GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Kila anayehojiwa na Mtangazaji ' Critical ' na ninayempenda na kumkubali kabisa Siza wa Cloudstv 360 on Saturday wakiwa ' mubashara ' kabisa kutokea Mlimani City kuwa aelezee Historia ya Mafanikio yake hadi leo wamefanikiwa Kimaisha unaona tu wanazunguka zunguka huku mengi tukifichwa.
Nikilitumia sana ' jicho ' langu Kali la ' Kisaikolojia ' na kwa jinsi ninavyowakodolea hawa Wanawake wakiwa ' mubashara ' wanatiririka na wanaserereka naona Shuhuda zao za Kimafanikio hayo waliyonayo zimejaa ' Unafiki ' mtupu hasa kwa wawili mmoja wapo akiwa anapatikana sana Millenium Tower Kijitonyama na mwingine akiwa mara kwa mara humkosi katika Vipindi vyake Channel Ten ambao ' Channels ' zao za hayo mafanikio yao zina mkono wa ' Kimahaba ' wa waliokuwa na Mamlaka yao / wenye Nyadhifa zao hapa Tanzania.
Wito tu Kwenu ambao huwa mnapenda ' Kutudanganya ' kuhusu mlivyopata hayo mafanikio yenu itapendeza sana na hata kutushawishi zaidi kama siyo kutufundisha endapo mtakuwa mnatupa zile Shuhuda zenu halisi hata kama zinatisha au kutia aibu kuliko kudhani kuwa huu uwongo wenu hatutaugundua haraka.
Ngoja niendelee kuwaangalia na nizidi Kudanganyika. Kazi ipo hakyanani!
Nawasilisha.

Wengi wao ni watu wa kamba sana
Msome huyu
"Wasichana au wakina mama tunaweza kununua madira ya elfu 13,000 au Lipstick ya elfu 3,000 lakini tukashindwa kununua unga wa maandazi wa elfu 10,000, wasichana wengi wanaonea aibu biashara zao wakihofoa watachukuliwa na jamiii, Mimi mpaka kufika hapa nilianzia na mtaji wa elfu 20,000 tu lakini kwasasa nimekuwa chanzo cha ajira nyingi za watu" Selina Letara [HASHTAG]#MalkiaWaNguvu[/HASHTAG] wa mwaka jana ambaye ni Mmiliki wa kampuni ya uzalishaji na usambazaji wa Hc Pads Tanzania
mwingine huyu hapa anaseama
"Mimi nilianza na mtaji wa laki moja (100,000) ambayo hiyo ukijumlisha na nauli ya kwenda na kurudi kariakoo ambapo nilikuwa nauza nguo za ndani kwa wanafunzi wenzangu chuoni, lakini kwasasa nina duka la nguo za kiume (Nguo za dukani) na Duka la nguo za kike (Nguo za Mtumba), Nauza kisamvu kwenye supermarkets, Popcorns na Spaghetti (Tambi)" Latifa Mohamed
mwingine huyu hapa
Bado kuna watu wengi ambao wanasoma Udaktari lakini mawazo yao yapo kwenye kuajiriwa wakimaliza masomo yao badala ya kuwaza ni kitu gani inabidi akifanya ili kusaidia jamii yake kwa kutumia elimu yake, Kuna watu wengi ambao ukiwapelekea mawazo yako wao wanayabeba na kufanyika kazi wao na hii isiwakatishe tamaa kwani wewe ndiyo unajua lengo la wazo lako ambalo ungetamani ulifanye na ulikuwa unalitazama kwa ukubwa ule" Juliana Busasu [HASHTAG]#MalkiaWaNguvu[/HASHTAG] 2017 ambaye ni mwanafunzi wa Udaktari mwaka wa tano na ni Mkurugenzi wa
Tanzania Health and Medical Education Foundation (TAHMEF)
mwingine huyu hapa
Mimi wakati nataka kuanza biashara yangu ya [HASHTAG]#Manjano[/HASHTAG] watu wengi walinikatisha tamaa lakini kwasababu nilijua nataka nini sikukubali kukatisha wazo langu, hata wakati nilipotaka kufungua Chuo cha urembo nilimfata 'Mental wangu' (Mshauri) na kumueleza wazo langu na alinishauri nifunge baadhi ya maduka yangu japo ilinitisha lakini nilifunga ili niweze kufungua chuo na kweli kwasasa nina chuo cha urembo na biashara zangu zinaenda vizuri" Shekha Nasser