Nawatazama hawa Wanawake waliofanikiwa kimaisha Clouds Tv, ila Shuhuda zao za Mafanikio hazinishawishi

Nawatazama hawa Wanawake waliofanikiwa kimaisha Clouds Tv, ila Shuhuda zao za Mafanikio hazinishawishi

Mimi kuna mdada mmoja tumesoma nae kuna siku nilisikia anahojiwa akaleta story yake alivyoanza biashara nikacheka sana...tunaomfahamu tunajua mtaji kapewa na mchepuko wake ambae ni mmoja wa viongozi wa TPSF
Wanawake wengi ni waongo....wakisha achana na watu wao utasikia biashara yangu nilianza na mtaji wa tsh 3500/=
 
Waongo waongo waongo kuna mmoja Dada wa mjini alikua punda haswaa sa hivi akikusimulia utaliaa
Kuna mmoja mwingine ni mtangazaji ana wadanganya kila leo watu kuwa kwa mshahara mdogo alio nao analima vitunguu uko morogoro tena heka kumi kumbe shamba ni la jamaa yake ana fanya kazi bank tena analima kwa mkopo...
Watanzania wengi tuna hulka ya uongo si wanawake tuu,,,yani tunapenda sana kuwafariji watu oooh mimi nilianza kuuza hapa kahawa na sasa nimejenga hotel mbili.....yani mtu kusema nimechukua mkopo anaona ni aibu....
Watanzania ni mabingwa wa uongo....kila aliyefanikiwa utasikia mtaji wake haukuzidi laki moja
 
kanisani pia nakukatalia, huwa nastaajabu shuhuda za kwa mzee wa upaka, mwanamke anasema, "mwaka jana sikua na gari, baada ya kuanza kuja kanisani na kupata upako, sa ivi nina gari langu, lipo hapo nje"
Sasa unajiuliza kwanini huwa hawaelezee walifanyaje, hupati jibu.
Watanzania uongo uko kwenye damu....
 
Hivi ni Mentor au ni Mental???
Usahihi ni mentor lakini kwa tafsiri sahihi aliyotaka kusema bora angetumia kiswahili tu angeeleweka vyema kulikokachumbali halafu inawekwa sukari badala ya chumvi.
 
Back
Top Bottom