Nawakumbusha tu zimebaki Siku 4 tu ili JWTZ waanze Msako wa Nguo zinazofanana na Sare zao Majumbani na Mitaani

Sare za JWTZ sio makombati tuu ya mabaka mabaka... kuna zile sketi na shati au suruali na shati rangi onakua kama dark blue na sharti la dark blue.... hizi itakuaje?
Na zingine hazifanani na combati ya Tz ila zinafanan na combati ya Ghan. Je wanazitaka na hizi?
 
Nina viatu, kalamu, vesti, handchief, tshirt, shati, bajaj nimeiremba mabakabaka, mpaka mwanangu ana nguo na kofia za mabakabaka. Ila hayo mabaka ni ya majeshi ya nchi za nje, nguo zingine nimezununua mitumbani sijui kama hao JWTZ watadai ni sare zao wakati hazina ufanano kimabaka
Kwa mfano, Arusha kuna viatu vingi sana maduka ya mtumba ziko boot kama za jeshi lakini siyo jeshi hili, sisi tunaita American boot, au jungle boot , nazo watasema ni zao?
 
Ilimradi chochote kile, iwe nguo yenye mabaka yanayofanana na zao au hata za nchi za nje🤦🏾🤦🏾🤦🏾
Kwanini halisimamiwi na sheria na badala yale wanasimamia wao? Ikitokea madhara tutamlaum nani?
 
Msije tu kusema kuwa Mzalendo Halisi GENTAMYCINE sikuwakumbusheni juu ya hili na Taarifa hii pia.

Na wamesema Siku zao Saba za Huruma na Kuzisalimisha Kwao zikiisha tu Wakikumata nazo kwa Watakachokufanya unaweza hata ukashindwa kutoa Haja Kubwa ( Kuukweka ) kwa miaka mitano na utajua Mwenyewe utaitolea wapi.

Shikamooni JWTZ akina Poti wangu.
si wasake wezi na wala rushwa.
 
du haya.
 
Nina viatu, kalamu, vesti, handchief, tshirt, shati, bajaj nimeiremba mabakabaka, mpaka mwanangu ana nguo na kofia za mabakabaka. Ila hayo mabaka ni ya majeshi ya nchi za nje, nguo zingine nimezununua mitumbani sijui kama hao JWTZ watadai ni sare zao wakati hazina ufanano kimabaka
Huruhusiwi kufanana nguo na jeshi lolote la Tanzania
 
Watafutiwe vita waende pigana na wababe wenzao huko...
 
Nina viatu, kalamu, vesti, handchief, tshirt, shati, bajaj nimeiremba mabakabaka, mpaka mwanangu ana nguo na kofia za mabakabaka. Ila hayo mabaka ni ya majeshi ya nchi za nje, nguo zingine nimezununua mitumbani sijui kama hao JWTZ watadai ni sare zao wakati hazina ufanano kimabaka
mkuuu wamesema nguo zoote hata za majeshi mengine hutakuwi kuwa Nazi wewe RAIA,zipeleke serikali ya mtaa

yasije kukupata mazito
 
Msije tu kusema kuwa Mzalendo Halisi GENTAMYCINE sikuwakumbusheni juu ya hili na Taarifa hii pia.

Na wamesema Siku zao Saba za Huruma na Kuzisalimisha Kwao zikiisha tu Wakikumata nazo kwa Watakachokufanya unaweza hata ukashindwa kutoa Haja Kubwa ( Kuukweka ) kwa miaka mitano na utajua Mwenyewe utaitolea wapi.

Shikamooni JWTZ akina Poti wangu.
Washindwe kusaka wauwaji kibiti waweze kuingia majumbani mwa watu kutafuta nguo zinazofanana na sare zao kweli kuna maajabu. Kwanza wangekataza nguo hizo kuingia kama mitumba au nguo spesho alafu ndio watoe katazo lao. Sasa wanatuuzia mtumbani alafu uswahilini wanatumendea. Nchi ngumu sana hii
 
Sare za JWTZ sio makombati tuu ya mabaka mabaka... kuna zile sketi na shati au suruali na shati rangi onakua kama dark blue na sharti la dark blue.... hizi itakuaje?
Hizi za walinzi wa makampuni hazina shida
 
Mm nina boksa ya bakabaka nani atanichungulia kuona boksa yangu??

Wanamaindi mambo ya ajabu sana.!!
 
Back
Top Bottom