Milion 10 kuifanya iwe bilion 2 ni jambo linalowezekana kikubwa ni kuifungua akili na kujua Nini Cha kufanya na vya kufanya viko vingi Ila kipi ni sahihi ?
Hilo ndio muhimu
Na Kwa kuanzia ni kuichakata hiyo bilioni 2 Ili uone unapaswa kutengeneza sh ngap Kwa mwaka, Mwezi, Hadi siku ili Sasa uone ni kipi ufanye Ili ufikishe malengo yako ndani ya miaka 5
Hebu tuone analysis ndogo hapa chini
2000,000,000 Ă·5= 400,000,000/=
Hapo tunagundua kumbe kila mwaka unatakiwa utengeneze milion 400 Ili kufikisha malengo yako ndani ya miaka 5
400,000,000Ă·12= 33,333,333/=
Hapo tunagundua pia kila mwezi unatakiwa utengeneze wastan wa milion 33 Ili utimize malengo yako ya 2bn ndani ya miaka 5
33,333,333Ă·30= 1,111,111/=
Hapo tunagundua pia kila siku unatakiwa utengeneze wastan wa milion 1 na laki 1 Ili kutimiza malengo yako ndani ya miaka 5.
Swali dogo la muhimu wote kujiuliza je ?
HAKUNA WATU WANAOTENGENEZA FAIDA YA MILION 1+ KWA SIKU?
Jibu ni wapo labda kama wewe tu hujatembea ila Kuna watu Wana business za kawaida sana na wanapiga faida ya Milion na change Kwa siku
Ni aina Gani ya business Sasa hiyo nayo ni business za watu kukupa hizo business idea Ndio maana walamba asali mjini ni wachache
Nafahamu lengo lako ilikuwa ni kukusanya ideas kutoka kwenye vichwa vya watu bahati mbaya sijaona aliyekupa idea ya kukufanya upate hiyo 2 bilion ndan ya miaka 5
Ila kwa kifupi ni jambo linalowezekana Tena hata Kwa kutumia nusu ya hyo pesa,
Mimi naweza kukwambia kama kweli unahiyo milion 10 hamia kwangu unaishi kwangu unanipa nusu ya hiyo pesa mm nakupatia milion 1 kila siku mm Ndio nitaifanyia Kazi hyo pesa yako ww mwenyew ukiishuhudia Kwa macho yako ndani ya miaka 5.
Hilo huwezi tuna business proposal zinazoweza tumia nusu ya pesa yako ila kama nilivyokwambia hapo juu ideas ya biashara au Nini Cha kufanya upate Hela nacho pia ni biashara toa pesa upate pesa business proposal inalipiwa 25% ya pesa uliyotaja kama hapo umesema ni 10M utalipa 2.5M unabaki na 7.5M utapigwa msasa wa Nini Cha kufanya na unafanyaje na connection zote za wapi uchukue bidhaa na uuze wapi Kwa pesa isiyozidi 5M na hyo 2B yako ndani ya 5yrs unaitengeneza mwenyew
Kama ulikuwa serious nitafute tuonane uso kwa uso Nina ideas 3 kwaajili yako ambazo ukifanyia Kaz utarud hapa kuleta mrejesho ila kama uliandika kama chai kufurahisha kijiwe usinitafute.
Kwa kumaliza bongo Bado hatujafunguka sana kwenye uaminifu kwenye business partner na kuwekeza kwa watu wafanye Kwa niaba Yako ila ukweli watu wengi wanaendesha maisha na matajir wakubwa wengi hufanya hvyo hao kazi yao ni kupokea tu Hela .
Mfano mdogo: Aliko dangote anakiwanda Cha cement Mtwara Lakini kile kiwanda sio kama yeye Ndio mwendeshaji , yeye kafanya uwekezaji wa miundombinu wezeshi Kisha kipo chini ya watu ambao wanakiendsha Kwa kitu Hadi ajira japo brand name ni yake wanaingiza zaidi ya 1B per day kwake ni kama kujenga frem ya duka na kukodisha Kwa mtu.