Naweza kusoma tena Degree ili niipandishe GPA?

Naweza kusoma tena Degree ili niipandishe GPA?

JIPIEI ina faida gani hapo kwenye kitengo chako mzee.
 
Acha matusi na usijihesabie haki. Overall Mimi sio mpumbavu au sitafuti pesa, sijaja kuomba pesa Bali ushauri
Ee baba nakuja mbele zako kuungama kwa kusoma uzi wa kijinga kiasi hiki. Amen
Mleta uzi ingekuwa unaenda kusomea kitu tofauti ningekuunga mkono ila wazo lako la kwenda kutafuta GPA kubwa ni la kipuuzi mno. Hapo ulipo kama ni mwanaume unatakiwa utazame kutengeneza hela zaidi ili kujiandaa na majukumu ya familia kama bado hauna. Tafuta hela jomba acha upumbavu.
 
  • Thanks
Reactions: FWC
TCU wanatoaga cheti kimoja tu kwa course husika km ilivyo NECTA... Huwezi ukaenda kurudia hiyohiyo course wakati ushahitimu na kutunukiwa cheti.

Hapo labda ukasomee degree nyingine inayoendana na hiyo uliyosoma mwanzo lakini sio kuirudia hiyohiyo.
Asante kwa taarifa, sikujua kuwa Ni Kama NECTA. Nitafanya kazi ushauri huu.
 
Elimu ni bahari haina mwisho ila kama nahodha lazima ujue unaelekea wapi...unaweza kutumia nusu au robo tatu ya maisha yako kusoma na usifanikiwe, hiyo Tutorial Assistant ni entry position na utatakiwa ukasome tena Masters na GPA isishuke 4.0 na ukimaliza tena itakulazimu ukasome PhD, kama nia ni kupata hela utakuwa umetumia njia ndefu sana
 
Habari ndugu Wana JF,

Kwanza nimshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai.

Pili, nawaomba wazoefu na Mambo wanipe elimu/ufafanuzi juu ya wazo langu lifuatalo kuhusu masomo ya elimu ya juu!

Kabla sijaweka swali, niruhusuni nijisemee kwa kifupi;

Mimi ni mwajiriwa wa serikali kada ya ualimu, Nina shahada (BAEd) masomo ya Geography na Kiingereza.

Nilipata GPA 3.4, hivi karibuni nimezongwa na kiu ya kutafuta sifa za kufundisha vyuo viwe vya Kati au juu Ila kwa kuanzia tu na "tutor or tutorial assistant" kitu ambacho natambua GPA hairuhusu.

SWALI: Je, naruhusiwa kusoma upya bachelor degree of Arts with Education ili kujaribu kutafuta GPA stahiki?

Au Kuna namna yoyote ya kufanya ili kuwa na sifa linganifu? Au nikisoma masters degree moja kwa moja inatosha?

Kwa kumalizia, natamani Sana niondoke kwenye ajira iliyo chini ya TAMISEMI, hivyo iwavyo yeyote anayeweza kunipa guidelines au fursa au connection ya transfer kutoka niliko kwenda kwingineko ninakoweza kufit Nita appreciate Sana. Dm zinakaribishwa pia.

Asante sana kwa ushirikiano
Hii inaonyesha wazi ubovu wa elimu yetu, tunasoma ili tuajiliwe wala si kutambua na kutumia fulsa zilizo ktk taifa letu pendwa

Kazi ambazo wasomi huzichukulia kama kazi za kishamba ndo kazi zinazowapa utajiri wa kutisha wale walioamua kuzitumia fulsa vema,

Elimu yetu ni ya kishamba sana, Mungu katupa akili katunyima ufaham wa kuzitumia vema

Hata wale waxhache waliojaaliwa ufahamu, wakienda tu shule kila kitu hubadirika
 
Maamuzi ni yako mkuu,Mana nna mtu alisoma degree akamaliza hakuipenda akarudia nyingine na kupiga mpka PhD ,Maamuzi ni Yako Hapa tutakuponda weeh ila uhalisia unajulikana kuwa lecturer chuo kikuu GPA ianzie 3.8 na 3.5 vyuo vya kati na ka masters pia ...Maamuzi ni Yako kama Nguvu unazo fanya kile moyo unachopenda
Yes hata Mimi nimesoma na jamaa alisoma Engineering hakuipenda kabisa .Akaenda kusoma medicine tena alianzia diploma kwasasa amemaliza MMED (Anaesthesiology)
 
