Nawashukuru Watanzania, Mwenyenzi kanijaalia afya njema

Nawashukuru Watanzania, Mwenyenzi kanijaalia afya njema

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
761
Reaction score
6,985
Ukiishi ukapata pumzi na maarifa ya kutambua mema na mabaya mshukuru Sana Mungu Kama unaamini yupo.

Ukipewa nafasi yakutubu tubu, ukipewa nafasi yakuhudumia watu hudumia watu bila kudhani una muda mbele wakuishi.

Lipo fumbo kubwa Sana Kati uzima na ugonjwa lakini lipo fumbo kubwa zaidi Kati ya uzima na kifo.

Kupitia fumbo hili ndipo waliowazima ufa na wagonjwa upona. Kupitia fumbo hili pia ndipo wasioamini ujiloweka kwenye dhambi na wenye dhambi upata nafasi ya kuokoka.

Lakini lipo fumbo kubwa la kiimani katika ulimwengu huu. Viongozi wa dini waliowengi ibada yao imekuwa dhidi ya matajiri na wenye madaraka na si ibada ya kumwabudu Mwenyenzi Mungu. Kwao wao uongozi wa dini nikumsujudia na kujiona mkubwa anapokaa mezani pa wanasiasa au wenye fedha.

Zamani viongozi wa dini walikuwa wanapata faraja ndani ya nyumba za ibada. Leo viongozi wa dini wamekimbilia majukwaa ya kisiasa na siyo kila siasa Bali siasa ya anayetawala. Tuliombee Taifa na tuombeane tusifike mahali tukabeba nafsi za viongozi wa dini za kuabudu watu bali tujiwekee nadhiri ya siku zote kuacha kuwasikiliza viongozi wa dini na kumsikiliza Mungu.

Nafahamu Mungu atuwezi kuzungumza naye ila naamini upeo uliopewa wa kujua mema na mabaya ndio upeo pekee unaoweza kukufanya uzungumze na Mungu. Pale unapotenda mema amini unazubgumza na Mungu na pale unapotenda mabaya amini unajadiliana na kushauriana na shetani.

Mliomba na kuendelee kuipigania Katiba mpya, nashukuru nimerudi nakukuta katiba mpya kwa tafsiri ya tunaowalipa mshahara ni UGAIDI. Napenda nikubaliane nao kwamba kupitia laana ya usikivu na kiburi cha kuona Wana muda mrefu wa kuishi katiba ni UGAIDI. Lakini kupitia roho mtakatifu katiba ni msingi wakuongozana kuelekea kwenye haki na ambapo mwisho wake Ni kuwa na jamii yenye amini.

Ashukuriwe atoae pumzi na ajuaye lini mwiso wetu. TUSIACHE KUJIANDAA MAANA SI KILA MMOJA ATAPATA NAFASI NILIYOPATA.
 
Welcome back mkuu, me nakuelewa sn,ambaye hakuelewi achana naye.

Inashangaza sn,halafu watu si wajinga sikuhizi.Kumbambikia mtu kesi kijinga hivi ni ushamba.

Watakufa et hawa watu jamani,mbona hawajifunzi?

Watanzania sikuhizi maombi yao ni makali wakiamua kumshitakia Mungu
 
Ashukuriwe na atukuzwe mwenyezi mungu mtukufu! Kwake yeye hakuna linaloshindikana. Hongera sana bi beatrice kwa kupata afya njema na kurudi kundini.
 
Ukiishi ukapata pumzi na maarifa ya kutambua mema na mabaya mshukuru Sana Mungu Kama unaamini yupo.

Ukipewa nafasi yakutubu tubu, ukipewa nafasi yakuhudumia watu hudumia watu bila kudhani una muda mbele wakuishi....
Mkuu watu walituaminisha asilimia 100 kuwa wewe ni Marehemu Padri Privatus Karugendo! Hatari sana.
Welcome back to the home of great sinkers thinkers mkuu.
 
Ukiishi ukapata pumzi na maarifa ya kutambua mema na mabaya mshukuru Sana Mungu Kama unaamini yupo.

Ukipewa nafasi yakutubu tubu, ukipewa nafasi yakuhudumia watu hudumia watu bila kudhani una muda mbele wakuishi....
Karibu Tena Mwanakikundi... Ashukuriwe Mungu Kwa Utetezi wake Kwako... Sifa na Utukufu Kwake. Nimefurahi Sana Sana upo Tena Jukwaani Nilihuzunika Sana nilikuwaza Sana Asante Pia kwa Moyo wako wa Ujasiri Ukakishinda Kifo.

Ulikikabili kwa Ushujaa mwingi na Ndiyo Maana kilifyata Mkia. Bravo Madame Beatrice. Karibu Sana Uendeleze wito wako Mkuu wa Kuisemea Jamii.
 
ule uzi wako mkuu nilipata sonona sana!
niliteseka sana juu yako nikifikiria hali uliyokuwa nayo!
mungu ni mwema sana.tunazidi kukuombea uimarike zaidi kiafya.
 
Back
Top Bottom