Nawakumbusha tu zimebaki Siku 4 tu ili JWTZ waanze Msako wa Nguo zinazofanana na Sare zao Majumbani na Mitaani

Vilevile Kuna Majaketi ya mabaka baka nawaona polisi na magereza wanavaa, lakini pia wale KMKM mavazi Yao ni kama JW! Hao vipi tangazo linawahusu?
 
Acha uoga,nawewe unaamini wataingia ndani mwako waanze kuzisaka?
Tulia,acha uoga.
 
Inabidi waje Wagner group kwanza ili wawe busy kidogo
 
Yaani ukasake nguo zako,kwa askari magereza?Ili?
Vilevile Kuna Majaketi ya mabaka baka nawaona polisi na magereza wanavaa, lakini pia wale KMKM mavazi Yao ni kama JW! Hao vipi tangazo linawahusu?
 
Nina viatu, kalamu, vesti, handchief, tshirt, shati, bajaj nimeiremba mabakabaka, mpaka mwanangu ana nguo na kofia za mabakabaka. Ila hayo mabaka ni ya majeshi ya nchi za nje, nguo zingine nimezununua mitumbani sijui kama hao JWTZ watadai ni sare zao wakati hazina ufanano kimabaka
Usitafute matatizo wacha matatizo yakufuate yenyewe
 
Msije tu kusema kuwa Mzalendo Halisi GENTAMYCINE sikuwakumbusheni juu ya hili na Taarifa hii pia.

Na wamesema Siku zao Saba za Huruma na Kuzisalimisha Kwao zikiisha tu Wakikumata nazo kwa Watakachokufanya unaweza hata ukashindwa kutoa Haja Kubwa ( Kuukweka ) kwa miaka mitano na utajua Mwenyewe utaitolea wapi.

Shikamooni JWTZ akina Poti wangu.
Katika Jf watu smart wanaotrendisha maudhui ya thread ama comments zao ni pamoja na wewe Genta.

Sasa basi kwa thread hii naona kama wamekuhac, si yako, ni yako kweli hii!

Suala hili tuliliongea sana juzi lilipozagaa mitandaoni na tunaopenda utawala bora na wa sheria tuliliona suala hili kuwa lina ukakasi na kasoro kubwa za kisheria, tukatoa maoni na kila mtu akatoa maoni yake.

Ingawa huwa hatufikii conclusion, lakini uzi ukikosa muhu ya wachangiaji uelewe jambo hilo limeeleweka, sasa nimeshangaa wewe kuliibua tena upya!

Sasa tuvumiliane!

Tulisema hivii?:
Kauli aliyoitoa msemaji wa jeshi, ilitolewa bila maandalizi na ni kauli yenye harufu ya kisiasa baada ya kuainisha mambo kadhaa.

Msemaji alisema hairuhusiwi raia kutumia nguo za jeshi ama zenye kufanana nazo, si ndiyo?

Sasa kauli kama hiyo ukiichambua, tamko hilo linaiingiza nchi kwenye mtafaruku mkubwa.

Tangu lini na ni sheria gani inaruhusu wanajeshi kumaintain misako mitaani na kufanya kazi za Polisi wakati wa amani ama wakati nchi haipo kwenye hali ya hatari(state of emergency)?

Pia rangi za jeshi zinazotumiwa na majeshi yetu ni nyingi kuliko tunavyodhania, kuna nyeupe, nyeusi, nyekundu, bluu, bluu bahari, kijani, kijani mpauko, kijivu mkolezo, kijivu mpauko, khaki mkolezo, khaki mpauko, njano, ugoro nk nk ambapo siwezi kuzikumbuka zote.

Pia tukauliza, hizo rangi wanazotumia wanajeshi kisheria wana haki miliki nazo na kama wana haki miliki, ni rangi gani hasa?

Msemaji mkuu wa jeshi aliulizwa swali rahisi toka kwa muandishi wa habari, lakini alishindwa kulijibu swali hilo rahisi hadi nikashangaa kwa sababu jambo hilo lipo kwenye vitabu vya sheria za msingi za jeshi(The defence forces regulations Vol.1)ambazo yeye alikuwa amesimama kuzitetea.

Aliulizwa kuhusu wasanii wanaoonekana kupenda kucheza na nguo zinazofanana na za jeshi.

