PreGE2025 Nawashauri Viongozi na Watu hawa wafuatao wakachukue fomu za kugombea Ubunge

PreGE2025 Nawashauri Viongozi na Watu hawa wafuatao wakachukue fomu za kugombea Ubunge

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Lucas acha tabia ya uchawa na kujipendekeza kwa wanaume wenzio!
Unachotakiwa kufanya ni kujiamini na kujipendekeza kwanza wewe!
Wewe ulizaliwa kubeba wenzio badala ya kujibeba? tabia za kimama kweli hizi!
Hakuna ubaya wa mimi kuwapendekeza hao.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Baada ya kufunguliwa Kwa pazia na kupulizwa kwa Filimbi ya kuchukua Fomu za Kuomba kuteuliwa nafasi za kugombea Udiwani na ubunge ndani ya CCM.

Nilikuwa nashauri na kuwashauri viongozi na watu hawa wafuatao wachukue ,kujaza na kurejesha Fomu za Kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge kupitia chama cha Mapinduzi yaani CCM

Nimeanza na Wachache ila nitakuwa naendelea kutaja majina Mengine kwa kadiri ya uchambuzi wangu . Kwa Leo naanza na hawa Wafuatao.

Mheshimiwa CPA Amoss Makalla. Huyu kwa sasa ni Katibu wa Itikadi, uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa. Huyu pia Msomi wa mahesabu amekuwa mkuu wa mikoa mbalimbali hapa Nchini na amefanya vizuri sana katika mikoa na maeneo yote ambayo amewahi kuongoza kama mkuu wa mkoa .lakini pia amewahi kuwa mbunge pia na hata alipojaribu kugombea tena kwenye kura za Maoni uchaguzi uliopita alishinda japo hakupata nafasi ya kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM. Nilikuwa namshauri agombee Ubunge Maana naiona Sauti yake na mchango wake Ukihitajika ndani ya Bunge letu na pengine ndani ya Baraza la Mawaziri.

Mheshimiwa Danieli Chongolo. Huyu kwa Sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe . Amewahi pia kuwa katibu Mkuu wa CCM pamoja na kuwa mkuu wa wilaya . Huyu pia naiona nafasi yake na Sauti yake ikihitajika pale Bungeni na Pengine ndani ya Baraza la Mawaziri.

Mheshimiwa Paul Makonda. Huyu kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha . Amewahi pia kuwa katibu wa itikadi, uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa. Lakini pia amewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam pamoja na kuwa mkuu wa wilaya. Hivyo anao uzoefu ndani ya serikali na ndani ya chama. Na anajua matatizo ya wananchi na namna mbunge na muwakilishi wa wananchi anapaswa kuwa. Naona nafasi yake na Sauti yake ikihitajika pale Bungeni na Pengine ndani ya Baraza la Mawaziri .

Mheshimiwa Juma Homela. Huyu kwa sasa ni RC Mkoa wa Mbeya. Amewahi pia kuwa mkuu wa wilaya . Ameiongoza Mbeya kwa Muda mrefu na amepata bahati ya kuaminiwa na kutohamishwa katika Mkoa huo maarufu hapa Nchini na wenye watu wenye misimamo na Elimu ya kutosha. Naona Sauti yake ikihitajika pale Bungeni na Pengine ndani ya baraza la Mawaziri.

Mheshimiwa Jokate Urban Mwegelo. Huyu kwa Sasa ni katibu Mkuu wa UVCCM Taifa. Amewahi kuwa pia katibu Mkuu wa UWT Taifa. pamoja na kushika ukuu wa wilaya katika maeneo mbalimbali hapa Nchini kama vile kisalawe na Temeke na huko Korogwe Tanga. Huyu Dada Naomba Usiku na Mchana ili Mungu Amsaidie kuingia Bungeni. Namuomba Sana tena sana Mungu Amsaidie huyu Dada kuingia Bungeni kwa njia au mlango wowote ule. Iwe ni kwa kuteuliwa au viti maalumu au kupitia jimboni. Natamani aingie Bungeni ili kuwapa hamasa watoto wa kike Kama ambavyo Leo hii tumeona namna Rais wetu Mpendwa amekuwa mfano bora wa uwezo mkubwa alionao Mwanamke kiuongozi. Naona sauti yake ikihitajika pale Bungeni na Pengine ndani ya baraza la Mawaziri.

