Naweza fanya biashara gani kwa mtaji wa 15m?

Naweza fanya biashara gani kwa mtaji wa 15m?

Lete mil.6 tufanye biashara ya dhahabu tutakua tunazungusha faida ya mil 1.5 kila week lakini kwa kuwa mie ntakua nashinda site itabidi niwe nalamba hizo laki tano then wewe unakula mil.1 hiyo ni hesabu ya week.....
Nimependa hii... nitumie namba yako mkuu
 
Kuna biashara ya kuku ambayo inaendelea kwa mjini mwanza ambapo wale jamaa wa *kuku poa* wanakupa vifaranga na chakula cha kuku .yaan mtaji wako wewe inakuwa ni mabanda tu.ila sharti yaweze kuweka zaidi ya kuku 5000, wanapita kukagua mara mbili kwa wik then ikiisha wiki tano wanakuja kuchukua kuku wao na kukulipa 1000 kwa kila kuku,
So kwa pesa uliyonayo unaweza tenga fungu ata ukaweka mabanda ya kubeba kuku 10000. Na baada ya wik tano ukawa na uhakika wa 10000*1000=10,000,000/=
Kwa maelezo zaid fika ofisi za kuku poa pale mwanza
Hii pia nzuri
 
Fungua pharmacy mimi nmesomea mambo hayo nitakusaidia kuoperate na faida yake n kubwa na utaiona. Mawasiliano 0658047048
 
Tengeneza kipato cha Ziada Kwa kupata kitabu maalumu kitakacho kufanya ujue kutengeneza bidhaa mbali mbali muhimu za viwamdani nyumbani kwako na uweze kujiajiri. Kitabu hicho utakipata Kwa bei ya TSh.5,000 tu! Katika email au whatsup yako. Nipigie au whatsup 0762208190 AU 0718978295. Utachagua unacho taka kujiajiri kitaalam kupitia kitabu hicho
 
Lete mil.6 tufanye biashara ya dhahabu tutakua tunazungusha faida ya mil 1.5 kila week lakini kwa kuwa mie ntakua nashinda site itabidi niwe nalamba hizo laki tano then wewe unakula mil.1 hiyo ni hesabu ya week.....
Biashara nzur sana lakin hauhitaji kuiweka kitega uchumi cha miaka yako yote....ni biashara nzur kupatia mtaji,na kupanulia akil ya kuwa na uwekezaj mwengne!! [emoji106] ...
 
Biashara nzur sana lakin hauhitaji kuiweka kitega uchumi cha miaka yako yote....ni biashara nzur kupatia mtaji,na kupanulia akil ya kuwa na uwekezaj mwengne!! [emoji106] ...
Always husitegemee biashara moja.....ukifanya business hii huwa haijifichi utaona fursa zingine
 
Duh kwel binadam tupo tofauti,,15ml hujui ufanye nn? Nipe hyo hela kila mwezi nikulipe 1.6 ml na hela yako IPO baada ya mwaka makupa hela yako yte...
 
Electronic money transfer pamoja na vocha za jumla na si rejereja ,akipata site nzuri mwaka mmoja anaendesha Audi q6 ,hizo gesi sijui kusajili laini uchawi tu kwa milion 15.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Vitu vingine vina mutual benefit. You win, I win. Kqtika mazingira kama haya ni ngumu kumwaga kila kitu. Ila ukitaka nikumwagie wewe nifate PM. Kuwa na amani
Kwa iyo unataka kwenye iyo m15 nawe ufaidike? sa si atabidi aje na thredi nyingine ya m10?!!
 
Kuna MwanaJF alitoa ushauri, ulionukuliwa hapa chini. Nami nasisitiza kuwa yawezekana na faida yake ni kubwa, baada ya miezi sita (6).

Ikumbukwe kuwa ujenzi wa viwanda, hasa vya kuonfeza thamani ya mazao ghafi, ni fursa kubwa ya kujihusisha na uzalishaji mazao ya biashara na chakula.

Kwa mfano, viwanda vya kusindika nyama ya ng'ombe, kitoweo kikubwa kwa wakazi wa mijini, kunatoa fursa ya kukua kwa ufugaji wa kuku, maana nyama ya kusindikwa ni kwa soko la nje, na bei ya nyama ghafi ikaongezeja bei, hivyo kuruhusu kukua kwa soko la nyama ya kuku.

