NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
- Kila siku hujisomea somo la wiki, ikifika jumamosi wanakusanyika kwa masaa takribani mawili kwenye vikundi vidogo kufundishana waliyojifunza na baada ya hapo ndio huingia wote kanisani kwenye ibada, hii ni nzuri kuzidi kukaa wiki nzima hujajifunza chochote kwenye biblia unasubiri tu ifike jumapili kwenda kwenye ibada kumsikiliza mchungaji.
- Ni nadra sana kusikia kuna vurugu kanisani mfano kwa viongozi wanaong'ang'ania vyeo mpaka kufikia kanisa kugawanyika, kwa kanisa kama kkkt walutheri zilitokea vurugu miezi michache iliyopita kanisa lilikuwa linafungwa na mapolisi wanaenda kutuliza ghasia, hali hii ilipelekea mpaka kuwe na kanisa jipya lingine.
- Hakuna shinikizo la kutoa sadaka, naona kuna makanisa yana mpaka vitabu vya madeni ya michango, usipochangia waweza usizikwe na kanisa.
- Mavazi ya kujisitiri kanisani wanajitahidi, nashangaa baadhi ya makanisa mwanamke anaenda na vazi la ajabu ajabu anajitetea kwamba Mungu anaangalia roho.
- wachungaji wao hawavumi kwenye skendo za kuchezea wake za waumini ama kulawiti watoto.
- Kwenye kwaya wanaimba kwa kutulia, nyimbo kama kwetu pazuri na mkono wa bwana hakuna purukushani za kucheza bolingo ama kutetema kama Mayele.
- Wanaomba kistarabu bila fujo, hawakemei kwa sauti utadhani Mungu ni kiziwi.
- Hakuna biashara ya mafuta ya upako wala maji ya baraka,