Nawashangaa sana watu wanaoniona mimi ni mtu mwenye akili. Sijui wameona nini kwangu?

Nawashangaa sana watu wanaoniona mimi ni mtu mwenye akili. Sijui wameona nini kwangu?

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,253
Reaction score
15,748
Ipo hivi, kuna ofisi moja kubwa sana hapa mujini nilianza kufanya nayo kazi takribani miaka minne hivi iliyopita mpaka sasa.

Wakati huo nikiwa bwana mdogo, ila sasa sijui ilikuwa kuwaje hawa wafanyakazi wenzangu kadri mda ulivozidi kwenda, walikuwa wananichukulia wa tofauti sana, mchapa kazi na mwenye akili sana.

Hata bosi wangu amekuwa akiniambia niandae report za strategy.. ama akiandaa pia report yeyote ananiambia nipitie mimi kama ina make sense.

Ki ukweli kabisa, japo sijawahi kuwaonesha reaction tofauti.. ila huwa nawashangaa sana hawa watu wanavoniona nna akili na mchapa kazi.

Ukweli kuhusu mimi, mimi ni mtu mvivu sana halafu pia nna uwezo wa kuwadanganya watu na kucheza na mawazo yao.. Hicho ndo nlichojaliwa tu... Hawajui yote nnayoyafanya kazini ni maigizo.. Na wao wameingia kingi wananiona mimi kama Einstein..

Nawaonea huruma sana, najua hawatewaza kuijui hii siri milele.. Maana hata watu nliosama nao chuo, nao nimefanikiwa kucheza na akili zao kwa mtindo huo huo..

Wananiona mimi ni mtu mwenye akili sana.. Kila siku lazima wadau wanipigie simu kuniomba ushauri.. Na mimi huwapatia kama vile wachungaji waongo waongo wanavocheza na akili za kondoo wao.

Nimefanikiwa kufika mahali kazini, nikitoa suggestion lazima ifatwe hakuna mwenye ubavu wa kuipinga hadharani. Nimewajengea picha ya kuogopwa na ni ngumu sana wao kujinasua. Unabishana na Genius?

Hayo ndo maisha yangu waungwana.. Huwa najiuliza sana kwanini watu wanakuwa wajinga kuniamini kiasi hicho..

Mimi deep down ni mvivu, sina jipya, sina akili nyingi kihivo... I am just a Conman... Lakini mbona sigunduliki?
 
Kuna usemi wa kibiblia Mithali sikumbuki ngapi.
Ila inasema When Pride begin....

Au
When pride comes, then comes disgrace.....
Ila sijawahi kuwaonesha pride yoyote mkuu... haya ni mawazo huwa nawaza tu
 
Hayo maigizo ndio akili yenyewe.

Werevu ni uwezo wa kubadilika kulingana na Mazingira.
Ujanja ujanja ujanja.

Kitendo cha kujiona huna lolote ndio akili zenyewe hizo

Wenye akili wote hujiona wajinga
Wajinga wote hujiona wenye Akili.

Wenye pesa wengi hujiona wakawaida
Wasio na pesa hujiona wanazo.

Watu wema hujiona Wabaya ndio maana hawajiinui, hata Yesu alikuwa anawashangaa watu wakimuita Mwema😀😀 kesi yako inafanana na kesi ya Yesu.
Yesu yeye anajijua sio mwema anawaambia watu mwema ni Mungu lakini watu wanamuita Mwema.😀😀

Watu Wabaya hujiona Wema ndio maana hujitukuza na kujionyesha wafanyapo mambo Mema.

So ukijiona upo hivyo jua ndivyo ulivyo.

Kama unauwezo wa kuwafanya watu wakuone unaakili na wakakuona unazo basi jua unaakili kweli. Ila kwako binafsi unaziona sio akili kwasababu zipo akili unazitamani haujazifikia
 
Ukishaweza kuwa naambo yafuatayo kibongo bongo unastahili heshima.

