Ni kweli. Kuna jamaa ni mtaoji sadaka mkubwa kuliko umri na muonekano wake, yuko kariakoo. Siku nakutana naye ananitembeza akaniambia yeye hatumii pesa zake, amefanya kazi na matajiri muda mrefu wanamuamini, anapewa bidhaa za viwandani tena hadi kutoka china bure, anauza anarudisha pesa zao na anakula faida.
Ndivyo alivyoniambia muuza dagaa mmoja Temeke Stereo. Anasema yeye hamjui hata anayemtumia dagaa, anasikia tu yuko kagera huko. Kule wanavua wanakausha wanapaki, wqnawatumia wao wanauza wanarushisha pesa yao na wanatumiwa tena mtaji uaminifu.
Pia kuna watu wanaoesa nyingi benk ni waoga, wengine hawana matumizi nazo, wengine waliiba tu serikalini, wengine ni urithi, chukua hizo, waazime benki zifanyie mambo ya maana alafu kula faida warudishie pesa zao na gharama kidogo ya kusaidia kulipa wafanyakazi wa benk, na majengo waliyopanga (riba).
Kama unaaminika unaweza kuwaomba wakakupa bila riba waliozitunza huko moja kwamoja.
Duniani huko ndivyo mambo yanavuoenda. Mtazamo eti hadi uwe na pesa zako ndio uwe tajiri ni mtazamo wa kijima na kimasikini sana.