Ambapo jibu lake lingelikuwa ni fupi na jepesi tu kuwa: "wasanii ama waigizaji wanaopenda kutumia mavazi ama vifaa vya kijeshi hutakiwa kupeleka maombi yao Makao makuu ya jeshi kwa hatua ya kibali".

Kwa hiyo hapo hakuna marufuku ya jumla jumla, ila ni "kwa kibali".

Sisi tunaelewa hivii, kama jambo flani ama kitu flani ni mali halali ya wananchi kisheria, na wakati huo Serikali ikazihitaji kuzitumia, basi kuna taratibu hufanywa za kuwalipa fidia waathirika ili Serikali iwe na uhalali wa kuhodhi mali hiyo moja kwa moja.

Kwa mfano, tumeona kwenye ujenzi wa barabara, reli nk nk namna wananchi wanavyolipwa fidia.

Kwenye jambo hili, ukakasi wake unakuja kwa sababu watu wana leseni halali za kufanya biashara za mitumba, vitambaa vya suti vyenye rangi za jeshi alizodai yeye kupiga marufuku.

Je kwa tangazo hilo Serikali imejiandaaje kulipa fidia za mitumba na vitambaa vya nguo halali kutoka kwa wafanya biashara halali wanazofanya wananchi?

Kutoa kauli ya jumla jumla namna hiyo kwamba wenye nguo hizo "wakazisalimishe" bila kuweka bayana wakazisalimishe wapi ni kauli inayoweza kuleta uvunjifu wa amani!

Nguo za rangi ya jeshi kama nilivyoeleza hapo juu ni nyingi mno (thouthans of metric tones) za vitambaa na mitumba wanazohodhi kwenye maghala na maduka ya wafanyabiashara hivi sasa, kwa hiyo ni lazima iainishwe kila Mkoa na kila Wilaya sehemu walipoandaa "base" za kupokelea marobota hayo ya nguo, pia na utaratibu wa kuwalipa fidia wafanya biashara hao namna ulivyoandaliwa.

Tunaofuatilia mwenendo wa siasa za hapa nchini, jambo hili limeanza hivi karibuni baada ya Mbowe kuonekana siku moja akihutubia mkutano flani, nyuma akawa na mpambe wake aliyevalia mavazi yenye kufanana na mavazi ya jeshi, ndipo matamko haya yakaanza kutoka kwenye vinywa vya wanausalana wetu.

Kwa hiyo hapo wanajeshi wanatumiwa na wanasiasa aidha kwa kutokujua ama kwa kujua.

Mtu yeyote anayejisikia kuvaa nguo zenye kufanana na za jeshi, atakuwa hana kosa la kuvunja sheria yoyote kwa sababu nguo hizo kazipata kwa njia "halali"(katika mzunguko wa biashara na uchumi).

Hilo katazo ni haramu kwa sababu limeandaliwa kwa hila za kisiasa zaidi.

Lingelikuwa ni halali, basi Jwtz wangetoka na cheti cha haki miliki (brand) yao kuonesha umma kwamba baka baka la mfumo huu na lenye rangi hii, tunamiliki sisi jeshi kisheria pamoja na rangi hizi kadhaa (plain) pia zinamilikiwa na jeshi katika taratibu zetu za mavazi ya kila siku.

Mbona kule "majuu" kuna maduka ya wazi ya nguo hizo na kila raia anaruhusiwa kujinunulia, isipokuwa za jeshi zinakuwa na brand yake na haki miliki yao.

Wanajeshi huenda kununua kwenye maduka hayo kwa maelekezo ya brand zao ambazo wananchi wanazitambua.

Ingawa hapa nchini jeshi letu linavishwa kwa zabuni, je halijui kuwa nguo zinazofanana na za jeshi si nguo za jeshi, bali ni nguo za kiraia ambazo si mali ya serikali(jeshi)?

Kwa mkanganyiko huu wa kisheria, tunaomba Jeshi letu, liitishe tena vyombo vya habari ili kufafanua ukakasi uliojitokeza kwenye tangazo lao hilo, pia wawaombe radhi wananchi kwa kutoa matangazo ya jumla jumla yenye kuleta mtafaruku wa kibiashara(kiuchumi), kijamii na kisiasa.
 
Msije tu kusema kuwa Mzalendo Halisi GENTAMYCINE sikuwakumbusheni juu ya hili na Taarifa hii pia.