Nakubaliana nawe, tunaenda kubumbwa bumbwa Hadi baadae muda unapotea application Ni below expectations. Tunazidiwa na tuliowaacha mtaani
Hii inaonyesha wazi ubovu wa elimu yetu, tunasoma ili tuajiliwe wala si kutambua na kutumia fulsa zilizo ktk taifa letu pendwa

Kazi ambazo wasomi huzichukulia kama kazi za kishamba ndo kazi zinazowapa utajiri wa kutisha wale walioamua kuzitumia fulsa vema,

Elimu yetu ni ya kishamba sana, Mungu katupa akili katunyima ufaham wa kuzitumia vema

Hata wale waxhache waliojaaliwa ufahamu, wakienda tu shule kila kitu hubadirika
 
Mbona unataka kupoteza pesa na mda wako pasipo na sababu za nsingi
 
Mbona unataka kupoteza pesa na mda wako pasipo na sababu za nsingi
Zipo, muda unaotumika kumtumikia gavoo na unaobaki kwa ajili yako binafsi compared na outcome kwenye hela Kuna haja ya kuona possible way kufikia hatua nyingine Ila ushauri nimeupokea
 
Kama una nafasi na fursa ya kusoma basi nenda kasome masters.
Kwa upande wa kurudia kusoma degree hapana labda degree ya kozi nyingine tofauti.

Ukisoma masters utakuwa umejiongezea sifa/vigezo vya kupata nafasi ya kufundisha chuo.

Kila la kheri!
GPA haitakusaidia kitu bali ubunifu wako wa namna ya kutumia ulichopata darasani ukikitumia nje ya darasa. Kwani Samia elimu na GPA yake ni vipi?
 
Nimepokea wazo hili.
Unaweza Nipa mwanga zaidi mathalani nimesoma Geography na Kiingereza masters ipi inaweza kuwa na market ambayo kwa msingi nilionao naweza pambana nayo
Pitia Prospectus ya Udsm, Udom na vyuo Vikuu vichache vya East Africa kama vile Nairobi na Kampala huko utapata kuona mwanga wa vigezo kwa program mbalimbali ambazo utatamani kusoma.
Naamini wewe si mvivu wa kusoma nakutakia kila la kheri.
 
Habari ndugu Wana JF,

Kwanza nimshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai.

Pili, nawaomba wazoefu na Mambo wanipe elimu/ufafanuzi juu ya wazo langu lifuatalo kuhusu masomo ya elimu ya juu!

Kabla sijaweka swali, niruhusuni nijisemee kwa kifupi;

Mimi ni mwajiriwa wa serikali kada ya ualimu, Nina shahada (BAEd) masomo ya Geography na Kiingereza.

Nilipata GPA 3.4, hivi karibuni nimezongwa na kiu ya kutafuta sifa za kufundisha vyuo viwe vya Kati au juu Ila kwa kuanzia tu na "tutor or tutorial assistant" kitu ambacho natambua GPA hairuhusu.

SWALI: Je, naruhusiwa kusoma upya bachelor degree of Arts with Education ili kujaribu kutafuta GPA stahiki?

Au Kuna namna yoyote ya kufanya ili kuwa na sifa linganifu? Au nikisoma masters degree moja kwa moja inatosha?

Kwa kumalizia, natamani Sana niondoke kwenye ajira iliyo chini ya TAMISEMI, hivyo iwavyo yeyote anayeweza kunipa guidelines au fursa au connection ya transfer kutoka niliko kwenda kwingineko ninakoweza kufit Nita appreciate Sana. Dm zinakaribishwa pia.

Asante sana kwa ushirikiano
Kupata sifa za kuweza kufundisha katika vyuo vya kati au vya juu ni lengo zuri sana ambalo linaweza kufikiwa kupitia njia mbalimbali.

Nimejaribu kuja na majibu ya kina kuhusu maswali yako.

1. Kusoma Shahada Mpya Ili Kuboresha GPA

Inawezekana kusoma shahada nyingine ili kuboresha GPA, lakini ni muhimu kufikiria yafuatayo;
- Gharama na Muda: Kusoma shahada nyingine ni mchakato wa muda mrefu na wa gharama, hasa ukiwa tayari una uzoefu wa kazi.