1. Kutunza muda
2. Kuheshimu miadi (promise)
3. Kuheshimu watu na kazi
4. Kujitambua nini unatakiwa kufanya na kukikamilisha kwa wakati
5. Kuepuka kuwa mzigo
6. Kuwa msaada hata kazini kwako hata kwa mambo madogo madogo.
7. Kuwa easy going. Masuala ya kazi yana purukushani zake za ghafla, unaweza kutafutwa hata weekend ufanye.
7. Kujitolea. Siyo kufanya kila kitu ulazimishe kulipwa.
 
Labda upo humble sana,na mtu humble kujikweza ni ngumu sana.Yote mazuri unayofanya au uliyonayo unaona kawaida(including high thinking capacity) na huwezi kujisifia kwa yeyote.Na labda ni introvert pia..maana tuna uwezo mkubwa wa kusoma hisia za wengine na uwezo mkubwa wa kuwa manipulative tunapoamua.
 
ujumbe wa kwanza anaopata mtu baada ya kukuona huamua 80% ya jinsi anavyokwenda kukuchukulia,20% ni kile unachokwenda kukifanya mkiwa naye.

tukiwa shule kuna watu walitusumbua kwa mionekano yao tu,ila kwenye matokeo darasani ikawa kinyume,

inawezekana unajiona upo upo tu,lakini kumbe watu wanafeel uzito flani wakikuona,ukijumlisha na mambo unayoyafanya ndio kabisaa,
mfano mwingine ni mzee aliekuwa mkuu awamu iliyopita akasataafu,hata asingepata cheo kile angetokea kukubalika tu kwa muonekano,ila bahati mbaya akaja kuharibu kwenye kuwasilisha kilichotazamiwa.
 
Sasa Kama unacheza na akili za watu na unafahamu kuwa unawachezea akili utasemaje huna akili?
Au Kwanza nikuulize akili ni nini?
 
(Ukweli kuhusu mimi, mimi ni mtu mvivu sana halafu pia nna uwezo wa kuwadanganya watu na kucheza na mawazo yao.. Hicho ndo nlichojaliwa tu... Hawajui yote nnayoyafanya kazini ni maigizo.. Na wao wameingia kingi wananiona mimi kama Einstein..)

[emoji121]mtu mwenye uwezo wa kuwadanganya wenye uwezo ni mtu mwenye akili lakini anaitumia vibaya.
Hakuna kazi ngumu kama kuwa muongo mwaminifu na asiyeyumba....hapa nitaeleweka na waongo wenye akili....
Kwaherini
 
Kifupi upo smart ki haiba.

Siku zote u smart wa kimuonekano ndiyo mtaji wa watu wote wabaya na wahalifu.

Mtu yeyote tapeli, mwizi na hata wachawi hutumia sana hii mbinu ya kujisoap soap!

Kuna ushauri ninataka nikupe hapa!

Jambo la kwanza mshukuru Mungu kwa kukustiri, pia wapende na kuwaheshimu sana hao wahanga wako, usiwaone wajinga na mabwege kama unavyowachukulia kirahisi namna hiyo.

Mambo ya kughushi tabia isiyo yako na kisha kuwaona watu uliowahadaa kuwa ni wajinga, huo ni upungufu wa utimilifu!

Kumbuka kuna watu walighushi vyeti, vikawapeleka kozi kusomea ujuzi, wakafaulu vizuri na kuajiriwa kazi zenye heshima kwa sifa zisizowastahili, lakini baadaye waliumbuka kirahisi sana na mpaka leo wanajuta kishenzi!

Uongo waweza kudanganya watu wote popote, lakini hauwezi kudanganya watu wote siku zote milele.

Ipo siku uzandiki na unafiki wako huo utafikia kikomo tu, labda Mungu akuue mapema usishuhudie nikuelezacho hapa.

Na siku utakapogundulika ubabaishaji wako huo, utadharaulika sana hadi mwenyewe utajiona si lolote kama choo na utakosa pa kushika!

Kwanini usijirekebishe muda huu ili uendane na uhalisia wa sifa ambazo watu wanakuchukulia?

Umebweteka kwa kuridhika kuwa wewe ni mjanja'eeh, bingwa?

Shauri yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usikute kajamaa kana GPA ya karai, tena karai lenyewe limetoboka toboka kwa sups za kutosha fuso
 
Back
Top Bottom