Mikopo Consultant
JF-Expert Member
- Oct 28, 2024
- 529
- 1,150
Huo ni mchezo maarufu sana unaojulikana kama Chess. Ni mchezo ambao ukizoea kuucheza sana, utaitengeneza akili yako kuwa mtu wa mikakati zaidi kwa wakati wote.
Kuna mafunzo mengi sana unaweza kujifunza kwenye mchezo wa chess, mojawapo ikiwa ni 'sacrifice' and 'trade off'; ili ushinde mchezo kuna mda itakubidi upoteze kete zako hata muda mngine zile za umuhimu kabisa, ili uweze kushinda mpambano.
Maana yake, kwa mchezaji anayejua ushindi wake utapatikana vipi, huwezi kuhofia 'trade off' and 'sacrifices'; ki uhalisia wa mambo, zinaweza kuwa in the form of wasting resources, kuharibu mahusiano ya kidiplomasia, etc etc
Kuna taifa ni wataalamu sana wa kuucheza huu mchezo wa Chess, nao sio wengine bali ni warusi; cha kushangaza ni taifa ambalo limeshinda vita vingi sana kwa miaka 200 iliyopita, na hii ni kwasababu warusi walishajua huwezi kushinda vita vikubwa bila kupoteza kwanza, na hapo ndipo iliyo mstari wa ushindi. Je, utaogopa urudi nyuma na kuacha vita au utaongeza nguvu ya kupambana ili ushinde vita?
Mimi sio mwanajeshi, ila ushauri wangu waweza kuwa waki puuzi, lakini nawashauri JWTZ kwamba, 'wakiua mwanajeshi mmoja ongeza battallion moja kwenye mstari wa mapambano'