna takwimu za watoto waliolawitiwa na wakawa mashoga, wala takwimu za ambao walilawitiwa na hawajawa. Hivyo madai yako ya kwamba waliopitia maisha ya kulawitiwa ni moja kwa moja wanakua mashoga sioni kama ni sahihi kwa 100%

Wakati nasoma shule ya msingi nilikua karibu na eneo linauzwa urojo watoto wengi waliingiliwa kwa kutaka kununuliwa urojo kiasi kwamba skendo ikawa kubwa jamaa akahamishwa na walimu wakatukataza kununua urojo.

Miongoni mwa ambao walikua ni case study ya wanaolawitiwa alikuepo dogo ambaye kwa sasa ni fundi makenika maarufu sana, ameoa pia. Ambacho katika saikoloji tunaweza kukithibitisha ni kwamba mtoto atakayepitia hizi sexual au physical abuse hukua akiwa na kinyongo na kujioverwork ili kucompensate yaliyowahi kutokea utotoni.

Hapa ndiyo tunakutana na mtu kama R. Kelly au Michael Jackson. Ila madai ya kwamba sexual abuse itasababisha uwe shoga nafikiri inahitajika kutafuta link ya uhakika.
 
Una mawazo kama yangu ikiwa ushoga unasababishwa na kulawitiwa utotoni vipi kuhusu usagaji?

Kulawaitiwa ndo kukufanye hata usitamani mwanamke na umtaman mwanume mwenzio? Wanawake walivyo wazuri kweli.

Ushoga na usagaji ni pande mbili za sarafu moja. Kisaikolojia hiyo hali ni aina ya disorder wale wamezaliwa hivyo hivyo na huo ulemavu basi.

Mleta mada nenda katafiti zaidi ingia hata fb kuna mashoga kibao jaribu kuwapeleleza uone walianzaje.
 
View attachment 2036928

Abuu Kauthar

Nianze kwa kuelezea uzoefu wangu katika maisha wa kukutana na kuwajua mashoga. Nianze kwa kuomba msamaha kwa jina hilo kwani sina hakika kama ni rasmi na linakubalika kwao.

Nimepata kujuana na mashoga watano. Najua kuna makundi mengi katika hao wanaojitambulisha kama jamii ya LGBT, lakini nikizungumzia mashoga ninakusudia wanaume wanaofanyiwa mapenzi kupitia tundu la nyuma, ambalo limezoeleka kama ni kwa ajili ya kutolea mavi.

Watu hao watano ninaowajua wana jambo moja linalofanana. Wote waliingia kwenye tabia hiyo utotoni baada ya kunyanyaswa kwa muda mrefu, kingono. Mmoja wapo, nilimjua katika taasisi moja ya elimu, alinambia alifanyiwa mambo hayo na baba yake mdogo, mwingine ambaye ni mdogo wangu wa mama mdogo alinyanyaswa utotoni na jirani ya.
Mwingine ni kijana wa Kiarabu kule Dodoma ambaye alikuwa rafiki wa mjomba angu, akisoma shule ya Mazengo. Mara kadhaa alimfuata mjomba kumuomba amuombee dua aache tabia hiyo na kukiri kuwa ina uraibu mkubwa, kama wa sigara kwa liayezoea kufanyiwa. Kijana huyo naye alianzishwa mambo hayo utotoni na watu wazima katika familia yake. Katika hao watano, kila mmoja alikuwa na hadithi yake.

Sina sababu ya kutowaamini kwa sababu hayakuwa mazungumzo ya kipolisi au ya kuwahukumu bali ya kirafiki kabisa.

Kule Zanzibar na hata baadhi ya maeneo mengine, tunaambiwa, vitendo vya ulawiti wa watoto ni vingi mno. Baadhi vinang’amuliwa maopema, baadhi ya vitendo hivyo havijulikani na vinaendelea na kutengeneza mashoga.

Swali langu kwa watetezi wa LGBT, hawa nao waliingia huku kwa hiari?

Sina tatizo na mtu mzima, walau kwa uchache miaka 18 na zaidi, anayejitambua tayari, kuamua kuingiliwa kinyume akaifanya ni starehe yake lakini kuingizwa huko kupitia unyanyasaji haikubaliki.

Kwa hiyo, wakati wakina Mishy Singano, Fatma Karume na wenzao wanaowatetea mashoga wakiendeleza harakati zao, wachungulie takwimu na kuona hali mbaya ya ongezeko la vitendo vya ulawiti kwa watoto wa kiume na kike, wachunguze mchango wake katika kuzalisha mashoga (bila hiari) na wajishughulishe na mapambano hayo.

Katika habari moja niliyoiona imechapwa katika tovuti ya Shirika la Habari la Ujerumani, Deutche Welle (DW) Jeshi la Polisi limenukuliwa kuwa visa vya ukatili na dhuluma ya kingono dhidi ya watoto mwaka wa 2020 ilifikia 7263 ikiwa ni ongezeko la asilimia 26 ikilinganishwa na mwaka 2015 ambapo vilirikodiwa visa 5803, hii ikiwa ni sawa na visa 615 kwa mwezi jambo ambalo linatajwa kuwa linahatarisha mustakabali wa ustawi kwa watoto nchini humo. Dhuluma hizi za kingono ndio zinazalisha uraibu wa kupenda kuingiliwa kinyume.