- Faida Kwenye CV: Waajiri wa vyuo mara nyingi wanathamini uzoefu wa kitaaluma na sifa za juu (kama Master's) kuliko kurudia shahada ya kwanza.

Ushauri Wangu: Badala ya kusoma shahada nyingine, elekeza nguvu na muda wako kwenye masomo ya uzamili (Master’s Degree) ambayo yanaweza kukupatia sifa zinazotakiwa kwa nafasi za kufundisha.

2. Je, Master’s Degree Inatosha?
Ndiyo, kusoma Master’s Degree moja kwa moja kunatosha, na kwa vyuo vingi, sifa za uzamili zinatosha kwa nafasi ya kufundisha.

Faida Zake:
- Inakubalika Kisheria: Vyuo vingi vinakubali waombaji wenye Master’s hata kama GPA ya shahada ya kwanza haijafikia 3.5.
- Kipaumbele cha Waajiri: Waajiri wanathamini zaidi maarifa ya uzamili na utaalamu wa masomo yanayohitajika kufundishwa.
- Njia Fupi: Master’s ni mchakato wa miaka 1-2 tu, ikilinganishwa na kusoma shahada nyingine kwa miaka 3-4.

Pendekezo Langu: Chagua programu ya Master’s inayohusiana na masomo yako ya sasa (Geography au English) au fani ya ualimu (Education) ili kuongeza nafasi za ajira.

3. Namna Nyingine za Kuboresha Sifa

Ikiwa unataka kuimarisha CV yako bila kusoma shahada nyingine, jaribu mbinu hizi:
- Kozi za Ziada: Jisajili kwenye kozi fupi za kitaaluma zinazohusiana na ualimu wa vyuo. Mfano, Teaching Methodology au Higher Education Pedagogy.
- Uchapishaji wa Kitaaluma: Chapisha makala za utafiti kwenye majarida ya kitaaluma ili kuonesha umahiri wako.
- Mitihani ya Kitaaluma: Tafuta vyeti kama TEFL (kwa Kiingereza) au mafunzo maalum ya kufundisha elimu ya juu.
- Jitolee au Ajira ya Muda: Tafuta nafasi za muda katika vyuo vya karibu kwa njia ya mafunzo au masomo ya muda mfupi.

4. Kuhama kutoka TAMISEMI
- Transfer ya Kawaida: Wasiliana na ofisi ya TAMISEMI kupitia mwajiri wako na uombe kuhamishwa kwa kazi nyingine nje ya mamlaka hiyo.
- Kutafuta Nafasi za Moja kwa Moja: Tafuta kazi zinazotangazwa katika vyuo na taasisi za elimu. Omba nafasi hizo na ukifaulu, tumia barua ya kazi mpya kama msingi wa kuhamishwa.
- Mitandao ya Kitaaluma: Tumia LinkedIn na mitandao mingine ya kitaaluma kuungana na watu walioko kwenye nafasi unazolenga.

Ikiwa unahitaji msaada wa kuangalia vyuo ambavyo vinatoa programu zinazokufaa, niambie!

Ova
 
Nakubaliana nawe, tunaenda kubumbwa bumbwa Hadi baadae muda unapotea application Ni below expectations. Tunazidiwa na tuliowaacha mtaani
Kuna umri nlichukia sana mvua, kumbe elimu ingejikita kunipa facts umuhimu wa mvua na maji yanayoizunguka mitaa yangu, nsingejikuta natoka usingizin kwa kuchelewa

Imagine mtu analilia kuajiliwa ili alipwe laki 5 per month,

Huku mvua na mazingira yake inaweza nipatia million 10 kwa mwaka ambayo nikiigawa kwa mwezi napata si chini ya 7+ per month

Elimu inaandaa mafisadi yenye kuharibu future ya wengine kwa manufaa binafsi, elimu inatengeneza wauwaji wa kisiasa na kijamii

Kuna sababu/ evidence nyingi zinazoweza kukusanywa ili kuthibitisha u butu wa ubongo wa mtu mweusi kuliko kuliko merits zake, hii ni kwa sababu tumeshimdwa kuelewa kwanini tunasoma, si maprofesa wala Master’s tz ote ni rubbish tu
 
Back
Top Bottom