Na wamesema Siku zao Saba za Huruma na Kuzisalimisha Kwao zikiisha tu Wakikumata nazo kwa Watakachokufanya unaweza hata ukashindwa kutoa Haja Kubwa ( Kuukweka ) kwa miaka mitano na utajua Mwenyewe utaitolea wapi.

Shikamooni JWTZ akina Poti wangu.
Mkuu

Kama hili tamko ni la kweli Bas kuna jambo jingine zaidi ya hilo!!

YAANI tutazoeshwa doria za kijeshi mtaani kama baadhi ya nchi kwa malengo Maalum!

Yaani

Jeshi la polisi limeshindwa!?hadi wajeda waingie kazini!!?

Hapa kuna sababu zinatafutiwa kuhalalisha JAMBO jingine!!

NAFSI inanibia siamini kama dp world ime signal JAMBO hili!!

Ukiona wajeshi kwa doria kama hivyo wanavotaka kufanya Bas ni dhahiri kuna JAMBO wanalitaka ambapo wa kwenda deep wanajua!!

Mawazo huru haya ya mlipa kodi asiekwepa!

"Rais ambae hajawahi kugombea ilitokea marekani itatokea na huku" Tumia akili!

Pia

"Operation iliyositishwa ipo on, desert mission"baadhi ya maneno kwenye uzi wa juzi wa Tumia akili"moderators walimeza uzi ule!!!!

Mawazo huru haya!
 
Wameacha kazi yao ya msingi kulinda mipaka ya nchi yetu ikiwemo bandari wanadeal na petty isues.

Ama hawana kazi ya kufanya tuombe friend war na Rwanda hapo wazichape kidogo
 
Msije tu kusema kuwa Mzalendo Halisi GENTAMYCINE sikuwakumbusheni juu ya hili na Taarifa hii pia.

Na wamesema Siku zao Saba za Huruma na Kuzisalimisha Kwao zikiisha tu Wakikumata nazo kwa Watakachokufanya unaweza hata ukashindwa kutoa Haja Kubwa ( Kuukweka ) kwa miaka mitano na utajua Mwenyewe utaitolea wapi.

Shikamooni JWTZ akina Poti wangu.
Waende huko bandarini zinapoingilia ili wazuie huko.
 
Mkuu

Kama hili tamko ni la kweli Bas kuna jambo jingine zaidi ya hilo!!

YAANI tutazoeshwa doria za kijeshi mtaani kama baadhi ya nchi kwa malengo Maalum!

Yaani

Jeshi la polisi limeshindwa!?hadi wajeda waingie kazini!!?

Hapa kuna sababu zinatafutiwa kuhalalisha JAMBO jingine!!

NAFSI inanibia siamini kama do world ime signal JAMBO hili!!

Ukiona wajeshi kwa doria kama hivyo wanavotaka kufanya Bas ni dhahiri kuna JAMBO wanalitaka ambapo wa kwenda deep wanajua!!

Mawazo huru haya ya mlipa kodi asiekwepa!

"Rais ambae hajawahi kugombea ilitokea marekani itatokea na huku" Tumia akili!

Pia

"Operation iliyositishwa ipo on, desert mission"baadhi ya maneno kwenye uzi wa juzi wa Tumia akili"moderators walimeza uzi ule!!!!

Mawazo huru haya!
desert mission imekuwa hatari sana mkuu, wacha tuone inaishaje
 
Uwezo wa kufikiri kwa binadam wa Tz ni tofauti na mataifa mengine?, Hivi hawa mapoti hili nalo ni Jambo la kuhangaika nalo?. Wanashindwa kulinda Mali zetu wanakuja kuhangaika na upuuzi huu?, 2025 ntagombea ubunge nauhakika nitashinda na ntapelaka mswaada Bungeni kuomba kila baada ya miezi 6 poti wetu wapate mapambano ya kirafiki.
 
Kuna dogo wa bajaji alfungulia mziki kwa sauti kubwa halafu akapita kwenye kambi ya jeshi hapa Mbeya. Walipomkamata wakamuuliza, "Flash yako ina nyimbo ngapi dogo?" Dogo akajibu zipo 180. Wakamwambia aweke sikio lake kwenye subwoofer huku akifungulia mpaka mwisho sauti mpaka nyimbo zote ziishe. Cheza na vitu vyote lakini sio "wajomba"
 
desert mission imekuwa hatari sana mkuu, wacha tuone inaishaje
Inaonekana desert ni huku sio kule kisiwani na matamko yameanza!