Hawa vijana walioingizwa katika ushoga bila kutaka kwa kubakwa mfululizo utotoni wanapitia mateso makubwa mno. Wakienda kufanyiwa vipimo, hukutwa na hali mbaya ya kiafya, wameharibika. Starehe gani hii ya kuvunja haki za watu wengine ya kuwa na afya nzuri, eti kwa kizingizio kuwa ameridhia wakati kumbe wengi wanalazimishwa kwa kuanza kubakwa?

Jambo la pili ambalo nataka kuligusia kidogo ni hii tabia ya kutumia nguvu nyingi kupromote ushoga, jambo ambalo kusema ukweli linaathiri jamii ya LGBT kuliko kuwasaidia.

Jamii ya LGBT ilikuwepo miaka na miaka na ndio maana jambo la kuingiliana kinyume wanaume kwa wanaume au hata kwa wanaume kwa wanawake limetajwa kama dhambi kwenye dini nyingi kubwa. Zamani, hasa huku Afrika, walikuwepo walivumiliwa, kama walivyovumiliwa wengine wenye tabia zisizokubalika katika jamii.

Siku hizi upinzani dhidi yao umekuwa mkubwa kwa sababu wajiitao wanaharakati (ambao wenyewe wanapambana watoto wao wa kuwazaa wasiingie huko) wanatumia nguvu nyingi kulazimisha jamii ipende na ikumbatia tabia hizi.

Mi nadhani kwanza, wanaharakati wa LGBT waanze kuchunguza vijana wengi waliingiaje huko na wana maoni gani kwa hivi sasa? Je wangependa kusaidiwa kutoka (naamini hivyo) kwa sababu wengi wanafanya kwa uraibu, kama ilivyo kwa dawa za kulevya, sio kupenda?

Lakini, nina hakika wanaharakati wa LGBT hawawezi kufanya jambo lolote litakalopunguza idadi ya mashoga, ambao wamewafanya mradi wao wakichuma mabilioni kutoka kwa wafadhili. Wanaharakati wanapenda kutuaminisha kuwa mashoga wote wamekuwa hivyo kwa sababu ya kimaumbil.e.. sijui homoni na kadhalika.

Jamani! hivi ukiwa na homoni za kike ndio uingiliwe kinyume? Kwani kwa hao wanawake huko nyuma ni rasmi kama eneo la starehe? Mi nina hakika wanaharakati nguli wa LGBT, wakina nanihii hawajawahi kutoa ‘tigo’ kwani wanajua madhara yake ila wanahimiza watoto wa kiume wa wanawake wenzao wafyokolewe nyuma! Disgusting!

Wazazi wenzangu nawashauri tuwe waangalifu. Sibishi kuwa huenda homoni fulani huchangia kumsukuma mtu kwenye ushoga, lakini tusisahau sababu kubwa ya watoto wetu kuingia huko ni unyanyasaji wa kingono.

Wazazi, tuwachunge watoto sio tu dhidi ya manyang’au watu wazima wanaowamendea kutaka kuwabaka, lakini tuwalinde watoto wasifanyiane wao kwa wao na kuzoesha na tabia hiyo chafu.

Mwenyezi Mungu atuhifadhi na tabia asizoziridhia! Aaamiin
Mungu akubariki sana mleza uzi na Mungu ambariki sana mwandishi.
Huu ushetani tusipoupigia kelele, miaka michache ijayo tutakuwa na taifa la hovyo kupindukia.
Tukiendelea kuufumbia macho huu ushetani, ipo siku ghadhabu ya Mungu itashuka kwetu kama ilivyoshuka kwa Sodoma na Ghomora.
 
Kama jamii tunapaswa kuanzia hapa ili kuwalinda watoto wetu chini ya miaka 18..

ukibainikia kulawiti kijana chini ya miaka 18 na ushahidi uko live, ni kunyongwa mpaka kufa kwa haraka...Huko majumbani ukijua ndugu yako ametenda huo uovu mripoti haraka hakuna kukaa na kuyamaliza msongesheni akanyongwe chap....mhusika aliyetendewa apewe matibabu na kuwa chini ya uangalizi ikiwa pamoja na counceling za hapa na pale..

Wale watu wazima walioamua kuingia huko, ni vyema wakapewa elimu juu ya watendayo na zisiwepo NGOs za kupromote na kuwaambia wajikubali sijui nini hapana...wahubiri misikitini na makanisani wahubiri juu ya ubaya wa hayo matendo..na jamii nzima iwakatae baada ya kuwapromote...
 
ushoga ni choice/maamuzi ya mtu katika maisha, Mimi naona hakuna link yoyote Kati ya mtoto anayefi.rwa muda mrefu na kuwa shoga ila tu akiamua na kupenda kuendelea kuingiliwa ful stop sababu hata hiyo addiction/uraibu/uteja nao ni maamuzi ya kuendelea kuwa hivyo. Je unajua siku hizi kuna kitu kinaitwa prostate massage watu wanafanya either kwa kujua au kutokujua lakini ni sexual fantasy ambayo ni nusu ya ushoga watu wanafanya wanafurahia faragha yao kwaiyo hili suala linahitaji mjadala mpana zaidi kuliko huo mtazamo finyu ulioutumia
 
Haya mambo ni ya kiroho!
Ni spirit zinazofanya kazi nyuma yake kuna madahabahu, so,sio rahisi kuacha tu bila kukutana na nguvu ya Mungu hawa watu!
 