Mheshimiwa David Kafulila. Huyu kwa Sasa ni mkurugenzi mtendaji wa PPP. Amewahi pia kuwa RC Simiyu,pamoja na kuwa RAS mkoa wa Songwe lakini pia amewahi kuwa Mbunge Mwaka 2010-2015. Huyu pia naiona Sauti yake ikihitajika pale Bungeni na Pengine ndani ya Baraza la Mawaziri.

Mheshimiwa Dokta Dorothy Gwajima. Huyu kwa sasa ndiye waziri anayeongoza kwa sasa kufuatilia kwa ukaribu sana vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa aina yoyote ile. Ni waziri mwenye ngozi ngumu sana pale anapokosolewa au kushambuliwa. Ni kiongozi ambaye amekuwa mstari wa mbele siku hadi siku katika kuhakikisha anafanyia kazi na kufuatilia na kuchukua hatua za haraka sana pale linapojitokeza jambo lililo kinyume na maadili au ukatili au unyanyasaji wa aina yoyote ile. Naiona sauti yake ikihitajika pale Bungeni na hata kuendelea kuaminiwa kuwa ndani ya Baraza la Mawaziri. Nimependekeza kwa sababu kwa sasa ni Mbunge wa kuteuliwa katika zile nafasi kumi za Rais. Hivyo natamani kuona kwa sasa akichukua Fomu ya kuomba kuteuliwa na CCM yetu kugombea Ubunge.

Majina Mengine nakuja kuendeleza hapa hapa kwenye Uzi huu. Lakini Ikumbukwe nimejikita katika watu ambao kwa sasa siyo wabunge na hawapo Bungeni. Mheshimiwa Dkt Dorothy Gwajima nimemtaja na kumuweka hapa kwa sababu kwa sasa hana jimbo na aliingia kwa kuteuliwa Ubunge na kisha uwaziri.

Na wewe mwana CCM mwenzangu kama kuna mtu ambaye Ungetamani kumuona Bungeni .unaweza kumtaja tu. Ikumbukwe ya kuwa wanapoingia watu wenye uwezo mkubwa wa kiuongozi inamsaidia na kumpa uwanja mpana Mheshimiwa Rais hata katika uteuzi wa Baraza lake la Mawaziri. Lakini pia unaweza mfanya hata Rais aachane na kuteua mtu nje ya Bunge katika zile nafasi kumi alizonazo kikatiba kwa sababu anakuwa na uwanja mpana na kuchagua waziri miongoni Mwa Wabunge waliopo Bungeni.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Wewe ZUZU, mwaka huu 2025 hakuna UCHAFUZI. Tutafanya juu chini kuuzuia usifanyike.
 
Hamna uwezo wala ubavu huo wa kuzuia uchaguzi
Hakuna uwezo wakati Mama yako tayari ameingiwa na hofu kubwa? Huyu ni Rais wa hovyo kabisa kupata kutokea Tanzania. Bahati njema ni kwamba hakupigiwa kura, ni Rais wa URITHI tu.
 
Hakuna uwezo wakati Mama yako tayari ameingiwa na hofu kubwa? Huyu ni Rais wa hovyo kabisa kupata kutokea Tanzania. Bahati njema ni kwamba hakupigiwa kura, ni Rais wa URITHI tu.
Huna adabu wewe.
 
Kwani lissu Aliposhinda ubunge 2010 na 2015 alikuwa anatangazwa na tume ipi ya uchaguzi?
Kwani wewe nguo uliyovaa 2010 bado unaivaa hadi sasa kunguni wa mama

?

Unaelewa dhana ya kubadilika ni kukua ,tume ni ile ile ila ushenzi wa 2010 sio sawa na ushenzi wa 2019,2020 na 2024 hivyo imeonelewa reform sasa zifanyike kudhibiti uhuni huu usijirudie.
 
Back
Top Bottom