Sodoku
JF-Expert Member
- Feb 3, 2016
- 1,271
- 2,903
1. Anna Shayo - huyu dada nlisoma naye Sangu Secondary School Form Five. Alikuwa akiishi Mwanjelwa kwa dada yake (kama sijakosea) naye that time alikuwa kidato cha 5 masomo ya Biashara au Sanaa. Sikumbuki vizuri.lakini moja ya matukio ambayo nlikuwa naye ni siku ambayo nlipiga naye picha tukiwa tumeandamana kwenda kwa Mkuu wa Mkoa kupinga Mwalimu Mkuu aliyepo kuondolewa na Kuletwa Bukuku. ( Tulikuja kushukuru Ujio wa Bukuku baadaye) popote alipo Anna Shayo naomba tuwasiliane. Nmemtafuta sana huyu dada bila Mafanikio.
2. Domina Chambi - huyu ni mdada ambaye nilisoma naye shule ya Laela Mkoani Sumbawanga akiwa kidato cha Tatu. Alikuwa dada mmpole na mwenye nidhamu sijapata ona. Toka miaka hiyo sijaweza tena pata mawasiliano naye.miaka ya 1990s tulikuwa tukiwasiliana kwa barua tu.
3. Theresia. Huyu nlimfahamu miaka ya 1980s nlipoenda likizo mbeya. Tulikuwa tunaishi nyumba zetu zinatizamana. Alikuwa na dada yake Vicky na Kaka zake Mashaka na Godfrey. Pia mdogo wake Lwiza/Luiza.
Ni mdada ambaye tulikuwa marafiki sana.miaka ya 1990s nlienda mtafuta tukaonana na baadaye kupotezana tena. Kama ndugu zake wapo humu tafadhari naomba tuwasiliane.
Birthday yangu inapokaribia siku kadhaa zijazo ngependa niweze washirikisha watu hawa kwa vyovyote vile ntakavyoweza niwakumbushe wao bado ni marafiki zangu.
Natanguliza shukrani.