Kifupi upo smart ki haiba.
Siku zote u smart wa kimuonekano ndiyo mtaji wa watu wote wabaya na wahalifu.
Mtu yeyote tapeli, mwizi na hata wachawi hutumia sana hii mbinu ya kujisoap soap!
Kuna ushauri ninataka nikupe hapa!
Jambo la kwanza mshukuru Mungu kwa kukustiri, pia wapende na kuwaheshimu sana hao wahanga wako, usiwaone wajinga na mabwege kama unavyowachukulia kirahisi namna hiyo.
Mambo ya kughushi tabia isiyo yako na kisha kuwaona watu uliowahadaa kuwa ni wajinga, huo ni upungufu wa utimilifu!
Kumbuka kuna watu walighushi vyeti, vikawapeleka kozi kusomea ujuzi, wakafaulu vizuri na kuajiriwa kazi zenye heshima kwa sifa zisizowastahili, lakini baadaye waliumbuka kirahisi sana na mpaka leo wanajuta kishenzi!
Uongo waweza kudanganya watu wote popote, lakini hauwezi kudanganya watu wote siku zote milele.
Ipo siku uzandiki na unafiki wako huo utafikia kikomo tu, labda Mungu akuue mapema usishuhudie nikuelezacho hapa.
Na siku utakapogundulika ubabaishaji wako huo, utadharaulika sana hadi mwenyewe utajiona si lolote kama choo na utakosa pa kushika!
Kwanini usijirekebishe muda huu ili uendane na uhalisia wa sifa ambazo watu wanakuchukulia?
Umebweteka kwa kuridhika kuwa wewe ni mjanja'eeh, bingwa?
Shauri yako.
Sent using
Jamii Forums mobile app