Ina maana kama jamaa wamepoteza imani na jeshi la polisi je Wana imani na anaeamuru majeshi yote!!?

"Next time baada ya operation yao wakagundua baadhi ya vitu si watasema jeshi la polisi halitimizi wajibu wake ipasavyo coz haliongozwi vizuri na anahitajika mwenye uwezo wa kuliongoza vizuri na wakaongeza kwamba Wana imani na waziri wa ulinzi anao uwezo wa kuliongoza vizuri jeshi lote!

"Na wakaamuru mamlaka ya uteuzi iteue makam mwenye uwezo huo,halafu baadae waseme huyu anafaa kua kiongozi mkuu wa kuliamuru jeshi!!!!!

Najaribu kuwaza!!
 
Katika Jf watu smart wanaotrendisha maudhui ya thread ama comments zao ni pamoja na wewe Genta.

Sasa basi kwa thread hii naona kama wamekuhac, si yako, ni yako kweli hii!

Suala hili tuliliongea sana juzi lilipozagaa mitandaoni na tunaopenda utawala bora na wa sheria tuliliona suala hili kuwa lina ukakasi na kasoro kubwa za kisheria, tukatoa maoni na kila mtu akatoa maoni yake.

Ingawa huwa hatufikii conclusion, lakini uzi ukikosa muhu ya wachangiaji uelewe jambo hilo limeeleweka, sasa nimeshangaa wewe kuliibua tena upya!

Sasa tuvumiliane!

Tulisema hivii?:
Kauli aliyoitoa msemaji wa jeshi, ilitolewa bila maandalizi na ni kauli yenye harufu ya kisiasa baada ya kuainisha mambo kadhaa.

Msemaji alisema hairuhusiwi raia kutumia nguo za jeshi ama zenye kufanana nazo, si ndiyo?

Sasa kauli kama hiyo ukiichambua, tamko hilo linaiingiza nchi kwenye mtafaruku mkubwa.

Tangu lini na ni sheria gani inaruhusu wanajeshi kumaintain misako mitaani na kufanya kazi za Polisi wakati wa amani ama wakati nchi haipo kwenye hali ya hatari(state of emergency)?

Pia rangi za jeshi zinazotumiwa na majeshi yetu ni nyingi kuliko tunavyodhania, kuna nyeupe, nyeusi, nyekundu, bluu, bluu bahari, kijani, kijani mpauko, kijivu mkolezo, kijivu mpauko, khaki mkolezo, khaki mpauko, njano, ugoro nk nk ambapo siwezi kuzikumbuka zote.

Pia tukauliza, hizo rangi wanazotumia wanajeshi kisheria wana haki miliki nazo na kama wana haki miliki, ni rangi gani hasa?

Msemaji mkuu wa jeshi aliulizwa swali rahisi toka kwa muandishi wa habari, lakini alishindwa kulijibu swali hilo rahisi hadi nikashangaa kwa sababu jambo hilo lipo kwenye vitabu vya sheria za msingi za jeshi(The defence forces regulations Vol.1)ambazo yeye alikuwa amesimama kuzitetea.

Aliulizwa kuhusu wasanii wanaoonekana kupenda kucheza na nguo zinazofanana na za jeshi.

Ambapo jibu lake lingelikuwa ni fupi na jepesi tu kuwa: "wasanii ama waigizaji wanaopenda kutumia mavazi ama vifaa vya kijeshi hutakiwa kupeleka maombi yao Makao makuu ya jeshi kwa hatua ya kibali".

Kwa hiyo hapo hakuna marufuku ya jumla jumla, ila ni "kwa kibali".

Sisi tunaelewa hivii, kama jambo flani ama kitu flani ni mali halali ya wananchi kisheria, na wakati huo Serikali ikazihitaji kuzitumia, basi kuna taratibu hufanywa za kuwalipa fidia waathirika ili Serikali iwe na uhalali wa kuhodhi mali hiyo moja kwa moja.

Kwa mfano, tumeona kwenye ujenzi wa barabara, reli nk nk namna wananchi wanavyolipwa fidia.

Kwenye jambo hili, ukakasi wake unakuja kwa sababu watu wana leseni halali za kufanya biashara za mitumba, vitambaa vya suti vyenye rangi za jeshi alizodai yeye kupiga marufuku.

Je kwa tangazo hilo Serikali imejiandaaje kulipa fidia za mitumba na vitambaa vya nguo halali kutoka kwa wafanya biashara halali wanazofanya wananchi?

