Naweza kuipata wapi dawa ya kunguni?

Nenda Kkoo sokoni floor ya juu kule kuna madawa yana uzwa yakuangamiza hao viumbe wakorofi
Kwa nini usimwambie tu kwamba aende kwenye duka linalouza madawa ya kilimo na mifugo kuliko kumwambia aende Kariakoo? Kama yupo mkoani na kama huko mkoani hakuna soko la Kariakoo afunge safari kwenda mji wenye soko la Kariakoo? BTW dawa nzuri kabisa a kuua kunguni ni Diazinon.
 
Tatizo tunakosea jins ya kutumia dawa.. mimi walinisumbua sana siku moja nikaenda kkoo kwenye haya maduka ya dawa za mifugo nikakuta muuzaji ni mama wa makamo nikamueleza tatizo langu akaniambia mwanangu ukitaka kuwmaliza hawa wadudu ni lazima upige dawa mara 4 au 5 kila baada ya siku 7 unapiga.. akanieleza sbb za kupiga dawa baada ya siku 7 ni kwamba unapopiga dawa unakua umeua kunguni as kunguni lkn mayai yanabaki, na mayai ya kunguni yanajiengua baada ya siku 7 wanakua tayar wadudu hivyo ukipiga tena unakua umeua wale walioenguliwa, baada ya siku saba yataenguliwa tena mengine hivyo ukipiga dawa unakua umeua kizaz kingine... so ukifanya hivyo round 4 au 5 utakua umetekeza kizaz chote... nilifanya hivyo had leo kwangu kungun historia... naatach dawa niliotumia
 
Huyo mama simtaalamu Sumu kama sumu ikilikuta yai inaliharibu hapohapo hata kama limetotolewa leo
 
Tumia LAVA aliyoweka jamaa juu hapo kuna ya kila kizibo kimoja na nusu unachanganya Lita moja ya maji mwagia kila Arch kitandani na chumbani kote sumu yake kali inauwa mpaka mayai mbu utaona wamedondoka chini
 
Pole sn mzee,

Ilishanitokeaga miaka ya nyuma nyuma kidogo, walisumbua sana nikakosa raha,, ila nilienda kariakoo soko kuu kwenye maduka ya madawa ya wadudu kuna dawa moja ya maji inaitwa Vita Shield ni balaa hio

Watakupa maelekezo namna ya kuitumia
Unapulizia angle zote za kitanda, chaga, kila pembe ya mkunjo wa godoro, madirishani kwa kifupi angle zote za chumba,,, hivo vijamaa vitateketea vyote na hutoviona tena asilani
 
kama unaona hali ni tete na huna njia ya haraka ,chukua mafuta ya taa ya kutosha,japo ndani patageuka shell usijali.

mimina kwenye kila uchochoro unaoujua kwenye kitanda,godoro,kabati,sofa,dressing table hata ukutani.kisha kwenye mikunjo ya godoro fanya kama unamimina hivi.

baada ya mwezi hutaona kiumbe wa kuitwa gofu.
 
Huyo mama simtaalamu Sumu kama sumu ikilikuta yai inaliharibu hapohapo hata kama limetotolewa leo

[emoji23][emoji23][emoji23] mi sijui bana ila nilifata utaalam wake nikafanikiwa[emoji120][emoji120]
 
Uliwapata kwenye shule ya bweni au kwenye daladala?? Tehtehteh
 
Spirit ile ya kijani imeonyesha ufanisi mkubwa
 
YES iyo dawa uliyo itaja kali sana. Big up chiwf kwa kumuokoa mjumbe maana angekimbia chumba huyo
 
Nashukurun wadau kwa michango yenu j3 naenda nunua dawa zote leo ntalala kwenye koch
 
Nenda pale kariakoo sokoni juu, au fika pale Ilala Amana hospitali kuna maduka ya pembejeo na madawa ya mifugo, utapewa dawa na hawatakaa kurudi kabisa huna haja ya kuchemsha maji wala nini

mimi walinisumbua nikatafuta hiyo dawa, baada ya kuchanganya tu nikanyunyuzia kwenye magodoro na chaga za kitanda nikaweka juani, afu nguo zote nikafua, na baadhi ya dawa nikadekia kabisa

ilibaki stori mpaka kesho no kunguni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…