Nawaonya vijana wa leo mnaofungua makanisa kila kukicha acheni mara moja kama hamna wito, Injili sio biashara.

Kuzimu imeingia makanisani kwa sasa kupitia haya makanisa yaliyotokea Marekani mengi yalianzishwa ili kuharibu Ukristo.
Aliyeanzisha music wa Rap na haya makanisa ya kufokafoka ni mtu mmoja ndio uzao wa uharibifu makanisani.
 
Ukikataa kuyajua maandiko bure utayajua kwa kuyalipia toka kwa hawa wajasiliadini
 
Unawaonea bure .

Shida ni waumin wa dini ya kikristo
Mbona vijana wa kiislam hawafungui misikit wala kujiita masheikh?

Niny wenyew mmeifanya kazi ya Mungu NI kazi Kama kazi nyingine na si huduma.
Tutaendelea kusali wabadilike
 
Pana motivation speakers na pana mens of God ipo haja ya mamlaka kuwakategorize.
Mfano kiboko ya wachawi yeye kabase kuuwa wachawi so ni wewe tu unachagua unataka injili kavu za kina mbarikiwa, Cassian,mwangila au unataka zile za kupokea makontena
Wengi wao ni motivational speaker wamejivisha utumishi kwa kivuli cha kanisa wapige hela
 
Umeandika vizuri lakini nikuambie ukweli: HAO MANABII, MITUME, WALIMU n.k wa aina hiyo na mambo yao hayo SIYO UKRISTO. NI USHETANI ULIOPAKWA JINA LA YESU. NI MAKUFURU. Wote wanaofuata upumbavu huo jwa hao wahubiri wanakufuru. Watakiona cha moto. Ukristo halisi umejengwa kwenye misingi iliyoachwa na mitume na si huu upumbavu unaoendelea leo. NI USHETANI MTUPU NA WOTE WANAOKIMBILIA MIUJIZA HUKO WOTE NI WAFUASI WA SHETANI WANAOLITAJA BURE JINA LA YESU KRISTO.
 
Unahakikishaje na kuthibitishaje mahubiri yao sio ya kweli ila ya wachungaji wengine ni ya kweli?

Wakikwambia kwamba Bwana wao Yesu haangalii mavazi bali mioyo yao, utajibu ni nini?

Utahakikishaje na kuthibitishaje huyo Yesu anajali na kuangalia mavazi ya wahubiri wake?
 
Na kuna wengine wanauza mchanga,maji na mafuta ya nyonyo,keki na kujidai vina baraka kila kitu kinaanzia buku, jamaa kila akifanya mahubiri huwa na lori la bidhaa zake anadanganya waumini wanunue ndio watapata upako, waumini wake ni hohe hahe yeye anazidi kuporomosha mahoteli, majumba ya kuishi, kumiliki mashamba na vitega uchumi kibao-wajinga ndio waliwao. Mimi nasali haya makanisa makuu lakini sitaki kuzoeana na wachungaji, wachungaji hupenda kufanya urafiki na mtu anayeweza kuamua kuwa kesho nataka nile biriani au pilau,wengi wao ni omba omba kwa waumini,hawa ni tofauti na hawa wenye SACCOS zao (makanisa yao) hao wote ni matapeli, nimemuona kijana mmoja eti ae ni pastor anasifiwa na Mwijaku pembeni amepaki Hummer, kavaa visiruali vya kubana Domo kasingiziwa.
 
Dhana nzima ya Mungu ilijengwa kwenye Uongo

Acha vijana watumie na wanufaike na dhana hiyohiyo iliyotumiwa na makanisa makubwa kuchota hela za watu kama Roman Catholic, KKKT, Anglican n.k

Hata kwenye hayo makanisa makubwa ni Hela za waumini tu ndizo huitajika and nothing else.

Kama huyo Mungu/ Yesu yupo kila mahali unaenda huko kanisani kufanya nini?

Huoni kwamba unaenda kutapeliwa tu hela zako utoe michango na sadaka kwa kigezo eti una mtolea Mungu?
 
Dhana ya dini kwangu haipo sana kwangu ni kama kusocialise tu, natoa sadaka ili nikiwa futi sita chini waje kuimba mapambio kuwafariji ndugu zangu na wanafamilia wangu wakati wakilia si kwa uchungu bali kwa jinsi watakavyoendesha maisha yao baada ya Bill Gates kuwa hawatamuona tena.
 
Nashukuru kwa swali zuri,

Nitakujibu kwa ushahidi wa kibiblia.

Kuhusu mahubiri yasiyo ya kweli:
Katika 2 Timotheo 3:16 inasema "Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuonya watu makosa yao, na kwa kuadabisha katika haki"
Hivyo mahubiri yeyote ambayo hayana mlengo wa utukufu wa Mungu hayo hayafai, mfano kuna mtu anajiita Nabii aliwahi kusema siwezi kuacha kuangalia chupi ya muumini wangu kisa nahubiri mtu kama huyu hawezi kuwa na mahubiri ya kweli.

Kuhusu mavazi:
Katika 1 Timotheo 2:9 inasema "Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujistri, pamoja na adabu nzuri na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, Wala kwa dhahabu na lulu, Wala kwa nguo za thamani"
Hivyo hata kama Yesu anaangalia moyo lakini sababu usijistri na kuvaa kwa adabu kama maandiko yanavyosema.
 
Natamani Ile kweli ya Kristo ndio ihubiriwe no matter what
 
For what I know you need to give us proof to support what you said.
 
Biblia si ushahidi bali hadithi zisizo na uthibitisho wowote ule.

Ni sawa na Hekaya za Abunuwasi uziite ushahidi bila kuthibitisha uwepo wa Abunuwasi mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…