Nawaonea wivu walionunua hisa za DSE

Kuna namna wanakuwa wanafanya ku manipulate soko. Kwa nje ya nchi wanakuwa wanaifanya pale ambapo wana quote price. Inakuwa ni kama tricky fulani to fish suckers. Mfano unaweza ona bei inashuka kwa kasi halafu ukauza and very soon baada ya kipindi fulani unashangaa bei inaanza kupanda. Kumbe that was fake move. Au pia unaweza ona bei inapanda kwa kasi halafu ukanunua then baada ya mda bei inaanza kuporomoka, hapo unakuwa umeshakuwa screwed.

Ila wataalam wa masoko wanajua namna ya kutambua hizo tricky, kuna kitabu kimoja kama upo interested kimeandikwa zamani sana kama miaka 70 iliyopita na bwana mmoja anaitwa Robert Wycoff anaeleza mbinu ya kugundua manipulation ikiwa ni pamoja na kuangalia volume ya stock inavo flow.

Kuna kitu ameeleza kwamba price ina move kwa kiasi fulani kutegemeana na certain volume. Sasa kuna circumstance nyingi ambapo unakuta price inapandaa lakini volume of trading ni ndogo, hapo ujue kuna manipulation ambao wana test response ya public ipoje. So ukiwa tricked ku buy unajikuta ume buy stock kwa bei kubwa halafu baada ya muda bei ishashuka. Ameeleza issue nyingi sana google vitabu vya richard wycoff though ni setup ya zamani na kinatia uvivu kusoma but tafuta hicho kipande cha volume usome.

Hata kwa DSE manipulation inawezekana, sema labda operation yake inaweza kuwa complicated maana manipulation inahitaji public ambayo wanaassume ni ignorant. Na ignorant people ndo wanaokuwa tricked easily na ku fall kwenye hiyo bait ya manipulation. And since soko letu bado halijawa na public wa kutosha ndo mana somehow inakuwa ngumu but i believe inafanyika.

Halafu the issue is not regulation, operation za soko zitakuwa kama kawaida bidding and offering, na manipulation inafanyika hapo hapo kwenye bidding na offering ambayo kunakuwa hamna ukiukaji wa sheria. Its just smart minds operations.

Ila pia kuikwepa hii manipulation lazima uwe vizuri sana ku value stock, yaani decision zako zisiwe driven na emotion za unachoona kwenye price. Iwe driven na real value ya stock.
 
Yeah. You need to be determined. Within 6 moons you'll find yourself being able to predict the market.
Endelea kukusanya mtaji mkuu, arround 1000$ kwa kuanzia. Hutakosa 100-200$ kwa siku kama hela ya mboga.
Naipitia pitia hapa... its an opportunity kwa kweli.. sema very risk
 
Yeah. You need to be determined. Within 6 moons you'll find yourself being able to predict the market.
Endelea kukusanya mtaji mkuu, arround 1000$ kwa kuanzia. Hutakosa 100-200$ kwa siku kama hela ya mboga.
Mimi nilikuwa nafatilia sana soko la hisa, huko kwenye forex nilikuwa situpi macho kumbe kuna fursa
 
Mi nimejaribu kuvi download baadhi ya hivo, uzuri wangu mimi nimeshazoea kusoma kwenye PC kwa hiyo nina uhakika ntavinusa hivyo vyote angalau kwa baadhi ya topics maana offcoz sio rahisi usome kitabu cha page 800 huo sio usomaji wa zama hizi. Nta choose topics halafu ntapitia. Kama hicho cha mishkin nilishakipitia pitia.
 
Mi nina wasiwasi sana na DSE, nahisi kuna watu wana uwezo wa kucheza na zile bei. Unaweza kuona price inaongezeka kwa kasi ya ajabu, wajanja wakauza hisa zao na baada ya hapo zinashuka tena kwa kasi ya ajabu, wale wajanja wananunua tena.
Kwa ufupi soko halina stability, kwa sababu haiwezekani bei ya hisa inaongezeka bila ata ya utendaji wa kampuni husika kuongezeka. Yaan ongezeko la bei haliendani na performance ya kampuni kabisa.
Sidhani kama kuna mtu mwenye longterm plans anafaidika, Wanaofaidika ni wenye shorterm plans tu.
Ata hawa walionunua hizo za DSE (Wakumbuke Swala ilikuaje) nahisi ni public imepanic tU, lakini hizo hisa hazina thamani hiyo. Wajanja wanaouza sasa wataula, ila wanaonunua sijui [emoji4][emoji4][emoji4].
Binafsi nimekula sana hasala katika hizo biashara, kila nikijitahidi na mimi niingie katika kundi la hao wajanja nafeli.
Naona bora visenti-senti vyangu nikaweke SACCOS tU.
 
Embu tuambie ulikulaje hasara, utakuwa umesaidia na wengine ili tuone kama kosa lilikuwa lako ama la upande mwingine. Kusema tu umekula hasara bila maelezo akati mi najua watu wanakula faida its an ambiguity.
 
