Nawalaumu sana Hamas, Serikali ya Israeli pamoja na wale wanaowaunga mkono

Nawalaumu sana Hamas, Serikali ya Israeli pamoja na wale wanaowaunga mkono

Nasubiri faida ambazo watapata HAMAS baada ya vita kuisha!!!
Waulize Israel wafanya kaxi 200,000 kwanini hawana kazi kwa sasa?

Waulize Israel hasara ngapi walizo zipata toka vita ianze

Waulize Israel nani anaye chukua video kwa karibu hivi kama sio wanajeshi wa Israel, ili kuwapelekea ujumbe waisrael tuokoeni tunamalizwa na Hamasi haswa hio video nimeweka chini.

Zingine tunajua ni Hamasi ndio anarecord, hata Aljazeera wanasema hi video kuonyesha askari wanamsaidia mwenzao na kwa karibu ni lazima jeshi la Israel wameivujisha, ili wananchi waisrael wawasaidie vita isimamishwe 😄

View: https://youtu.be/lAwMpISRZlw?si=qnqiFOKZprIaOMt8
 
Huko Darfur maelfu na maelfu watoto na wanawake wanauwawa na displaced tena ni waislam na waafrika weusi ila dah hawana thamani kama mipalestina
Hayo yote hayafai , umwagaji wa damu bila sababu za msingi ni moja Kati ya mazambi ya juu kabisa , na sijui umetumia kigezo kipi kusema hazina thamani au kisa attention ndogo kwani haujui kuwa case ni tofauti?

Mbona huku bongo watu wengi wanauwana halafu kifo cha Joshua watu wanapaza sauti kuliko na kuonyesha machungu au wanaouwawa huku Mbagala na Buza hawana thamani mbona haujawahi kuwatetea na kuwapigania ?
 
Moja kwa moja..

1. Kwa nini nawalaumu Hamas ?

Sikatai ukweli kwamba Raia wa Palestine wameishi kwa mateso miaka mingi chini ya utawala wa Wazayuni,wakiuwawa kunyimwa haki za msingi nk na nakubali kwamba wanayo haki ya kupambana katika kujikomboa na madhila wanayopitia.

Ninapowapinga ni njia ambazo wanatumia katika kujikomboa asilimia kubwa napingana nazo kwani zimeleeta maafa makubwa kwa Raia wao baada ya ukombozi ,kwani naamini matokeo ndio hujulisha faida ya Jambo na kama wanataka ukombozi wa kweli ingekuwa bora kwao kujipanga kwa nguvu zote kiimani ,kimbinu na mikakati silaha nk na sio kukurupuka tu na kushambulia ambapo matokeo yake kila siku yanaonekana maafa yanayopatikana ni makubwa zaidi kukiko faida.

Wawe na huruma na raia wao hakuna sifa wala wema kwa watu wachache kusababisha vifo na maafa makubwa kwa watu wao hiyo no hasara kubwa sana hata Mimi nikijiona sina nguvu na nikitunisha misuli nitapata madhara makubwa sana nitakubali kuishi kinyonge huku nikijipanga kisasawa mpaka pale nitakapokuwa na uhakika kuwa sasa ninaweza kushinda.

Lawama sehemu ya pili
Hapa ninazungumzia suala zima la kukamata raia wasio na hatia ,kuua ,kutesa nk ,hili swala napinga moja kwa moja hata ikiwa adui anafanya hivyo dhidi yako lakini haipaswi adui tena muovu awe mwalimu wako ,kwani hata Sheria za Uislamu inaelekeza vyema katika mapambano ikitokea vita hairuhisiwi kuua watoto wadogo ,wazee ,wanawake ,kuharibu mwili wa marehemu na kuudhihaki baada ya kukata Moto,kuharibu mashamba ,majengo nk pamoja na kuua wale wasiokushambulia na wanataka Amani.

View attachment 2845883

2. Kwa nini nailamu Serikali ya Israel?
Hawa kwa miaka mingi wamekuwa wakiwafanyia unyama na udhalimu Raia wa Palestine ,pamoja na kufanya collective punishment kwa Raia wa Palestine kwa mwamvuli wa kuwaua magaidi hii sio sawa kabisa wanafanya ugaidi wa wazi

View attachment 2845884

Huku ni westbank hakuna Hamas

View attachment 2845886

View attachment 2845885

Summary ya idadi ya mauaji kwa Raia wa Palestina tokea zamani kabla ya hata Hamas kuwepo.

View attachment 2845888

Nahamia kwa Wapambe Uchwara na Wanafiki.

NB : Haipaswi kwa mtu yeyote aliye na akili timamu kufuraia mauaji ya mtu yeyote asiye na hatia na kushangilia kama Jambo zuri limefanyika haswa waathirika zaidi wakiwa watoto ,wakina mama na wengine wasio jiweza.

