Nawashukuru wote mliochangia uzi wangu mwaka jana mwezi wa 8

Mkeo akizaa ng'ombe usije kuanza kulialia, uendelee kuwa surprise hvy hvy
HAPO SASA LIMETIMIA NENO, USIMWAMBIE HAYA MAMBO MTU ASIEKUA NA HIUO EXPERIENCE.

KWETU TIBA HUFUATI MIMBA/MTOTO

KULE UNAFUATA TIBA KUTOA KIKWAZO ILI UTAFUTE MTOTO BILA KIKWAZO/KIZUIZI KILICHOKUWEPO.

HAKUNA MGANGA WALA YOYOTE YULE ANAETOA MTOTO.
 
"Watoto wa dawa" ndiyo huzaliwa kama hivi.

Msipofanikiwa kuongeza wengine, jua huyo ni MTOTO WA DAWA.

Huwa wana future isiyo nzuri sana.

Hivyo chukua hatua za ziada za kumnusuru huyo dogo!
Hayo maneno wengi wanakosea, HAKUNA MTOTO WA DAWA LABDA UWE UMEENDA KWA MGANGA WA KIENYEJI WA KIBUYU ( WA MASHARTI) SIWEZI NIKAZUNGUMZIA HILO MAANA SIJAWAHI KWENDA HUKO.

SIKILIZA YA DUNIA.

HAKUNA DAWA INAYOTUMIWA MTU APATE MIMBA NEVER! MIMBA NI YAI LINALORUTUBISHWA NA MBEGU ZA KIUME HAKUNA KINGINE NNJE YA HILO.

NDIO MANA NASEMA MTU AANZIE HOSPITAL, MAANA MKEO ANAWEZA KUTOLEWA KIKWAZO NA BADO ASIPATE MIMBA (SHIDA INAWEZA IKAWA MBEGU ZA MWANAUME)
 
Labda nitoe elimu kidogo.

Kuna watabibu wa mitoshamba wa aina 3 au zaidi.

1. Wa mizimu NA masharti ( hawa sio wazuri pia sijawahi kwenda)
2. Waganga wa kibuyu (hawa ni kama wachawi tu)
3. Wasoma kisomo/masheikh
Wanajua dawa za sunna na mizizi ya porini ( WA AINA HII NDIO ALIENISAIDIA)
 
JAPO MPAKA SASA JAMIIFORUMS NA UZI HUU KUMEKUA NA MASIHARA BILA UTU UZIMA NA WAHITAJI, NISEME NENO MWAKA WOWOTE ULE MWENYE UHITAJI AKIONA UZI HUU ASOME VIZURI USHAURI WANGU KUNA KITU ATAKIPATA.

GOODBYE 👋
 
Umetuandikia kwa herufi kubwa sehemu nyingi sana haswa pale kwenye ushauri wakuhangaika kutafuta tiba. Hii unamaanisha kitu Gani mkuu mbemba🤣🤣
 
Mimi na wife tulipoacha kujitia stress kuhusu mtoto na kuacha kuhangaika kila sehemu na kuamini kwamba ipo siku Mungu atabless, na kweli tukapata mtoto
 
Mkuu kabla hijapost uwe unasoma wewe kwanza ulichoandika..kisha ufanyie editing...angalia ulichoandika
 
Umeandika vizuri sana na kwa hisia, nimekuelewa Mkuu
 
Naelewa mkuu.

Kwanza naomba niseme hapa tunaelimishana tu, I mean no malice at all.

Jiulize why umehangaika kooote lakini ukaenda kufanikiwa Pangani kwa masheikh?

Kwa nini kwa manabii na maaskofu na mapadre ilishindikana?

Kumbuka waganga wa kienyeji sio lazima wavae tunguli na wakupe mitishamba au mizizi au wakuchanje chale. Hata hao wa visomo ni waganga waliochangamka maana tunguli zao ni za kisasa ikiwemo kutumia MAJINI.

Cha msingi hapa, mleeni mtoto wenu kwa makini sana.
 
JAPO MPAKA SASA JAMIIFORUMS NA UZI HUU KUMEKUA NA MASIHARA BILA UTU UZIMA NA WAHITAJI, NISEME NENO MWAKA WOWOTE ULE MWENYE UHITAJI AKIONA UZI HUU ASOME VIZURI USHAURI WANGU KUNA KITU ATAKIPATA.

GOODBYE 👋
Upo sahihi kabisa maana kunaleo na kesho, toa location ya mtaalam ikikupendeza weka na jina lake. Mwenye changamoto zake akapate kusaidiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…