Naweza kukopa pesa benki dhamana ikiwa pesa zilizokuwepo kwenye account yangu?

Naweza kukopa pesa benki dhamana ikiwa pesa zilizokuwepo kwenye account yangu?

TEAM 666

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2017
Posts
4,399
Reaction score
8,594
Habari wakuu naweza kupata mkopo bank dhamana ikiwa pesa zilizokuwepo kwenye account yangu?

Mfano, kwenye account Nina million 40 nataka kununua Guta nifanyie biashara hivyo sitaki kushusha salio la balance yangu iliyokuwepo kwenye account hivyo Sasa nataka kukopa milion 4. Je inawezekana?
 
Inawezekana. Kama unaziweka fixed account. Pili kwanini ukope si bora upunguze kwenye akiba yako na uweke nadhiri ya kuzirudisha.

But yote ni maamuzi tu.
Economy yake ni very poor! Anasema ^sitaki kushusha salio la balance yangu,^ all the while anasahau akilipa mkopo na riba husika, anakuwa ameshusha balance mara nne! Ushamba huu wa mjini umerudije tena Tanzania kwa kasi hivi?

BTW: Why would anyone in their right mind even venture to keep such relatively lavish sum of money dormant?

Au anataka tujue kwamba sasa anamiliki hizo milioni alizolipwa posho pale hazina?
 
Inawezekana kukopa dhamana ikiwa ni hiyo saving yako. Lakini fanya utafiti kwanza, hiyo 40m ikikaa tu banki kama saving inakuingizia faida kiasi gani kwa mwaka?

Kama una wazo la kuwekeza basi hiyo 4m itoe kwenye saving utengeneze portfolio mpya ya investment. Balance yako itakuwa 36m saving + 4m investment ya guta.

Hiyo 36m au 30m wekeza kwenye hatifungani za Serikali za muda mrefu. Huko kwa savings acha kitu kama 6m tu.
 
Economy yake ni very poor! Anasema ^sitaki kushusha salio la balance yangu,^ all the while anasahau akilipa mkopo na riba husika, anakuwa ameshusha balance mara nne! Ushamba huu wa mjini umerudije tena Tanzania kwa kasi hivi?
My tagert

Ile pesa nitakayochukua ndio nitakayoifanya baishara na ikarudisha mkopo wa bank huku salio langu la hakiba likabaki palepale
 
Habari wakuu naweza kupata mkopo bank dhamana ikiwa pesa zilizokuwepo kwenye account yangu

Mfano kwenye account Nina million 40 nataka kununua Guta nifanyie biashara hivyo sitaki kushusha salio la balance yangu iliyokuwepo kwenye account hivyo Sasa nataka kukopa milion 4. Je inawezekana?
Inawezekana
 
Embu fafanua vizuri hapo mkuu
Ok... well kwa mfano salio lako ni 40millions. Unataka mkopo bank. Unachokifanya unaomba kuweka kiasi cha pesa yako kwenye fixed account na utapewa faida yake kwa kila mwaka inategemea na bank zilizo nyingi hiwa wanatoa asilimia 8 mpaka 14 kwa mwaka. Maana yake ni kwamba pesa yoyote ukiiweka kwenye fixed akaunt utapewa faida yake kwa asilimia kila mwaka. Pia hiyo pesa uliyoweka unaweza ukaikopea na mkopo wake unapata ndani ya 72 hours ,na kiwango utakachopewa hakitazidi asilimia 90 ya pesa uliyoweka.

Pia utapewa special interest rate kwa sababu faida yako inaweza ikapunguzwa kwenye riba ya mkopo.
 
Inawezekana kukopa dhamana ikiwa ni hiyo saving yako. Lakini fanya utafiti kwanza, hiyo 40m ikikaa tu banki kama saving inakuingizia faida kiasi gani kwa mwaka?

Kama una wazo la kuwekeza basi hiyo 4m itoe kwenye saving utengeneze portfolio mpya ya investment. Balance yako itakuwa 36m saving + 4m investment ya guta.

Hiyo 36m au 30m wekeza kwenye hatifungani za Serikali za muda mrefu. Huko kwa savings acha kitu kama 6m tu.
Hapa kwenye hati fungani za serikari mkuu naomba unieleweshe.
 
My tagert

Ile pesa nitakayochukua ndio nitakayoifanya baishara na ikarudisha mkopo wa bank huku salio langu la hakiba likabaki palepale
Unashindwa kufanyia biashara 40 mil hadi ukaifiche benki? Umaskini unauvuta mwenyewe. Nakushauri umtafute financial advisor ukae naye, akupe ABCs za uzalishaji wa pesa.
 
Serikali huwa inakopa kila mwezi, hufanya hivyo kupitia matoleo ya hatifungani za miaka 2,5,7 10 n.k.

Kama una mkwanja kuanzia 1m umeweka tu kwenye saving stuka! Nenda tawi lolote la banki hizi NMB au CRDB ulizia utaratibu wa kununua hatifungani.

kama uko Dar, tafuta madalali wa soko la hisa...Orbit Security, Solomon Security n.k watembelee utapewa maujanja ya kutosha. Kila la kheri!.

CC: Mine eyes
 
Ngoja namie nifanye hivi. Ninunue hati fungani za 5m nione itakuaje after two years.
 
5m una uhakika wa faida kitu kama laki tano kwa mwaka inayolipwa katika awamu mbili kila baada ya miezi sita i.e 250,000 TSH X2/mwaka mara miaka miwili= 1000000+5000000 ~ 6000000 !.

Mlolongo
 
5m una uhakika wa faida kitu kama laki tano kwa mwaka inayolipwa katika awamu mbili kila baada ya miezi sita i.e 250,000 TSH X2/mwaka mara miaka miwili= 1000000+5000000 ~ 6000000 !.

Mlolongo
Vp kuhusu usalama wa pesa
 
Back
Top Bottom