Nawaomba radhi Watanzania kwa kumpendekeza hayati Magufuli kwa hayati Mkapa

Mkuu Bora umekua mkweli kwa Sababu Kila kitu Cha Nchi yetu unakijua ukizingatia wewe ni WA mfumo .Ni kweli Magufuli amehatibu Sana nchi na haya matozo kuongezeka ni kutokana na sera zake mbovu za kuua uchumi ndiyo maana Hali ni ngumu na itatuchukua miaka mingi kuweka uchumi wetu vizuri.Pia kwa upande mwingine utawala wa Magufuli umekua kama Mwalimu kuja kutufundisha kama nchi tunatakiwa tuwe na mifumo imara ya kiendesha nchi .Katiba ipatikane ili nchi iende mbele.

Kwangu mimi utawala wa Magufuli ni kama umeua Kila kitu na inabidi tuanze upya na hii kwa Mujibu wa unabii wa kiutawala Tanzania nchi ipo Gizani na badae kidogo mwanga utakuja.
Asante kwa kuomba radhi.
 
Msimamo wangu ni ule ule , Hata mfanyeje JPM was the Hero of Africa . Jipendekezeni tu lkn alikuwa kipenzi kweli kweli wa Watanzania . Ukifanya Tafiti mitandaoni profile picture za Watanzania , JPM bado anadunda kwenye mioyo ya Watanzani . Siyo huyu wa kuyumbishwa yumbishwa tu na kundi la watu wachache .

Marais ambao hawatasahaulika Tanzania basi Nyerere na Magufuli . Sijawahi kusikia Wananchi wa Taifa fulani wanatamani kuongozwa na Rais wa Nchi nyingine ila kwa JPM imetokea .
 
Wwe lazima utakua mpiga deal! Haya Sasa wwe endelea kupiga deal Sasa na Mama wala hana noma na Wapiga deal mradi pesa tu ije kitaa!!
 
NI busara kuchutama unapogundua umekosea ila ingekua vyema uyaseme haya wakati akiwepo ili naye tusikie upande wake. Nakupongeza kwa dhati
Ungependelea kama na mimi nipatwe na lakupatwa kwa kuongea kipindi kile?
 
nyie kunguni msaidieni mama laah sivyo 2025 atakuwa na wakati mgumu sana jukwaani.

mwambieni hakuna njia salama kwake zaidi ya ile aliyopita jpm.
 
kwa upande mwingine utawala wa Magufuli umekua kama Mwalimu kuja kutufundisha kama nchi tunatakiwa tuwe na mifumo imara ya kiendesha nchi. Katiba ipatikane ili nchi iende mbele
Hili ninaamini litafanyiwa kazi. Kwangu hii ndio kazi pekee mhe Samia alitakiwa kuifanya maana yeye alikuwa mhanga mkubwa kipindi kile.
 
We sema tu ukweli alivyoingia madarakani ali athiri maslahi yako acha kuzungukazunguka.
 
Tambua pia kuwa umechangia ulemavu wa Lissu, kuumizwa vibaya kwa akina Mdude na kupotea kwa akina Saanane. Binafsi sina msamaha na wewe
 
Hayupo mwanadamu aliyemkamilifu. Mema ya JPM mwisho wa siku yatazidi mabaya yake ambayo yanaimbwa kila itwayo leo ilikufunika mazuri yote aliyoyafanya.
Achana nao hawa wa vyeti feki hawawezi kumpenda magu kamwe
 
Nilitarajia kuona namna ulivyomtambulisha Magufuli kwa mkapa nakumbana na uzi ulioandika kwa ajili ya mwaka 2015.

Hakuna logic yeyote katika uzi huu.
 
Nilitarajia kuona namna ulivyomtambulisha Magufuli kwa mkapa nakumbana na uzi ulioandika kwa ajili ya mwaka 2015.

Hakuna logic yeyote katika uzi huu.
Ni jambo jema kwamba uko huru kutoa maoni yako. Magufuli hakupenda maoni tofauti na yakwake.
 
Tambua pia kuwa umechangia ulemavu wa Lissu, kuumizwa vibaya kwa akina Mdude na kupotea kwa akina Saanane. Binafsi sina msamaha na wewe
Mkuu haya yanabakia kuwa makosa yake mwenyewe. Sidhani kama kuna mtu anayepaswa kubeba hukumu ya haya mambo isipokuwa yeye mwenyewe.
 
Gunzi la moto alilokutia magufuli mataconi bado linakuumiza sana, hivi hauonagi aibu kupambana na marehemu !? shame on ptuuuuuuu i spit on you.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…