Mimi sio mshabiki wa Yanga, lakini napenda kusema ukweli. Yanga ya sasa hivi ni bora kuliko timu yoyote ya Tanzania. Hata Simba kwa sasa hatuna viwango vya ubora wa Yanga. Sababu za msingi ni hizi:
1. Kwa aina ya kocha waliyenaye sasa Yanga, uwezo wake (kumsoma adui ndani ya mechi na kuibadili timu kucheza ndani ya mechi), hicho ndio kiwango cha kucheza mechi za kimataifa.
2. Ubora wa wachezaji kama Fiston Mayele katika kufunga, Aziz Ki katika kugawa mipira na Feitoto katika kusukuma timu kushambulia, Yanga wanaweza kuifunga timu yoyote hapa Afrika. Narudia tena, Yanga ya sasa wanaweza kuifunga timu yoyote hapa Afrika.
Kiwango cha uchezaji wa kiushindani kinachoonyeshwa sasa na Yanga, bila ushabiki ninapenda kusema wazi, ni kiwango tunachokiona kwa timu za hatua ya robo fainali. Sio mtoano wala makundi kunakoweza kumsimamisha Yanga, labda hatua ya robo fainali. Al hilal sio timu tishio kwa Yanga, sijaona kitu kipya au kitu cha ajabu.