Kuna uthibitisho wa picha za miaka ya 1900s wanawake kwa wanawake wakioana.

Sidhani kama kuna uhusiano wa moja kwa moja wa kua shoga na kulawitiwa kwa lazima. Hii ni kwakua hata katika video za juzi tumeona jamaa akiwekwa ila alikua amedindisha.

Pia hatuna takwimu za watoto waliolawitiwa na wakawa mashoga, wala takwimu za ambao walilawitiwa na hawajawa. Hivyo madai yako ya kwamba waliopitia maisha ya kulawitiwa ni moja kwa moja wanakua mashoga sioni kama ni sahihi kwa 100%

Wakati nasoma shule ya msingi nilikua karibu na eneo linauzwa urojo watoto wengi waliingiliwa kwa kutaka kununuliwa urojo kiasi kwamba skendo ikawa kubwa jamaa akahamishwa na walimu wakatukataza kununua urojo.

Miongoni mwa ambao walikua ni case study ya wanaolawitiwa alikuepo dogo ambaye kwa sasa ni fundi makenika maarufu sana, ameoa pia. Ambacho katika saikoloji tunaweza kukithibitisha ni kwamba mtoto atakayepitia hizi sexual au physical abuse hukua akiwa na kinyongo na kujioverwork ili kucompensate yaliyowahi kutokea utotoni.

Hapa ndiyo tunakutana na mtu kama R. Kelly au Michael Jackson. Ila madai ya kwamba sexual abuse itasababisha uwe shoga nafikiri inahitajika kutafuta link ya uhakika.
Kulawitiwa kwa mda mrefu
 
ushoga ni choice/maamuzi ya mtu katika maisha, Mimi naona hakuna link yoyote Kati ya mtoto anayefi.rwa muda mrefu na kuwa shoga ila tu akiamua na kupenda kuendelea kuingiliwa ful stop sababu hata hiyo addiction/uraibu/uteja nao ni maamuzi ya kuendelea kuwa hivyo. Je unajua siku hizi kuna kitu kinaitwa prostate massage watu wanafanya either kwa kujua au kutokujua lakini ni sexual fantasy ambayo ni nusu ya ushoga watu wanafanya wanafurahia faragha yao kwaiyo hili suala linahitaji mjadala mpana zaidi kuliko huo mtazamo finyu ulioutumia
Unazungumzia mtoto wa kuanzia hadi miaka 7 afanyiwe hivyo for years.., Unadhani ni rahisi ku break from hiyo tabia baada ya kufanyiwa kwa miaka?
 
I give up brother (or sister) 🙌
Usigive up.

We live in a golden era kila unachokifikiria kimeshafanyiwa utafiti badala ya kugive up zama chimbo tafuta sources zitakazoconfirm madai yako.

That way utakua unatuelimisha ambao hatujui huku na wewe ukielimika na huku tukiendelea kubadilishana maoni.
 
Unazungumzia mtoto wa kuanzia hadi miaka 7 afanyiwe hivyo for years.., Unadhani ni rahisi ku break from hiyo tabia baada ya kufanyiwa kwa miaka?
haimfanyi akawa shoga, Je ukiangalia hawa watu waliofanyiwa hivyo vitendo utoto na wakawa mashoga kulinganisha na idadi ya watu hao kudhibitisha kuwa mashoga wote walitokana na hivyo vitendo?
 
Usibishe sana kwa hawa wanaofanyiwa hivi vitendo kwa kipindi kirefu.
Kuna binti mmoja alikua anajieleza kua hua anaenjoy zaidi kwa mpalange kuliko mbele.
Katika maelezo yake alidai kua boyfriend aliempenda ndio aliemuanzishia huo upuuzi, mwanzo alikua anapata maumivu sana ila taratibu mpaka akazoea, na kwa maelezo yake mwenyewe anadai kwa sasa hua anaenjoy zaidi nyuma kuliko mbele.
Huyu ni mwanamke anaejua utamu wa mbele na nyuma, na kwa maelezo yake anadai raha na msisimko zaidi upo nyuma.
Kikubwa ni kuwalinda watoto wote wa kike na kiume, kuwafundisha dini ili wawe na hofu ya Mungu na kumuomba sana Mungu awalinde na hii dhambi inayochipukia kwa kasi sana zama hizi.
 
Je wanaowaingilia wanaume wenzao nao wanaitwa mashoga? Maana kwa kiingereza "gay" ina maanisha mtiwaji na mtiaji?
 
Back
Top Bottom