Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Nashauri wapigwe ban na nyuzi zao za kinaa zifutwe, ili kulinda heshima ya jf.
 
Ukiwa Kiongozi wa wizara ya Michezo,
Je unafikiri nchi yetu itakuwa na uwakilishi wa kiushindani katika michezo hii ijayo ya Olimpiki?
2.Nini matarajio yako katika mashindano hayo?
 
Pale kwa mkapa kwa macho ya nyama tu kama nimuendaji wa uwanjani huhitaji maelezo mengi ile budget walisema watakarabati pitch, miundombinu, na viti pia lakini niaibu kwa kweli pitch some how now mvua ikinyesha maji hayatuami tena nankingine kilichoongezeka ni zile LED screen zamatangazo ila hata screen ya ku display matokeao ilishindikana labda kama wamefanya baada ya ligi lakini kimsingi CAG anahusika pale kwa special Audit
 
Mnapaswa kuandaa vijana na kuwa na academy nyingi,nyie mnashabikia masimba na mayanga,hayatusaidii timu ya taifa
 
Big up mkuu
 
Gerson, huo utangulizi wa Salam yako unatukwaza wengine..kwa jina la jamhuri ya muungano ndio nini?? Wewe ni mkristo kweli..huwezi kubadilisha Salam ya kiimani ukaipeleka hivyo..hivi, nikisema nakusalimu kwa jina la gerson msigwa kwako unaona imekaa sawa? Usije sema hukujua..nimekukumbusha! aliyeianzisha anaweza kuwa hajui alichokuwa anatamka!
 
Naona viongozi wa serikali wanaongeza kasi ya kuja jf. Ndio mnataka kuifungia twitter? Hamtaki kukosa pa kusemea?
 
Mbona mnakuja kwa wingi humu mwishoni mwa utawala huu??

Humu tunapeana ukweli tu pindi kiongozi na ama yeyote inapotokea hajasimama kwenye ukweli, hii ndiyo maana halisi ya kujenga msingi bora wa nchi yetu

Embe huwa tunalitaja embe na siyo kuliremba remba, kuna wakati mmekaa kimya sana kuhusu jambo la Katiba Yetu, katiba inayowahusu nyinyi na kizazi cha watoto wetu na Taifa letu kwa ujumla

Hii ilimaanisha kwamba, hamtaki kuitazama Tanzania katika kipindi kirefu kijacho ikiwa imesimama katika msingi imara na katiba bora

Sasa mnakuja humu kwa uwingi wenu hasa nyinyi viongozi wetu kutaka kupokea maoni yetuuu...au vile mbele yenu kuna uchaguzi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…