Nawashukuru Watanzania, Mwenyenzi kanijaalia afya njema

Umefufuka ukakuta msemo ulio kwenye chati ni Ugaidi, polisi wetu wakikukuta na kibiriti mfukoni watakwambia unataka kuchoma nyumba ya watu.
Sa kibiriti mfukoni cha kazi gani?
 
Nafahamu Mungu atuwezi kuzungumza naye ila naamini upeo uliopewa wa kujua mema na mabaya ndio upeo pekee unaoweza kukufanya uzungumze na Mungu. Pale unapotenda mema amini unazubgumza na Mungu na pale unapotenda mabaya amini unajadiliana na kushauriana na shetani.
 
Twambie mji wa yerusalem mbinguni kukoje,moto wa milele upo very kweli au stori za vijiweni
 
Hii forum sasa tutaanza kukosa imani na mnayotuandikia humu. Si ulituaga wewe na wosia ukatuachia? Leo umefufuka ?
 
uliamua kuweka id zako zote mbili wazi
ile uliyojitangaza mfu na hii
 
Naam, Mimi ni mwanachama wa muda mrefu hapa kwenye ukurasa wa Siasa. Nimetoa mchango wangu kwa umoja huu kupitia ukurasa huu. Nimerekebisha baadhi ya mambo kutokana na hoja zangu na niseme tu nimekuwa nikifarijika sana pale ninaposhauri au kutoa hoja ikaleta positive impact kwenye jamii.

Nimefika kikomo cha kushiriki nanyi, nimefika wakati ambao bila ridhaa yangu nawajibika kukaa pembeni bila kuandika Wala kuona chochote kuhusu hata wale watakaosoma ujumbe huu. Nafika ukomo na nauona ukomo wangu.

Ninapoaga leo hapa tarehe 23/06/2021 saa 23: 15 usiku naaga kwa uchungu mkubwa kwamba moja ya Jambo nililopigania kwenye jukwaa, kwenye jamii na kwenye mitandao ya kijamii halijafanikiwa kutokea na naamini sitoweza kushuhudia likitokea. Jambo ilo si jingine Bali ni KATIBA MPYA YA JMT.

Nilitamani nimshirikishe Mwalimu Nyerere juu ya hatua hii huko alipo endapo ningekutana naye lakini nasikitika kwamba sitoweza kumwambia chochote juu ya agenda hii. Ni maumivu makubwa.

Niliipigania Katiba baada ya kuona kwamba mfumo wakusimamia haki nchini haupo Tena kwenye mategemeo ya sheria za nchi. Mfumo huo toka enzi ya Mkapa hadi leo hii awamu ya sita umebaki kutawaliwa na maamuzi ya mtu mmoja ambayo ni maamuzi ya Mkuu wa nchi.

Niliipigania Katiba mpya baada ya kuona taifa langu linazidi kuongeza Kinga za kushtakiwa kwa kundi la wanasiasa na Watumishi wa umma. Mkakati huu wakutochukuliwa hatua za kisheria kwa viongozi utaliua taifa na ndipo nilipoona natakiwa kusimia hoja ya Katiba mpya itakayotamka na kutekelezwa kwa amri au takwa la binadamu wote wapo sawa chini ya sheria.

Nilijaribu na naondoka bila kuiona, naamini waliobaki watazidi kuisimamia hii na itapatikana kabla Taifa halijapoteza kabisa imani miongoni mwa wananchi na kuanza kusambaratika.

Ninaponyamaza na nikiwa katika maumivu makubwa nimepata nguvu yakuuandikia ulimwengu kwamba Tanzania inahitaji katiba mpya.

Kwa Mhe. Rais, kwa Hali ilipofikia Sasa, maendeleo pekee unayoweza kuwarithisha Watanzania wakiwemo watoto wako na wajukuu ni katiba mpya. Jenga barabara, vivuko nk lakini tambua kiu ya umma wa Watanzania inahitaji katiba inayotokana na kizazi kilichopo Sasa.

Wasaidie Watanzania, wape katiba mpya. Anzisha mchakato, la sivyo kelele na mwangwi wa kilio cha Watanzania kitaambatana nawe Kama kinavyoambatana na mzee Kikwete hata baada ya kustaafu. Naondoka mie, nakuomba Jambo naamini sitoiona katiba hiyo ila wape wananchi katiba mpya.

Niwashukuruni sana na niwaombe msisite kuendelee kumkumbusha kuhusu maumivu yangu juu ya Tanzania mpya. Endapo lolote litatokea may be ntarudi ila nimefika ukomo. Mwenyenzi Mungu mtoa maarifa na njia akawajaze ufunuo na maono ya mwisho mwema Kama Mimi. Mkaondoke mkiwa kwenye toba na siyo mkiwa dhambini.

Naitwa Beatrice Kamugisha (nick name), naandika kutoka Regency Dar es salaam Tanzania.


[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827]kuna utofauti mkubwa sana kati ya haya mabandiko mawili hasa kwenye mpangilio wa sentence, sarufi na vitenzi
 
Kumbe JF mbali ya kila MTU kuwa na maisha mazuri, kazi nzuri, gari nzuri, ndoa nzuri kuna wengine wameenda mbali zaidi. Yaani wameona hayo yote hayatoshi, wameamua kufa na kufufuka!
Mkuu utanilipa mbavu zanguuuu🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kizunguzungu! INAWEZA KUWA huyu sio yule original?
 
Duuh ule waraka wako sikusoma mpaka mwisho niliumia kweli na ipo siku nilipita humu nikasoma maandishi ya umefariki daah nikauzunika zaidi aisee...karibu tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…