Nawaomba radhi Watanzania kwa kumpendekeza hayati Magufuli kwa hayati Mkapa

Nawaomba radhi Watanzania kwa kumpendekeza hayati Magufuli kwa hayati Mkapa

Kwahio huyu aliyopo sasa ni All Right ???!!!!!!

Nadhani huu muda tungeutumia kuganga ya Sasa wala sio Yaliyopita ambayo si Ndwele basi tungeisaidia nchi yetu...

Au tunangoja huyu akishatoka ndio tuanze kumzodoa ?!!!
Unaangalia ulipojikwaa wakati unatafuta hatua sahihi. Sidhani kama mfumo utarudia tena lile kosa.
 
Asili ilichukua mkondo wake.. Ameshaondoka sasa maisha yaendelee hata tukiendelea kuishi kwa majuto haitatusaidia bali tuwe makini sasa na huko tuendako yasije kujirudia haya
Hakika, tuijenge kesho iliyo bora.
 
Hatuwezi kukusemehe kwa kutuletea yule kiongozi muovu. Tunamshukuru tu Mungu kwa kutuondolea yule kiongozi muovu bila damu kumwagika.
Kusamehe ndio kunapelekea kupona.
 
Ungeomba tukusamehe kabla sir God hajafanya yake....


Anyway.... "Ee Mungu, ikikupendeza mchukue huyu luteni kabla mwez hujaisha"

Wote tuseme Amen
Kama ni hukumu basi ilishamfikia mkosaji. Wengine tuombeane heri.
 
Kwa tabia za Magufuli wote tulibaki midomo wazi kasoro:
Bashiru
Polepole
Makonda
Sabaya
Mzee wa Gwambina
Kalemani
Joyce Malomo
Angela Kairumi
Doto James na
Heri James.

R.I.H Magufuul!

Umenisahau kumtaja na Shehullohi
 
JPM was a great man every day people are composing every kind of melodious tune to influence the public to dance but in vain; his impact is still intact and deeply felt by whoever was directly or indirectly exposed to his command therefore his legacy whether positive or negative shall prevail for a number of years ahead.
It is a great thing that now we welcome opinion from every individual in the bid to build our democracy and society. These things were far above the reach of the long gone guy.
 
Hilo la msamaha ni moja je twawezaje kuzuia yasijetokea tena?

Wale wahuni wake waliobaki mpaka waburuzwe kortini kama yule mmoja wa kule kaskazini.

Baada kuna wahuni wengi aliokuwa akiwatumia na bado wapo mtaani tu japo wamejitahidi kujificha ila wanajulikana haki itendeke tu , wengine hadi walisababisha nchi ikaingia kwenye red flag alert na wakazuiwa kuingia nchi za watu.
 
Mwaka 2013 nilikuwa namkubali sana Magufuli kwa namna alivyokuwa anasimama imara kufuata sheria kama waziri. Nilileta huu uzi kumfanyia lobbying kwenye chama Kwa timu hii ya rais na makamu wa rais, CCM tutashinda 2015.

Niliamini huyo ndio atakuwa msaada katika kuijenga Tanzania inayofuata sheria hivyo siku moja nilikutana na Mkapa nikawa namsifia sana huyo waziri. Najua Mkapa alikuwa anampenda Magufuli kama kijana wake lakini watu tulipokuwa tunamtaja mbele yake akapata hamasa sana kumpigania apitishwe.

Bahati mbaya Magufuli alipopata uraisi alibadilika sana na kuacha kufuata sheria na katiba. Hakutaka uhuru wa habari wala changamoto yoyote ya kimawazo. Aligeuka kuwa katili na msema hovyo. Aligeuka akawa muongo sana, aliendesha nchi kwa mikopo lakini anadanganya ni fedha za ndani. Aliua uwekezaji.

Wote tulibaki mdomo wazi kwa aliyoyafanya. Watanzania naomba mnisamehe.

Asante kwa kumpendekeza JPM kwa Mkapa...

Purpose yako ushaitimiza...unaeza ukapotea tu huna maana tena kwa taifa hili...
 
Back
Top Bottom