Nawashukuru Watanzania, Mwenyenzi kanijaalia afya njema

Hongera sana mkuu kwa kupona! Maana ile siku baada tu ya kutoa ule waraka wako, ghafla na Padre Privatus Karugendo naye si akatangulia mbele ya haki! 😪

Mbaya zaidi na yeye alilazwa hapo hapo Regency ulipokuwepo wewe!! Kilichofuatia hapo, ilikuwa ni kuunganisha tu dots!! 🙄
 
Jamani wewe dada/kaka, watu walilia humu wakaandika RIP, kumbe hukufa[emoji848]basi sawa, karibu tena njamvini, tunamtukuza Mungu kwa ajili yako
 
Niliamini Beatrice ana mwandiko tofauti na Padre. Hata kama Padre nilimsoma mara ya mwisho miaka kadhaa nyuma nikiwa na akili ndogo ila alikuwa anapenda makala ndefu na zinahitaji utulie kiakili
 
Simjui huyu mtu lakini niliumia sana ule uzi aliposema yupo hospital, na aliposema hana uhakika na kesho akatusisitiza tupambanie katiba hafu akaja baharia akasema amekufa.

Aisee niliumia ova namjua. Hafu leo anakuja hivi. Okay, kama ni wewe Mungu ni mwema.
 
Tanzania Sasa hivi maombi ni kifo, Ni Kama tumeondoka KUJADILI maendeleo tunajadili kifo kupitia mijadala ya covid, mijadala ya utekaji., Viongozi wanaombewa kifo, wananchi wanaombeana kifo yaani Taifa mitandaoni nikuombeana kifo mwanzo mwisho

Viongozi w dini wakemeeni waumini waache kuhubiri kifo na kukitukuza kifo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…