Nawatakia Eid Al Adh'ha njema

Dkt. Gwajima D

Minister
Joined
Nov 28, 2015
Posts
966
Reaction score
6,019

Wapendwa wote salaam,

Mwenyezi Mungu awe nasi sote kwenye Maadhimisho haya ya EID AL ADH'HA, 2024.

Naomba tukumbuke kuwalinda watoto wetu wawe salama pamoja na makundi yote yenye mahitaji maalum wakati wote wa kufurahia Sikukuu hii kubwa, In Sha Allah, Amina,

Heri ya Sikukuu kwetu sote.... 🌹
 
Asante sana mheshimiwa iwe heri kwako pia na familia yako.
 
Inshallah! Inshallah!
Sasa hawa ndugu zetu wakisha kula Biryani na nyama hua wanaenda matembezini hasa hao wa huko Pwani na Daslam hua wanaenda beaches mbali mbali huko wawe makini na watoto zao maana kwa ule msongamano kuna Watu hua wanawapoteza watoto zao kwa uzembe au bahati mbaya,
Sasa nawapa onyo wazazi humu kuweni seriously mnavyokuja huku
Coco beach,Bahari beach,Ununio huko kigamboni na maeneo mengine yenye msongamano mkubwa,
Lindeni watoto zenu kuna mambo ya hovyo hua yanaendelea sababu penye wengi pana mengi!

Nitawakieni Eid njema japo hata jirani yangu bwana Ostadhi Khamisi kavunga kunipa mualiko sijui ndio vile navyompiga nyundo katika Moja na mbili za kijiwe cha kahawa anapanic na kuniona Kafir la Kigalatia anyway
Sijui sikukuu njema!
😁😁
 
Mheshimiwa kazi za udalali Hadi sahv bila bila hakuna Dili. Hebu sambaza Upendo na huku mkuu namimi nifurahie na familia
 
Na kwako pia mheshimiwa.

Karibu hapa Kinondoni tule sikukuu. chair fire kavu itakuwepo.
 
Nilichokiona leo si kawaida. Nyama imekuwa nyama, kidogo watoane roho.
Waturuki analeta ngombe (wananunuliwa hapa) kwa ajili ya kuchinja na kugawa kwa waumini. Sasa management yake italeta kuuana siku za usoni kama hapatakuwa na utaratibu madhubuti. Nimeona leo!

Id Njema
 
Maisha magumu, hapo leo hadi wakristu wanapanga foleni
 
hujambo evelyn salt. Muda mrefu hatujawasiliana hapa, uliasi JF naona
Sijambo, nipo ndugu yangu we upo bize siasani majukwaa mengine hautembelei.

Vipi lakini nyama umepata, au bila bila 😹
 
Back
Top Bottom