Nawezaje kuficha Mali zangu kwenye ndoa iliyojaa migogoro?

Nawezaje kuficha Mali zangu kwenye ndoa iliyojaa migogoro?

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
16,871
Reaction score
39,881
Wakuu naombeni mbinu Niko mahali pagumu, ndoa hii haina muda mrefu itavunjika.

Nawaza sana juu ya mali zangu nilizozipata kwa shida, huyu kibaka asipite nazo siku za mbeleni.

Haya mambo ya haki sawa yanakata.

Huyu mwanamke ananyemelea documents tugawane Mali

Naomba tu msaada wa mawazo
 
Usifiche mali, watakuja kunufaika usiowajua, afadhali hata ndugu wajue au kama umejaliwa watoto basi andikisha majina ya watoto kama wamiliki. Mali haifichwi
Akizuchukua Mali zote na watoto, Mimi nitaishi vipi mkuu.

Lengo lake achukue Mali na watoto Bado ni wadogo kisheria wanapaswa kuwa mama.

Sasa Mimi nitaanza upya aisee

Nibaki Sina kitu
 
Kama ndoa imefika pabaya, usikimbilie kuficha au kuhamisha mali kwa siri. Hilo linaweza kukuongezea matatizo kisheria.

Tafuta ushauri wa mwanasheria, tambua mali zipi ni zako binafsi na zipi zinaweza kuwa mali ya ndoa, kisha hifadhi documents zako kwa njia salama na halali.

Muhimu zaidi, usifanye maamuzi kwa hasira.
 
Back
Top Bottom