Kutoa kauli ya jumla jumla namna hiyo kwamba wenye nguo hizo "wakazisalimishe" bila kuweka bayana wakazisalimishe wapi ni kauli inayoweza kuleta uvunjifu wa amani!

Nguo za rangi ya jeshi kama nilivyoeleza hapo juu ni nyingi mno (thouthans of metric tones) za vitambaa na mitumba wanazohodhi kwenye maghala na maduka ya wafanyabiashara hivi sasa, kwa hiyo ni lazima iainishwe kila Mkoa na kila Wilaya sehemu walipoandaa "base" za kupokelea marobota hayo ya nguo, pia na utaratibu wa kuwalipa fidia wafanya biashara hao namna ulivyoandaliwa.

Tunaofuatilia mwenendo wa siasa za hapa nchini, jambo hili limeanza hivi karibuni baada ya Mbowe kuonekana siku moja akihutubia mkutano flani, nyuma akawa na mpambe wake aliyevalia mavazi yenye kufanana na mavazi ya jeshi, ndipo matamko haya yakaanza kutoka kwenye vinywa vya wanausalana wetu.

Kwa hiyo hapo wanajeshi wanatumiwa na wanasiasa aidha kwa kutokujua ama kwa kujua.

Mtu yeyote anayejisikia kuvaa nguo zenye kufanana na za jeshi, atakuwa hana kosa la kuvunja sheria yoyote kwa sababu nguo hizo kazipata kwa njia "halali"(katika mzunguko wa biashara na uchumi).

Hilo katazo ni haramu kwa sababu limeandaliwa kwa hila za kisiasa zaidi.

Lingelikuwa ni halali, basi Jwtz wangetoka na cheti cha haki miliki (brand) yao kuonesha umma kwamba baka baka la mfumo huu na lenye rangi hii, tunamiliki sisi jeshi kisheria pamoja na rangi hizi kadhaa (plain)zinazomilikiwa na jeshi katika taratibu zao za mavazi ya kila siku.
Mbona kule "majuu" kuna maduka ya wazi ya nguo hizo na kila raia anaruhusiwa kununua,isipokuwa jeshi linakuwa na brand yake na haki miliki ya ngo zake.

Wanajeshi huenda kununua kwenye maduka hayo kwa maelekezo ya brand zao ambazo wananchi wanazitambua.

Ingawa hapa nchini jeshi letu linavishwa kwa zabuni, je halijui kuwa nguo zinazofanana na za jeshi si nguo za jeshi, bali ni nguo za kiraia ambazo si mali ya serikali(jeshi)?

Kwa mkanganyiko huu wa kisheria, tunaomba Jeshi letu, liitishe tena vyombo vya habari ili kufafanua ukakasi uliojitokeza kwenye tangazo lao hilo, pia wawaombe radhi wananchi kwa kutoa matangazo ya jumla jumla yenye kuleta mtafaruku wa kibiashara(kiuchumi), kijamii na kisiasa.
Wakikumata na Nguo zifananazo na Sare zao utawaeleza yote haya kwa Kirefu huku wakiwa Wanakutizama tu?
 
Mimi nimesema kwa mujibu wa "kisheria" zaidi.

Ebo! Kwa hiyo wakikukamata wanatakiwa wajichukulie sheria mkononi, kwa faida ya nani?

Wayajua madhara na matokeo ya kujichukulia sheria mkononi kwa mambo kama hayo mbele za sheria?

Lakini pia si unaelewa kuwa ni mwiko na ni marufuku wanajeshi kuwaweka mahabusu zao za jeshi raia?

Maana yake hapo mtuhumiwa akidinda kwa kujua sheria, ama watamwachia au kama ni lazima watampeleka Polisi na kisha mahakamani sehemu ambayo ubabe hushushwa kwa maswali magumu ya kisheria toka kwa kina "wakili msomi".

Na ikifikia hapo "walalamikaji" huanza "kukataana" au kutafuta sababu za kuliondoa shauri hilo mahakamani ikiwemo kutelekeza kesi.
 
Wapo busy na nguo wakati wahuni wanachukua Bandari Dunia ya kisasa mambo ya nguo ni ya kizamani sana enzi za Mwalimu na sio sasa ukiona huyo mtu anaongelea nguo na rangi jua bado yupo zama za Mwalimu...
 
Back
Top Bottom