Watu wengi ukiacha wale wapo neutral nasema wake ambao wana mahaba na wanashangilia Israel katika kipindi kirefu wakati Raia wasio tena kuonyesha kurahia hadharani kuwa wote ni magaidi , mifano halisi ni hiyo
chini.

View attachment 2845893

Wa pili huyu.

View attachment 2845895

Sasa nauliza Raia kibao wa Palestine wao hawana wazazi ,ndugu au sio binadamu kiasi ambacho mtu kuona mauaji Yao ni kitu cha mchezo na kuwehuka kama hao juu ? mtu huyo huyo Maghayo na genge lake jana wakitoa lawama kubwa na kusikitika ,na kutukana hovyo kwa hasira kutokana na video ya kifo cha kikatili cha mtanzania mwenzetu inayosambaa ambayo binafsi ilinisikitisha sana na kuharibu mood yangu ya siku nzima.

Jambo lingine ambalo limejishangaza watu walijustify Raia kuuwawa kwa kisingizio cha kutafuta magaidi wakati huohuo wanajeshi wa Israel walipoua kimakosa Raia watatu katika kutafuta Hamas maandamano makubwa yamefanyika nchini mwao pamoja na kuoewa lawama ,sasa kwa nini isiwe fair wao kuuwa wenzao wa tatu Tu katika kufuta magaidi lakini wakiuliwa maelfu wa Wapalestina wasio na hatia iwe poa ?

HITIMISHO

Ujumbe kwa wote acheni kufanya vita ushabiki kiasi ambacho kufurai umwagaji damu wa Raia yeyote yule na uharibifu mwingine kuweni waadifu pamoja na utu.

#I Hate Hypocrisy and Injustice
Naunga mkono hoja
 
1. Mkuu nikiri kutolisoma lote andiko lako. Ni refu mno. Jifunze kufupisha au kuligawa nyuzi vipande.

2. Unakiri wapalestina na hivyo HAMAS wana haki ya kujipigania ila taabu yako ni matumizi ya nguvu.

3. Mkuu nguvu ni hatua ya mwisho baada ya mengine yote kushindwa tokea 1948.

4. Kwa maoni yako Maji Maji, Mau Mau, ANC, FRELIMO, MPLA, KANU, TANU nk ulikuwa upuuzi.

5. Kwa hapo #4 sote tungekuwa tungali makoloni.

6. Dhahama hili lawama ni kwa wajomba na babu zake Mungu Natenyahu na Joe Biden!

Ya nini kulalama?
Umeona matokeo yake sasa jinsi uharibifu uliotokea na vifo vya kikatili mpaka sasa na Hamas walitaka mapigano yasitishwe ...

Je yakisitishwa sasa Kati y Hamas na Israel Nani atakuwa amepata hasara ,uharibifu na vifo vingi ?

Je kuna faida zozote ambazo muhimu zitakuwa zimepatikana ?
 
Ninapowapinga ni njia ambazo wanatumia katika kujikomboa asilimia kubwa napingana nazo kwani zimeleeta maafa makubwa kwa Raia wao baada ya ukombozi ,kwani naamini matokeo ndio hujulisha faida ya Jambo na kama wanataka ukombozi wa kweli ingekuwa bora kwao kujipanga kwa nguvu zote kiimani ,kimbinu na mikakati silaha nk na sio kukurupuka tu na kushambulia ambapo matokeo yake kila siku yanaonekana maafa yanayopatikana ni makubwa zaidi kukiko faida.
Humu JF hakuna muislamu ambaye yupo kuweza kufikiri kama wewe.

Wote wanaotetea hivi vita wanaendeshwa na mahaba ya dini kwako imekua tofauti, kuanzia sasa upo kwenye top 5 yangu.

Hili swali niliwahi uliza kilichofata ni matusi na kejeli.

Unaenda vipi kumchokoza jirani yako ambaye anakuzidi nguvu, Halafu familia yako hujajua jinsi ya kuilinda na hawana taarifa?

Hon. adriz big sana kuliona hili.

Hapa JF
1 ni wewe
2. Sir john Robert

Wengi waliobaki ni hisia tu na mahaba ya dini.
 
Umeona matokeo yake sasa jinsi uharibifu uliotokea na vifo vya kikatili mpaka sasa na Hamas walitaka mapigano yasitishwe ...

Je yakisitishwa sasa Kati y Hamas na Israel Nani atakuwa amepata hasara ,uharibifu na vifo vingi ?

Je kuna faida zozote ambazo muhimu zitakuwa zimepatikana ?

Unajua mapigano yakisitishwa ni katika maelewano gani?
 
Humu JF hakuna muislamu ambaye yupo kuweza kufikiri kama wewe.

