BLACK MOVEMENT
JF-Expert Member
- Mar 11, 2020
- 4,548
- 11,901
Katika Maisha yangu huwa kuna wakati nawalamu mno wazazi wangu , Walimu wangu na Serikali pia kwa Mfumo wa hovyo sana,
Katika Maisha yangu nilikuwa na Kipaji kikubwa sana cha kucheza Mpira, Wakati huo TV hazikuwepo tulikuwa tunawekewa mikanda ya mpira hasa World Cup na kwa sisi tulikuwa tunapata mikanda ya Timu za Uingereza pia.
Kwa sababu nilikaa Kotazi nilianzisha hadi timu ya Kotaz na tulikuwa tunashindana na timu za mitaa mingine na na kwa sababu ya kipaji changu hasa kwenye kufakamia nyavu na aina ya uchezaji timu ya mtaa wetu ilikuwa tishio sana kwa timu zingine.
Kuna wakati hata kanisani nilikuwa naenda na Mpira tukifika wakati ibada inaendelea natoroka na wenzangu tunatoka nje ya kanisa tunaanza kucheza mpira, na some time Mama alikuwa akijua hilo nilikuwa nakula kibano sana baadae.
Wakati wote huo Mama alisisitiza kwenye kusoma tu na si vinginevyo kwa kweli Darasani nilikuwa vizuri pia kwenye top 5 lazima unikute.
Kitu kinacho nifanya nimlaumu sana mzazi wangu na pia walimu wangu ni kwamba Kotazi tulizo kuwa tunakaa bahati nzuri zilikuwa na wazungu kwa sababu ni kotaz za Mission hivyo wazungu walikuwepo ingawa wao walikuwa na Block zao tofauti na za kwetu, na ndio walio kuwa wanatufadhili mpira na wakati mwingine Jesi
Kuna Mzungu mmoja nakumbuka alikuwa akiitwa James, huyu alikuwa ni Mwingereza alikuwa anapenda tumu yetu na kuna wakati alikuwa anatoa Gari yake Toyota Hilux tunabebwa tunaenda kucheza mpira.
James kuna siku tulikuwa na mechi na tumu ya Kotazi za Magereza alikuja na Camera Video yake akaturecord mkanda na baada ya hapo alienda nao kwao ili akatengeneze then akirudi aje kutuonyesha, Zamani Camera Video ilikuwa wanatumia kama kanda ya Kaseti kurecord, Akiwa kwao Uingereza baada ya kutengeneza mkanda aliwaonyesha Marafiki wenzake ambao walikuwa mashabiki wa Timu ya Sunderland A.F.C. na nilikuja kujua pia hii kupitia jezi alizo kuwa ana tupatia make zilikuwa na chata ya Sunderland A.F.C.,wale Mashabiki walipenda sana uchezaji wangu kiasi kwamba wali peleka ile Video kwenye offisi za Club na pale pia wakapenda sana, sasa katika wale mashabiki kuna mmoja alijitolea kugharania mimi niende kujifunza zaidi kule.
James alivyo rudi pamoja na kutuonyesha ule mkanda pia bakumbuka alibileta zawadi ya njumu za ngozi panoja na jezi alipewa na wale mashabiki aniletee, James baadae akaniita kwake akanieleza mkasa mzima wa kule na kwamba wanataka niende kule, mimi binafisi nilifurahi mno ingawa nilijua nitakumbana na kikwazo cha mzazi, nilifurahi kwa sababu pia nisha anza kujua Uingereza kupitia mikanda ya Jamesa alikuwa akituonyesha mikanda mingi sana ya timu za Uingereza, Baada ya pale nakumbuka Mama alikuwa amesafiri baada ya kurudi nikamueleza aisee mama alikuja juu sana kwamba nisome, James akajaribu kumueleza Mama akakataa kata kata, Mama angu alikuwa ni Concervative sana, Msabato Masalia, Kibaya zaidi kulikuwa na walimu Marafiki zake nao wakasapoti kwamba nisome, James akawa hana namna na baada ya pale nikaja kwenda Secondary nikacheza cheza baada ya pale Chuo na ikawa ndo mwisho wa kipaji changu.
Wazazi mnao nisikiliza ni kwamba heshimu sana vipaji vya watoto wenu, hebu fikiria Diamond kama angekomaliwa asome sana huenda angekuwa Mwalimu anakula vumbi ya Chaki, lakini ona leo hii alipo.
Heshimu saba kipaji cha mtoto wako na msaidie kukiendelea, kwanza kwa sasa ajira ni ngumu na sayansi ilisha ua kazi nyingi.

Upvote
3