Anzisha hy shule tujifinze tuinvest
 

Pole ubaya watu wengi wanafanya maamuzi ya fedha kwa mihemko na siku zote watu ambao hawafanyi utafiti wa kutosha ndio wanaliwa vibaya na ndio wanachangia liquidity sasa kwa kiswahili kuna msemo kiaendacho juu kingoje chini sasa au mpira ukiujaza sana mwisho hupasuka . Kuna watu wa aina mbili kubwa kwenye hii mambo kuna investor na speculator sasa kwanza kabla hujaingia unatakiwa kujiuliza wewe ni nani na mpango wako ni upi na hasara au faida kiasi gani unaitafuta. Steam ya hii kitu sasa imerudi kawaida. Ukifuatilia mambo ya hii kitu ni kawaida kama kitu kimepokelewa vizuri kupanga mara mbili hata tatu kumbuka Alibaba, Facebook, Microsoft kama nakumbuka in 1990 kwenye lile boom la technologia haya mambo yako ila cha muhimu ni kujua unataka nini na sera ( stratergy yako ni ipi) halafu unatafuta watu mwenye mtazamo wako. Nakupa mfano Mzee Warren Buffet ni mheshiwa wa value stock au buy and hold lakini vilevile anacheze forex mwaka juzi alipiga faida 12.billion mheshimiwa Soros mzee wa forex toka kabla ya Brexit atakuwa alikuwa anachukua position 1992 allitengeneza 1.0 billion dollar kwa siku mgoogle. Lakini wanachanganya kuna wakati kunatokea fursa unaingalia ukiwa na jicho sahii unatoka nayo. Ila lazima ujue point yako ya kuinama ni mpaka wapi
 
Embu tuambie ulikulaje hasara, utakuwa umesaidia na wengine ili tuone kama kosa lilikuwa lako ama la upande mwingine. Kusema tu umekula hasara bila maelezo akati mi najua watu wanakula faida its an ambiguity.
Wakati niko chuo nilikuwa natumia excess niliyokuwa nayo kununua hisa, kwa lengo la kuja kuuza nikimaliza chuo, ili nipate visent vya kunilinda mtaani na ata kutafutia further professional qualifications.
Nilikuwa nanunua CRDB kwa sana coz niliamini ni kampuni ambayo inakua so sikutegemea hisa zake kuja kushuka. Na ndio maana nasema mtu wa long term plans kuna uwezekano mkubwa sana asifaidike.
Na kuna nyingi tu nilinunua kipandi kile bei 320. Na bei yake ilipanda hadi 525 (kwa kumbu kumbu zangu) baada ya hapo nadhani unaona sasa hv bei yake ni Tshs ngapi.
Nikaja kujaribu ku-diversify na kununua za TPCC na nyinginezo yakawa yaleyale tu.
Mbaya zaidi unaweza kuweka selling order ikakaa zaidi ya mwezi unaambiwa wanunuzi hamna na bei inazidi kuporomoka. Hapa ndipo nilipokata tamaa kabisa na kuona soko halina stability.
 

Kwa Tanzania regulator ni CMSA kwahiyo usiogope na hili swala la kupanda bei inatokana na wale watu waliozidi kutokana na hii kitu ilikuwa so much oversubsribe sasa lazima wafike target zao utakuta imeshaamuliwa na bodi lazima tuwe na stake kwenye kampuni fulani ya kiasi fulani ndio tuache kununua kwahiyo bei sio issue na kama ni invest wa nje bei hiyo bado hiyo inawekwa kwenye penny stock a stock with value less that $5 sasa hii iko kwenye cent 50 watu wananunua tu mpaka hapo matakwa yao yatakapotimia na jua kuwa tunaelekea kudiscourge ununuzi wa t.bill na bond sasa unafikiri ile hela itaenda wapi. Na ulaya interest rate 0 to negative capital has to flow somewere kwenye higher returns. Ila kwa habari ya ipo hili ni jambo la kawaida sana angalia hapa CRDB ilitokaga 400 to 850 ila sasa iangalie sokoni. Wanasemaje wale press the Ironn...........
 
huwezi amini nilipigiwa simu na jamaa yangu akaniambia kama nina pesa ninunue hisa DSE ,,,Da sikutilia maanani kwa kweli opppsss.....kweli Knowledge is power,,,,,,,damn
 
Hapo kwenye bold naona ina apply zaidi kwenye nchi za wenzetu kama states maana stocks nyingi kubwa kubwa ziko na price ya 2 digits na Kwamba stocks priced below $5 ndo cheap. Ila kwa tanzania i dont know if that benchmark can apply.
 
Yaan hiyo biashara ni "One man's gain, anther man's loss"
Buffet huyohuyo ndie anaesisitiza kuwa usitarajie kufanikiwa in the short run katika share investment. Ma-speculators wazee wa short term plans ndio wanaofaidika, sasa kwa mazingira hayo huwezi sema soko lina stability.
 
So you are saying, investment is a ZERO SUM GAME?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…