Wote wanaotetea hivi vita wanaendeshwa na mahaba ya dini kwako imekua tofauti, kuanzia sasa upo kwenye top 5 yangu.

Hili swali niliwahi uliza kilichofata ni matusi na kejeli.

Unaenda vipi kumchokoza jirani yako ambaye anakuzidi nguvu, Halafu familia yako hujajua jinsi ya kuilinda na hawana taarifa?

Hon. adriz big sana kuliona hili.

Hapa JF
1 ni wewe
2. Sir john Robert

Wengi waliobaki ni hisia tu na mahaba ya dini.

Ujinga nambari 1 ni kudhani kuna vita vya kidini Gaza jambo ambalo hata HAMAS, Israel, wala dunia havijasema; ila wale wajinga ndembe ndembe wa JF!
 
Ujinga nambari 1 ni kudhani kuna vita vya kidini Gaza jambo ambalo hata HAMAS, Israel, wala dunia havijasema; ila wale wajinga ndembe ndembe wa JF!
Haswa!

Na ndicho nilichoandika, wengi hapa JF mkuu brazaj hivi vita wamevipa sura ya udini.

Bora adriz, wewe kidogo mnahoji logical.

Yupo ndugu yangu anaitwa malaria ana udini mpaka nashangaa.

Kama unabisha hili tazama wengi wachangiaji vita hii wamevipa udini.

MK254 yeye anatetea israel haoni baya wanalofanya.

Ritz yeye ni hamas.

Yote yote adriz ni mtu wakwanza kuwa unbiased kwenye hii ishu nampa 100%
 
Hakuna popote katika wahusika wakuu wa vita walipo onyesha kuwa ni mpambano wa kidini.

Haipo shaka kuwa ni mpambano wa kugombea ardhi wa muda mrefu baina ya Israeli na Palestina.

Anayeupeleka mgogoro huu kidini au kigaidi wote wanafanana. Hapo kuna wasiojitambua na wenye agenda zao binafsi. Tofauti zao ni majina tu.
 
Bora umekua mkweli.

Hon. Brazaj
 
Sidhani hata ni kuwa mkweli as a person, bali huo ndiyo ulio ukweli.

Penye ukweli, uongo hujitenga.
Wanaogombana hapa jf kuhusu hivi vita wanavipa sura ya udini ndio ilikuwa pointi yangu.

Umeelewa lakini mkuu?
 
Wanaogombana hapa jf kuhusu hivi vita wanavipa sura ya udini ndio ilikuwa pointi yangu.

Umeelewa lakini mkuu?

1. Kugombana humu vita viko Gaza pia si shahihi sana.

2. Kuweka ushabiki kwenye vita ni jambo la kusitikisha.

3. Kushindwa kutambua sababu za vita ni jambo la kuhurumiwa.

4. Hapo #3 ni case ya ujinga kama mwingine wowote.

Otherwise nakuelewa sana tu ndugu.
 
Unajua mapigano yakisitishwa ni katika maelewano gani?
Sifahamu ila sio mwaka huu kutokea Hamas kufanya mashmbulizi kisha mapigano kusitishwa bila faida yeyote ya maana kwa Wapalestina.

Wakati Hali sasa ni kama hivi
IMG_20231230_171406.jpg
 
Haswa!

Na ndicho nilichoandika, wengi hapa JF mkuu brazaj hivi vita wamevipa sura ya udini.

Bora adriz, wewe kidogo mnahoji logical.

Yupo ndugu yangu anaitwa malaria ana udini mpaka nashangaa.

Kama unabisha hili tazama wengi wachangiaji vita hii wamevipa udini.

MK254 yeye anatetea israel haoni baya wanalofanya.

Ritz yeye ni hamas.

Yote yote adriz ni mtu wakwanza kuwa unbiased kwenye hii ishu nampa 100%
Jamaa uliowataja hapo ni kweli ,mfano ndugu Malaria mara alete Uzi wa kushangilia mapambano watu wakichapana na kuuwana kishabiki kisha baadae kuanza kuleta Uzi wa kuilaumu unyama na mauaji yanayofanyika hiyo sio sawa ,ilitakiwa tokea mwanzo mpaka mwisho ushabiki uwekwe pembeni ..

Jamaa Mkenya anafahamika vyema kashindikana kwenye sekta ya ushabiki maandazi.
 
Sifahamu ila sio mwaka huu kutokea Hamas kufanya mashmbulizi kisha mapigano kusitishwa bila faida yeyote ya maana kwa Wapalestina.

Wakati Hali sasa ni kama hivi View attachment 2857745

Kwa vile hujui busara kusubiri mwisho. Waungwana wanasema:

"He who laughs last, laughs best."
 
Back
Top Bottom