Nawaza mateso waliopata watu kwa kutongozana kabla simu hazijaja

Nawaza mateso waliopata watu kwa kutongozana kabla simu hazijaja

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
16,295
Reaction score
33,994
Kipindi cha nyuma 1985-2000 simu zilikuwa nadra sana,

Lakin pamoja na uchache wa simu, watu walitia maneno mpaka wenza wao wakawaelewa,

Kwa wale wa juzi juzi mmerahisishiwa kazi sana,

Mtu kipindi hicho anakaa Tabata anamfuatilia msichana wa makumbusho bila hata simu, inabidi apande gari akashuke mwenge atembee mpaka bamaga kwakuwa anahisi msichana yule atapita maeneo yale kama siku alivyomuona akipita nyuma,

Na anamkosa, anaamua kurudi home, kesho yake anatia kambi tena lakin hafanikiwi, hii ilileta hamasa kwamba hata akimpata maneno ni hapo hapo,

Watu wameng'atwa sana na Mbu wakiwasubiri kina Mwajuma wapite njia fulani kisa wameona anapita asubuhi,

Watu wameshinda mtoni wakiwasubiri akina hilda ili wapate nafasi ya kutema yao

Watu wameteseka mno,

Siku hizi wanaume hata kutongoza imekuwa shida neno linalotangulia ni NAOMBA NAMBA YAKE HIYO DADA,

hawana uwezo tena wa kumface mwana mke kumtemea cheche live,

Siku hizi wamerahisishiwa sana , mwanamke akikunyima namba ya simu unamuomba basi anayotumia tigo pesa haha anaachia mara moja
 
Na anamkosa, anaamua kurudi home, kesho yake anatia kambi tena lakin hafanikiwi, hii ilileta hamasa kwamba hata akimpata maneno ni hapo hapo,
,
Eee mkuu....mi nakumbuka kuna mmoja nilikuwaga kila Jumapili naenda kumsubiri njia anayopita anavotoka kanisani
 
Tuliteseka kwel Mariam wang alinifanya ninga’twe na mbu vichochoron,ooh we acha tyu uvumilivu ndo kila kitu...


Sent using Jamii Forums mobile app
alafu wengi walisubiriwa wakitoka ama mtoni, dukani au jumapili kutembea maana mara nyingi walikuwa wana majukumu mengi nyumbani au wana kuwa shuleni
 
Kule vijijini tulikuwa tunaandika barua tunajificha kichakani tukisubiri binti anapokwenda au kutoka kuteka maji kisimani tunairusha barua njiani uso wa bahasha kwenye anuani yake ukiwa juu, akifika na kuiona anaichukua, ngoma ilikuwa kufuatilia majibu ya hiyo barua
 
alafu wengi walisubiriwa wakitoka ama mtoni, dukani au jumapili kutembea maana mara nyingi walikuwa wana majukumu mengi nyumbani au wana kuwa shuleni


Shuleni tulikuwa tunaandika barua tunaiweka katikati ya daftari ya binti, wengi walipata misukosuko kwani baadhi ya mabinti waliozembea barua zilinaswa na walimu na wengine zilidondoka njiani bila wao kujua
 
Back
Top Bottom