Mzee mimi ni muhanga wa Hao wadudu kwa miaka karibu Mitatu! ni wadudu wa ajabu sana, Nilitumia Dawa zote za Kunguni bila mafanikio. Ila nilikuja kuwaangamiza kwa njia rahisi sana.
Kwanza unatakiwa kujua maeneo wanamojificha zaidi katika chumba.
Sehemu yao No 1 ni kwenye Foronya.
Sehemu yao ya 2 ni kwenye Kitanda hasa kikiwa cha mbao, Hujificha kwenye pembe na maungio ya kitanda. huzaliana humo kwa raha mustarehe wakipata food ya damu kila siku na kurudi kwenye makao yao salama ya kitanda.
Sehemu yao 3 ni kwenye sofa, hasa kama una sofa la kitambaa.
Sehemu yao ya 4 ni kwenye nguo unazazovaa.
TIBA YA UHAKIKA.
Kwa upande wangu Naamini Tiba kiboko ya kunguni ni MAJI YA MOTO
Hatua.
1. Chemsha maji kwenye sufuria yachemke na kutokota.
2. Weka maji hao kwenye Chombo
3.Tenganisha Dogoro na Kitanda.
Kama unaweza Fungua Kitanda kabisa Uweke chini
4.Mwagia Maji yaliyotoka kutokota kitanda na chaga vyote, Vilowe kwa maji ya moto hasa, Chukua Foronya Hilo Loweka kwenye maji ya Moto hasa Ulifue. Godolo litoe foronya na kama Godoro lina tundu lolote Hakikisha unamwagia hapo maji ya moto.
Ukimaliza Operation hiyo kwenye kitanda siku hiyo hiyo hakikisha unatoa nguo zako zote na kuzifua kwa maji ya moto.
Kama una sofa la kitambaa hakikisha unamwagia maji ya moto kwenye pembe zote, hapo uwe mwangalifu sana maana wale jamaa ni wahuni wanaweza kula kona.
Ukimaliza kumwagia maji ya moto kitanda, nguo, Godoro na sofa. Hakikisha mwisho na nguo ulizozivaa hapo Zinafuliwa kwa maji ya moto. Zoezi hilo lifanye mara mbili ndani ya mwezi mmoja.
Hao kunguni wote watapotea na katu hutawasikia ndani kwako.
Bila ya kufanya hivyo mzee jiandae kuishi nao hao jamaa maana huwa hawaishi. Unaweza kuwapoteza kwa mwezi mmoja baadae unakuta wameshafurika tena ndani.