Naweza kusoma tena Degree ili niipandishe GPA?

Naweza kusoma tena Degree ili niipandishe GPA?

Pu
Yaani usomee taaluma uliyonayo tena Kwa level hiyo hiyo ya shahada ya Kwanza?

Bila Shaka wewe ni wale wenye vyeti vingi vya o level na A level
Punguza ujuaji, toa ushauri kulingana na request yangu
 
Habari ndugu Wana JF,

Kwanza nimshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai.

Pili, nawaomba wazoefu na Mambo wanipe elimu/ufafanuzi juu ya wazo langu lifuatalo kuhusu masomo ya elimu ya juu!

Kabla sijaweka swali, niruhusuni nijisemee kwa kifupi;

Mimi ni mwajiriwa wa serikali kada ya ualimu, Nina shahada (BAEd) masomo ya Geography na Kiingereza.

Nilipata GPA 3.4, hivi karibuni nimezongwa na kiu ya kutafuta sifa za kufundisha vyuo viwe vya Kati au juu Ila kwa kuanzia tu na "tutor or tutorial assistant" kitu ambacho natambua GPA hairuhusu.

SWALI: Je, naruhusiwa kusoma upya bachelor degree of Arts with Education ili kujaribu kutafuta GPA stahiki?

Au Kuna namna yoyote ya kufanya ili kuwa na sifa linganifu? Au nikisoma masters degree moja kwa moja inatosha?

Kwa kumalizia, natamani Sana niondoke kwenye ajira iliyo chini ya TAMISEMI, hivyo iwavyo yeyote anayeweza kunipa guidelines au fursa au connection ya transfer kutoka niliko kwenda kwingineko ninakoweza kufit Nita appreciate Sana. Dm zinakaribishwa pia.

Asante sana kwa ushirikiano
USHAURI WANGU NI HUU
Tofautisha na uchague kati ya;

Unachokitaka Vs Kinachokufaa
 
Maswali machache ndugu mwalimu,
1. Unadhani utapewa ruhusa kwenda kusoma tena kwa kitu kile kile?

2. Kama ulishindwa pata jipiei nzuri kipindi cha mwanzo unahisi nini kimebadilika sasa hivi utaipata?
3. Ukitaka kuwa mwalimu chuo wale wajinga wanaangaliaga kuanzia jipiei ya bachelor kwahiyo usiwaamini sana wanaokushauri ukasome masters moja kwa moja
4. Haya mambo ni saikolojia tu mkuu, ukipata sehemu ingine nako utaboreka tu. Imejini kuna mtu saa hizi ana degree kama wewe ya ualimu au hata udokta ila saa hizi yupo mtaani na kashafanya intavyuu ya tamisemi mara kibao anakosa. Mshukuru Mungu kwa hapo ulipo alafu jiendeleze
Nashukuru kwa ushauri. Jibu la swali lako Ni kwamba najua sababu zilizonikosesha hiyo 3.5 and above na kuangukia 3.4
 
Dah hongera kwa kuwa na ajira lakini pia mkuu ni Ile ukasome masters au fani nyingine mkuu! Full stop

Brother kwenda kusoma degree Ile Ile Kwa umri ni kujitakia shida. Labda kama huna majukumu makubwa, huna watoto na una mda wa kuchezea hapo ukute your 30 and above?
 
Jf imekua ya hovyo dadeki, majitu yanatema nyongo tu na sio msaada wowote, ni kejeli, matusi na kukatisha tamaa.

Itafute masters kijana, tafuta pia taarifa toka taasisi husika na watu walio huko kama unawajua, hapa hamna majibu utakayo. Jamii forums has fallen.
 
Sijui hii inawezekana au lah , nashauri now si umesoma Bachelor of Arts in Education. Ukirudi unaenda kusoma Bachelor of Education in Special needs au Bachelor of Education in Early Childhood 🤣 hii mbinu inaweza ikakubeba mkuu !

Unapiga course ya Elimu ila kwenye kipengele tofaufi !
 
Chuo gani atapata nafasi kufundissha na GPA ya 3.4 ya bachelor degree!? Hapo ni kusoma tu bachelor nyingine kama ndoto ni kupata qualifications za kufundisha chuo. Unatakiwa uwe na GPA ya 3.5 kwa vyuo vya kati, na 3.8 kwa baadhi ya vyuo vikuu.
 
Ee baba nakuja mbele zako kuungama kwa kusoma uzi wa kijinga kiasi hiki. Amen
Mleta uzi ingekuwa unaenda kusomea kitu tofauti ningekuunga mkono ila wazo lako la kwenda kutafuta GPA kubwa ni la kipuuzi mno. Hapo ulipo kama ni mwanaume unatakiwa utazame kutengeneza hela zaidi ili kujiandaa na majukumu ya familia kama bado hauna. Tafuta hela jomba acha upumbavu.
 
Ndio maana nikaja kujiuliza kupata wazo jipya. Najua wazo vigezo Ni tight ndio najaribu kuwaza Kama naweza boresha mambo
Chuo gani atapata nafasi kufundissha na GPA ya 3.4 ya bachelor degree!? Hapo ni kusoma tu bachelor nyingine kama ndoto ni kupata qualifications za kufundisha chuo. Unatakiwa uwe na GPA ya 3.5 kwa vyuo vya kati, na 3.8 kwa baadhi ya vyuo vikuu.
 
Back
Top Bottom