Nawaza tu, kama mwenye haki ya matangazo angekua DSTV!

Southern Highland

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
14,938
Reaction score
25,405
Tunachukuliana poa kwakua mmiliki wa haki ya matangazo ni MTanzania mwenzetu. Lakini proffessionally, financially hata socially anaenda kulilia chooni kwa hasara anayoingia na anafanya hivyo asiwakere waliompa tender.

Pole sana Azam, nia yako ni njema ila waliokupa kazi hawathamini jasho lako.
 
Sasa yeye Azam ana hasara Gani wakati ameshauza vifurushi Tena kwa bei kubwa kwa watanzania wenzake. Waliopata hasara hapo ni wananchi walionunua vifurushi na wengine kusafiri kutoka mbali kuja kuona mechi hiyo.
 
Sasa yeye Azam ana hasara Gani wakati ameshauza vifurushi Tena kwa bei kubwa kwa watanzania wenzake. Waliopata hasara hapo ni wananchi walionunua vifurushi na wengine kusafiri kutoka mbali kuja kuona mechi hiyo.
Wewe unadhani biashara inaishia tu kwenye mauzo ya ving'amuzi? Kuna watu wameweka matangazo ya kabla, wakati na baada ya mechi, kuna mauzo ya matangazo youtube. Lakini hata yeye kujiuza kwa kuonyesha ligi kuu ya TZ ila kwa kinachotokea inashusha brand yake pia.
 
Azam wameshapata pesa ya vingamuzi
 
Azam kama mrusha matangazo hajapata hasara, wananchi waliolipia vifurushi na makampuni yaliyopeleka matangazo yao ili yarushwe wakati wa mechi ndio wamepata hasara na pesa hairudishwi.
Mechi kuahirishwa haishushi brand ya Azam labla kama wao ndo mana walishindwa kurusha na sio vinginevyo mana sio mara ya kwanza kuonyesha derby.

Tangazo moja pale wakati wa mechi ya derby n 2M+
 
Low IQ mbumbumbu fc
 
Mtoa mada, wenye hasara ni waliokata tiketi za mechi na walipia vingamuzi
 
Mara nyingi anaepata hasara ni mlaji wa mwisho, ukiongeza kodi au gharama yoyote kwenye bidhaa yeye mfanya biashara atahakikisha anakuongezea wewe mlaji gharama husika.
 
Bodi ya Ligi inapaswa kuburuzwa mahakamani kwa kuchukua maamuzi ya kijinga bila kufikiria, tangu lini mechi ikaahirishwa kisa timu kushindwa kupasha uwanjani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…