Naweza kupata wapi vitabu original vya Torati, Zaburi na Injili ambavyo havijapotoshwa/kuchakachuliwa?

Sasa utajuaje hiki kimerudiwa sana na kuandikwa upya kama huna kitabu original cha kulinganisha??
Utaona vilivyopo vinatofautiana, kwa hiyo utajua hapa kuna shida ya kupata ukweli kama original
 
Vikusaidie nini?

Yaani hayo mangonjera na mahadithi yasiyo na kichwa wala miguu ndio yanasumbua akili yako hivyo?
Mkuu

Nafikiri haujaelewa swali, ungelielewa usingejibu hivyo.

Kwa msaada, muktadhanuko hivi; Waislamu hudai kwamba dini yao ni mwendelezo wa dini ya kiyahudi na kikristo zilizotangulia, na wanatumia manabii hao wa kale kuongeza ushawishi kwamba dini yao ni mwendelezo tu, sio dini Mpya.

Lakini, ukisoma maandiko ya dini hizi mbili, dini ya kiyahudi (Torati) na dini ya kikristo (Injili) unagundua kwamba uislamu ni dini tofauti kabisa, na hasa inatambulishwa kama dini inayopotosha mafundisho ya hizo dini mbili.

Hivyo, Waislamu hujitetea kwamba maandiko hayo ( Injili na Torati) zilizopo sasa, zimepotoshwa, sio nakala halisi za Injili na Torati halisi.

Ndipo swali linaulizwa, HIZO Torati na Injili halisi, nakala zake ni zipi? Maana huwezi kusema hii ni nakala batili bila kuwa na nakala halisi, itatupa shida kujua umejuaje ni batili wakati halisi hauna.
 
Mkuu

Wewe umejuaje kwamba hayo uliyoyasema yako kweli kwenye hivyo vitabu? Wewe mwenyewe umevisoma hivyo vitabu, ama umehadithiwa na mtu aliyehaditihiwa kwamba kuna mtu alimwadithia kuna mtu aliwahi kukisoma kwenye vitabu ambavyo hakuna mtu anaruhusiwa kuvisoma?

Halafu, kwa nini waendelee kukitumza kitabu ambacho kilichoandikwa hawataki watu wajue, si njia rahisi ni kukiteketeza hicho kitabu?
 
Utaona vilivyopo vinatofautiana, kwa hiyo utajua hapa kuna shida ya kupata ukweli kama original
Mkuu

Ikiwa vitabu viwili au zaidi vinatofautiana, na wewe hujui kipi ni sahihi, Kuna uwezekano wa angalau aina tatu
1. Kimoja kinasema ukweli, vingine vinadanganya
2. Vyote vinadanyanga
3. Vyote/baadhi viko sahihi, hujavielewa .

Huwezi kulazimisha uwezekano 2 kuwa ndiyo sahihi, bila kupata ukweli, lazima uwe na ukweli ndipo utatambua kwamba vyote vinadanyanga.

Kwa muktadha huo, huwezi kusema Injili na Torati tulizonazo kwa sasa sio sahihi, bila kutuonyesha nakala nyingine zinazoaminika ni sahihi na tofauti na hizi.
 
Ishu sio Qur'an, ishu Biblia ambayo mnasema ni injili, torati na Zaburi zimechangangwa

Anataka hivyo vitabu, ajiridhishe kweli vimechanganywa?

Quran haina shida kwa kuwa ishajitenga na hivyo vitabu.
 
Kwanza inabidi utambue uwezo wako kama mwanadamu ni mdogo mno hata ukijiona una akili sana.

Kichwa ambacho hata mke wako anakucheat, anakusingizia mtoto na unalea mtoto sio wako, kisha ndio unajifanya una akili sana za kupata uhalisia wa Mungu?

Hata rafiki yako anakunafikia hujui ila unajifanya unataka uhalisia na kufikiria nje ya box juu ya Mungu?

Anyway, kwa mtu mwenye akili Kuna alama na ishara kibao juu ya uwepo wa Mungu.

Mwili wako tu ukiutafakari ni ishara tosha
 
Umeongea ujinga sana, nature ya mwanadamu ni kulazimishwa kufuata taratibu.

Mwache mwanao awe huru, uone kama ataenda shuleni

Fungua ofisi yako kisha mwache mfanyakazi awe huru uone kama itafika mwaka bila kufirisika

That's nature ndio maana hata kwa watoto Kuna muda tunatumia nguvu
 
Hakuna hivi vitabu. Vilivyopo vimerudiwa sana na kuandikwa upya na wafuasi tofauti mpaka baadhi mambo muhimu aidha hayamo au yanapishana.
Una ushahidi ?

