Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,677
- Thread starter
- #141
Kuna namna wanakuwa wanafanya ku manipulate soko. Kwa nje ya nchi wanakuwa wanaifanya pale ambapo wana quote price. Inakuwa ni kama tricky fulani to fish suckers. Mfano unaweza ona bei inashuka kwa kasi halafu ukauza and very soon baada ya kipindi fulani unashangaa bei inaanza kupanda. Kumbe that was fake move. Au pia unaweza ona bei inapanda kwa kasi halafu ukanunua then baada ya mda bei inaanza kuporomoka, hapo unakuwa umeshakuwa screwed.Hivii labda nahitaji ufafanuzi zaidi kwenye hili la ku manipulate stock price au kupandisha bei makusudi au kuishusha.
Nachojua DSE kama soko pia alikuwa regulator au msimamizi wa kampuni zote zitazojisajili sokoni hii nj pamoja na kuangalia kampuni isifanye ujanja ujanja kwa manufaa yake.
Sasa kwa DSE kuingia sokoni yenyewe inasimamiwa na nani? Nani ni regulator wa DSE? Je ni CMSA? Kama ni CMSA hawalioni hili la bei kupanda twice ghafla na wakawachukulia hatua? Hapa meters wa umma ni yupi? Au ndo DONS WILL REMAIN BE DONS NO MATTER WHAT. .......
Ila wataalam wa masoko wanajua namna ya kutambua hizo tricky, kuna kitabu kimoja kama upo interested kimeandikwa zamani sana kama miaka 70 iliyopita na bwana mmoja anaitwa Robert Wycoff anaeleza mbinu ya kugundua manipulation ikiwa ni pamoja na kuangalia volume ya stock inavo flow.
Kuna kitu ameeleza kwamba price ina move kwa kiasi fulani kutegemeana na certain volume. Sasa kuna circumstance nyingi ambapo unakuta price inapandaa lakini volume of trading ni ndogo, hapo ujue kuna manipulation ambao wana test response ya public ipoje. So ukiwa tricked ku buy unajikuta ume buy stock kwa bei kubwa halafu baada ya muda bei ishashuka. Ameeleza issue nyingi sana google vitabu vya richard wycoff though ni setup ya zamani na kinatia uvivu kusoma but tafuta hicho kipande cha volume usome.
Hata kwa DSE manipulation inawezekana, sema labda operation yake inaweza kuwa complicated maana manipulation inahitaji public ambayo wanaassume ni ignorant. Na ignorant people ndo wanaokuwa tricked easily na ku fall kwenye hiyo bait ya manipulation. And since soko letu bado halijawa na public wa kutosha ndo mana somehow inakuwa ngumu but i believe inafanyika.
Halafu the issue is not regulation, operation za soko zitakuwa kama kawaida bidding and offering, na manipulation inafanyika hapo hapo kwenye bidding na offering ambayo kunakuwa hamna ukiukaji wa sheria. Its just smart minds operations.
Ila pia kuikwepa hii manipulation lazima uwe vizuri sana ku value stock, yaani decision zako zisiwe driven na emotion za unachoona kwenye price. Iwe driven na real value ya stock.