Ukiishi ukapata pumzi na maarifa ya kutambua mema na mabaya mshukuru Sana Mungu Kama unaamini yupo.
Ukipewa nafasi yakutubu tubu, ukipewa nafasi yakuhudumia watu hudumia watu bila kudhani una muda mbele wakuishi.
Lipo fumbo kubwa Sana Kati uzima na ugonjwa lakini lipo fumbo kubwa zaidi Kati ya uzima na kifo.
Kupitia fumbo hili ndipo waliowazima ufa na wagonjwa upona. Kupitia fumbo hili pia ndipo wasioamini ujiloweka kwenye dhambi na wenye dhambi upata nafasi ya kuokoka.
Lakini lipo fumbo kubwa la kiimani katika ulimwengu huu. Viongozi wa dini waliowengi ibada yao imekuwa dhidi ya matajiri na wenye madaraka na si ibada ya kumwabudu Mwenyenzi Mungu. Kwao wao uongozi wa dini nikumsujudia na kujiona mkubwa anapokaa mezani pa wanasiasa au wenye fedha.
Zamani viongozi wa dini walikuwa wanapata faraja ndani ya nyumba za ibada. Leo viongozi wa dini wamekimbilia majukwaa ya kisiasa na siyo kila siasa Bali siasa ya anayetawala. Tuliombee Taifa na tuombeane tusifike mahali tukabeba nafsi za viongozi wa dini za kuabudu watu bali tujiwekee nadhiri ya siku zote kuacha kuwasikiliza viongozi wa dini na kumsikiliza Mungu.
Nafahamu Mungu atuwezi kuzungumza naye ila naamini upeo uliopewa wa kujua mema na mabaya ndio upeo pekee unaoweza kukufanya uzungumze na Mungu. Pale unapotenda mema amini unazubgumza na Mungu na pale unapotenda mabaya amini unajadiliana na kushauriana na shetani.
Mliomba na kuendelee kuipigania Katiba mpya, nashukuru nimerudi nakukuta katiba mpya kwa tafsiri ya tunaowalipa mshahara ni UGAIDI. Napenda nikubaliane nao kwamba kupitia laana ya usikivu na kiburi cha kuona Wana muda mrefu wa kuishi katiba ni UGAIDI. Lakini kupitia roho mtakatifu katiba ni msingi wakuongozana kuelekea kwenye haki na ambapo mwisho wake Ni kuwa na jamii yenye amini.
Ashukuriwe atoae pumzi na ajuaye lini mwiso wetu. TUSIACHE KUJIANDAA MAANA SI KILA MMOJA ATAPATA NAFASI NILIYOPATA.
Naam, Mimi ni mwanachama wa muda mrefu hapa kwenye ukurasa wa Siasa. Nimetoa mchango wangu kwa umoja huu kupitia ukurasa huu. Nimerekebisha baadhi ya mambo kutokana na hoja zangu na niseme tu nimekuwa nikifarijika sana pale ninaposhauri au kutoa hoja ikaleta positive impact kwenye jamii.
Nimefika kikomo cha kushiriki nanyi, nimefika wakati ambao bila ridhaa yangu nawajibika kukaa pembeni bila kuandika Wala kuona chochote kuhusu hata wale watakaosoma ujumbe huu. Nafika ukomo na nauona ukomo wangu.
Ninapoaga leo hapa tarehe 23/06/2021 saa 23: 15 usiku naaga kwa uchungu mkubwa kwamba moja ya Jambo nililopigania kwenye jukwaa, kwenye jamii na kwenye mitandao ya kijamii halijafanikiwa kutokea na naamini sitoweza kushuhudia likitokea. Jambo ilo si jingine Bali ni KATIBA MPYA YA JMT.
Nilitamani nimshirikishe Mwalimu Nyerere juu ya hatua hii huko alipo endapo ningekutana naye lakini nasikitika kwamba sitoweza kumwambia chochote juu ya agenda hii. Ni maumivu makubwa.
Niliipigania Katiba baada ya kuona kwamba mfumo wakusimamia haki nchini haupo Tena kwenye mategemeo ya sheria za nchi. Mfumo huo toka enzi ya Mkapa hadi leo hii awamu ya sita umebaki kutawaliwa na maamuzi ya mtu mmoja ambayo ni maamuzi ya Mkuu wa nchi.
Niliipigania Katiba mpya baada ya kuona taifa langu linazidi kuongeza Kinga za kushtakiwa kwa kundi la wanasiasa na Watumishi wa umma. Mkakati huu wakutochukuliwa hatua za kisheria kwa viongozi utaliua taifa na ndipo nilipoona natakiwa kusimia hoja ya Katiba mpya itakayotamka na kutekelezwa kwa amri au takwa la binadamu wote wapo sawa chini ya sheria.
Nilijaribu na naondoka bila kuiona, naamini waliobaki watazidi kuisimamia hii na itapatikana kabla Taifa halijapoteza kabisa imani miongoni mwa wananchi na kuanza kusambaratika.
Ninaponyamaza na nikiwa katika maumivu makubwa nimepata nguvu yakuuandikia ulimwengu kwamba Tanzania inahitaji katiba mpya.
Kwa Mhe. Rais, kwa Hali ilipofikia Sasa, maendeleo pekee unayoweza kuwarithisha Watanzania wakiwemo watoto wako na wajukuu ni katiba mpya. Jenga barabara, vivuko nk lakini tambua kiu ya umma wa Watanzania inahitaji katiba inayotokana na kizazi kilichopo Sasa.
Wasaidie Watanzania, wape katiba mpya. Anzisha mchakato, la sivyo kelele na mwangwi wa kilio cha Watanzania kitaambatana nawe Kama kinavyoambatana na mzee Kikwete hata baada ya kustaafu. Naondoka mie, nakuomba Jambo naamini sitoiona katiba hiyo ila wape wananchi katiba mpya.
Niwashukuruni sana na niwaombe msisite kuendelee kumkumbusha kuhusu maumivu yangu juu ya Tanzania mpya. Endapo lolote litatokea may be ntarudi ila nimefika ukomo. Mwenyenzi Mungu mtoa maarifa na njia akawajaze ufunuo na maono ya mwisho mwema Kama Mimi. Mkaondoke mkiwa kwenye toba na siyo mkiwa dhambini.
Naitwa Beatrice Kamugisha (nick name), naandika kutoka Regency Dar es salaam Tanzania.
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827]kuna utofauti mkubwa sana kati ya haya mabandiko mawili hasa kwenye mpangilio wa sentence, sarufi na vitenzi