Isitoshe, mfugaji wa kuku akiweza kuweka na bwawa la samaki, anakamilisha mnyororo wa uzalishaji. Kuku watampatia mbolea kwa ajili ya kurutubisha bwawa la samaki. Maji ya bwawa yatampa maji ya kumwagilia bustani. Mazao yatokanayo na ufugaji wa kuku, samaki na bustani, hakika ni pato tosha la kuondokana na umaskini.

TAHADHALI NI LAZIMA UTUMIE WATAALAMU KWA SHUGHULI HIZO ZA UZALISHAJI.

Nukuu:

"MCHANGANUO WA TSHS 300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MRADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.

Hapa utahitaji kuku 11 tu wakubwa wanaotaga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu (300) au na zaidi kama unataka.

Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.Tafuta sehemu ya uhakika na nunua kuku wenye matunzo na kinga ili wasipatwe na magonjwa na wenye afya nzuri.

Unaponunua kuku wakubwa kwanza unapowafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae.

Usinunue kuku kabla hujaandaa banda la kutosha kulingana na idadi ya kuku na kwa ajili ya badae kwa kuwa mradi utaongezeka kadri siku zinavyoenda na Chakula.

Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia.

Mchanganuo Wa 69500 ni:-
1) Pumba gunia 1. Shs.20000 gunia la pumba lina kilo 70.<
2) Paraza (mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku) kilo 25 = 700x25 =17500.
3) Mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10500
3) Layer's concetrate, Kilo 25 kifuko. = 21500.

Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.

Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi - Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku: Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300. Hivyo tutaweza kuona Chakula hicho kitakupeleka zaidi ya siku 100 au zaidi ya miezi mitatu.

Kwa laki 3 utabakiza 170000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU, na mchanganuo wake ni: Kwa kila kuku mzuri ambaye hajazeeka anayetaga utampata kwa shilingi 15000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20000 - Majike 10 x15000= 150000 jumla 170000.

Itakuwa imebaki shs. 60500 kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi 20.

Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati wakutaga

Kuku wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga nyunyizia Dawa ya utitiri.

Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani urefu kwenda juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi 4. Tumia materio yaliyo karibu nawe kama mirunda, mabanzi, Mabati reject au yaliyochakaa chicken wire au wire mesh, fito mbao 2x2 au 4x2 n.k. Kama ni sehemu za mjini litakugharimu kama Tsh 50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000 hadi 35,000.

Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata kuku wengi hadi utakao wataka. Hapa itabidi ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi 10000. Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240. Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye Mashine yakutotolea (incubator). Hivyo kwa mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa Vifaranga 200.

Hivyo baada ya mwezi nakushauri usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni wengi sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua Chakula cha kuku cha kutupeleka miezi mitatu basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza kwaajili ya kupata hela ya Chakula cha Vifaranga watakao toka hao zaidi ya 200. Hivyo mradi huu utakuwa unajiendesha wenyewe. Kwa maana kwamba kama kuku 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni wazi kuku hao wanakuingizia 120,000 kwa mwezi ambaya sasa hela Hii itatumika kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga ambapo Mayai ya mwezi tu yataweza kununua Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi pamoja na chanjo na Dawa zote.

Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na Chakula cha kuku wakubwa ndo kitakuwa kinaishia, hivyo utachanganya Chakula cha aina moja tu, kwa kuwa wale Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha kula Chakula chochote.

Kumbuka kujibana ili kuongeza ukubwa wa banda"
Ulishawahi fikiria soko?
 
Nakushauri fanya biashara ya mazao(chakula) hutajutia.

ANGALIZO:
>Tafuta unae mwamini akufundishe hii biashara.

>Usitake (usiwe na tamaa au haraka ya )faida kubwa kipindi unaanza biashara mpya!

>Usitumie akiba yako yote kufanya biashara mpya( siku moja utapiga ukunga )

>Usilete nyodo/kuwa dharau ulio wakuta kwenye hiyo biashara mpya!
atakama umewazidi mtaji au umri.

>Pamoja unabidi uwe kalibu na wenyeji na kusihi sana kua makini nao na katika swala la pesa usimwamini mtu!

>Kwenye biashara kuna hasara,kila penye faida kuna hasara kama wewe ni risk avoider ludisha pesa za watu ujasiliamali huta uweza!
 
Yaani hilo dau ulilolitaja limewatoa watu udenda badala ya kutoa ushauri wamebaki wanaweweseka, yaani karibu wote walio changia wanaitaka hiyo mil 15 yako so take care, wengine wanataka uwape kazi wengine uende pm wakupige sound, wengine wanataka ununue vitabu vyao vya ujasiriamali, wengine wanakupa links za thread zao za kutafuta hela dah
 
Back
Top Bottom