Nawashukuru wote mliochangia uzi wangu mwaka jana mwezi wa 8

🤣🤣🤣 Mzee umemkomalia huyo jamaa hadi kakimbia, ila uhalisia ni kwamba wanawake wanafungwa sana wasizae kichawi, na vifungo hivyo vikotolewa wanazaa vzur tuu.

Kuna jamaa yangu yeye mke wake alitupiwa jini cheketu, hilo mimba ikiwa changa tu linakula, yani hapo mpaka kupata mtoto ilibidi wapate mtaalamu wa kutoa ile shida maana hata usiku mke wake alikua halal ni kama alikua na jini mahaba.

Wanawake wengi wanatupiwa mnyama anaenda kukaa kwenye kizazi, chakula chake inakua ni kula mayai yanayoanza kurutubishwa.

Kuna wengine wanatupiwa kitu kinakaa kwenye kizazi kazi yake ni kupuliza hewa chafu kuharibu mayai yasikomae.

Mambo ni mengi sana mkuu.
Ila kama huyo jamaa alivyosema hapo juu kama mtu huamini haya mambo na hujapitia ni ngumu sana kuelewa na kuamini, mimi sijapitia shida hizo lakini nina washkaji sio chini ya watatu walikua na changamoto.

Na huyo jamaa kwa maelezo yake itakua hajaenda kwa mganga wa kienyeji ila kaenda kwa wale mashehe wanaotibu na dawa za suna.
 
Nimekuelewa mkuu😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…