Nawaonea sana huruma vijana na wanaotaka kuanza biashara maana, sehemu nzuri za biashara zimeshaisha

Nawaonea sana huruma vijana na wanaotaka kuanza biashara maana, sehemu nzuri za biashara zimeshaisha

Optimists

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2021
Posts
467
Reaction score
1,358
Kwa miaka ya sasa hivi million 10 sioni kama ni mtaji tosha katika biashara, hasa hizi biashara za kukaa kusubiri wateja, kwasababu frame za biashara (mahali palipochangamka) ni kama zimeisha na ukipata basi Kodi itakua ni kubwa, au utahitajika kumuondoa mtu, ulipe wanaita kiremba, kwahiyo mtaji wa million 10 utatumia zaidi ya million 4/5 Kwa ajili ya frame, bado uitengeneze Frame pamoja na kuirekebisha kulingana na biashara Yako, utabaki na mtaji mdogo sana, no back up baada ya mwaka utashindwa kulipia Kodi na utakimbia, kwasababu mtaji mdogo na competition ni kubwa.

Kwa mtazamo wangu, ninaona Bora kijana au anayetaka kuanza biashara ajikite kwenye skills, uzalishaji, kilimo, ufugaji.

Ufugaji, kilimo n.k hakina competition ardhi ni kubwa zaidi, unauza mifugo muda wowote unaotaka,
Nimeona podcast Moja mama Mmoja alianza na mbuzi 60 sasa hivi anazo karibia 400, na hajawahi kutafuta mteja zaidi ya watu kwenda kununua kwake.

Hizi biashara au uchumi wa frame , ni scams na chanzo kikubwa cha umaskini.
 
Hili lina ukweli sana. Siyo sehemu nzuri tu, biashara nyingi zimekuwa saturated. Vijana waangalie tu kuwekeza kwenye uzalishaji.

Hesabu(za kwenye karatasi). Ukiwa na ekari moja kwenye hali nzuri ya hewa. Ukapanda nyasi za mifugo(elephant grass). Unaweza kulisha mbuzi 50 hadi 100. Kwa 10m unaweza ukafanya hili na kuwa na kipato cha kuendesha life.
 
Kwa miaka ya sasaivi million 10 sioni kama ni mtaji tosha katika biashara, hasa hizi biashara za kukaa kusubiri wateja, kwasababu frame za biashara (mahali palipochangamka) ni kama zimeisha na ukipata basi Kodi itakua ni kubwa, au utahitajika kumuondoa mtu, ulipe wanaita kiremba, kwahiyo mtaji wa million 10 utatumia zaidi ya million 4/5 Kwa ajili ya frame, bado uitengeneze Frame pamoja na kuirekebisha kulingana na biashara Yako, utabaki na mtaji mdogo sana, no back up baada ya mwaka utashindwa kulipia Kodi na utakimbia, kwasababu mtaji mdogo na competition ni kubwa.

Kwa mtazamo wangu, ninaona Bora kijana au anayetaka kuanza biashara ajikite kwenye skills, uzalishaji, kilimo, ufugaji.
Ufugaji, kilimo n.k hakina competition ardhi ni kubwa zaidi, unauza mifugo muda wowote unaotaka,
Nimeona podcast Moja mama Mmoja alianza na mbuzi 60 sasaivi anazo karibia 400, na hajawahi kutafuta mteja zaidi ya watu kwenda kununua kwake.

Hizi biashara au uchumi wa frame , ni scams na chanzo kikubwa cha umaskini.
Biashara haipo hivyo ndugu, kama Una Quality za ujasiriamali wala huhangaiki, mjasiriamali anaweza popote kufanya biashara na kuona opportunities ambazo wengine hawajaziona.

Kuna watu kibao wapo so called sehemu hot za biashara na wanashindwa kutoboa na wengine wapo ndani ndani huko na bado watu wanawafuata.
 
Back
Top Bottom