Nawashangaa Mo na Bakhresa kuendelea kuishi Tanzania

Shooter Again

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
5,603
Reaction score
9,263
Hivi Kwa utajiri wa Hawa jamaa wanawezaje kuishi Tanzania yaani mipesa kibao na umri umeshaenda baada watafute sehemu ya kuishi American au Europe wao kila siku wanakula vumbi la Tanzania na kudhamini vitimu vya mpira ambavyo havitakuja kuwa na ukubwa wowote kulinganIsha na klabu za Ulaya mpaka dunia inaisha nchi inayonuka kweli unaweza kuwa na mabilioni ya pesa ila ukawa mshamba ila najua Kuna masikini watakuja kuniambia nitafute pesa jamani Mimi pesa sijazipoteza ninazo
 
Tatizo lako unaishi uswahilini na unadhani nchi nzima ipo km kulivyo uswahilini, wenzako wanaishi masaki a.k.a uzunguni barabara zote zina lami maji na umeme havikatiki kwa masaa 24
 
Ungejaliwa kutembea ndio ungejua uzuri wa Tanzania 🇹🇿 ♥
 
Siku ukijua kwamba Tanzania ni nchi nzuri sana kuishi ukiwa na hela kuliko ukiwa kapuku ndio utaelewa kwanini matajiri wengi hawatoki kwenda Ulaya japo wamewekeza huko Ulaya.

Bongo ukiwa na hela kidogo tu nchi itakutambua na wewe kila sehemu utakuwa unapewa VIP treatment. Sio hospitalini, sio bank wala sehemu yoyote ya starehe ama mahotelini. Kero za mamlaka za serikali pia utaishia kuzisikia kwenye vyombo vya habari tu.

Bongo kuna peace of mind sana kama unamiliki utajiri hata wa kawaida tu ila ukawa una affiliates kwenye system ya serikali. Hakuna jambo lako litakwama na msaada ni wa haraka sana ukihitaji.

Kwa masikini bongo ni jehanamu kwa sababu hayo yote niliyoyaandika yatakuwa kinyume chake 🤣🤣🤣! Kwa mtu maskini bongo ndio anapaswa afungashe virago akimbilie ulaya haraka iwezekanavyo.
 
Bakhresa unashindwaje kumjua wewe itakua unaishi porini sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…