Unajua biblia Ina manuscript zaidi ya 58000

Tofaut na Quran ?
 
Mwanangu umendika pumba sana

Unadai kuna vitabu vinavyothibitisha kwamba Yesu si Mwana wa Mungu bali Mtume tu, na kwamba Muhammad ametabiriwa, lakini vitabu hivyo vimefichwa. Huo tayari ni uthibitisho wa kutokuwepo kwa hoja thabiti. Kama kweli vitabu hivyo vilikuwepo, kwa karne zaidi ya elfu moja, kwa mamilioni ya watu waliobadili dini na kwa watafiti wa kila aina, kwanini visiwahi kuvuja hata mara moja? Historia ya kanisa na maandiko iko wazi kwa yeyote anayetaka kujifunza, hata wasio wakristo wana ruhusa kuichunguza. Hakuna ushahidi wa maandiko ya kale yanayosema Muhammad atakuja baada ya Yesu.

Kuhusu mapadre kuuawa kwa kusema Muhammad ni mtume, hiyo ni propaganda inayotumika kwa waumini wasiofanya uchunguzi. Vatican ni taasisi ya kidini yenye rekodi za karne nyingi, na bado haijawahi kuonesha hata kurasa moja ya hiyo Injili unayosema iko “imefichwa” kwanini basi unataka tukubali jambo ambalo hata nyinyi hamna nalo mkononi? Hili sio suala la ubishi, ni la hoja na ushahidi. Aidha, tuna mamia ya nakala za kale za Biblia kabla ya Muhammad kuzaliwa – Dead Sea Scrolls ni mfano, hazimtaji kabisa Muhammad wala Injili kubadilika kama unavyodai.

Na pia jiulize, kama kweli Ukristo ni wa uongo na unategemea kufichwa kwa maandiko ili uendelee, iweje uendelee kuwa na waumini zaidi ya bilioni mbili hadi leo, katika mataifa huru ya kielimu na kisayansi? Huo si ushahidi kwamba watu wanajua ukweli, bali wanapima kwa akili na ushahidi.

Kama kweli kuna maandiko ya kale yanayothibitisha unachosema, tafadhali yaweke wazi, tuyaone. Kama hamna, basi hoja yako inabaki kuwa hadithi ya kutungwa isiyoweza kusimama mbele ya ukweli wa kihistoria na akiolojia. Sasa, ni kweli unajua hoja zako, au unarudia tu alichokuambia mwingine?

Je, umewahi kuona hata kurasa moja ya hiyo Injili ya “kweli” unayodai?
Kwa nini hata wanazuoni wa kiislamu wakubwa kama Al-Tabari na Al-Bukhari hawakuiandika hiyo Injili unayosema imefichwa?
Kama kweli Muhammad ametabiriwa, kwa nini hakuna hata moja ya maandiko ya kale ya Kiyahudi au Kikristo yanayomtaja wazi?
Ni nani hasa aliyeandika hiyo Injili ya kweli na ilipoteaje kutoka karne ya kwanza hadi sasa?
Je, Mungu ni mdhaifu kiasi kwamba hawezi kulinda neno lake lisipotee?
 
Waulize hao hao waliokwambia vimechakachuliwa, wakwambie zilipo nakala halisi.
 
DAI la kusema vimechakachuliwa ni la waislamu ili kuji defend

Maana Quran imejaa uongo mwingi ,
 
Vipo ndani yako
 
Hofu yako tu. Hakuna awezaye kupotosha maandiko matakatifu. Kwanza hadi sasa nakala za sehemu ya vitabu vya kale vinaendelea kugundulika na wanapolinganisha na vitabu vilivyopo hakuna tofauti. Wayahudi ni watu makini sana ktk kuhifadhi vitu vyenye thamani. Wameweza kuhifadhi lugha na utamaduni wao kwa zaidi ya miaka 2000. Biblia Agano la kale ni sehemu ya utamaduni wao. Haiwezekani kuchakachua.
 
Biography ya kwanza ya Mtume Muhammad iliandikwa miaka 200 baada ya yeye Kuwa ameshakufa, mtu aliyeandika anaitwa Al-Bukhari alitoka central asia kwenda Hejaz
 
Upo sahihi 100%

Kuna manuscript za kutosha za biblia ,na zote zipo sahihi kwa 99.99% na biblia hii ya sasa




 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…