Nawezaje kuiokoa familia yangu na mateso ya jini huyu?

Nawezaje kuiokoa familia yangu na mateso ya jini huyu?

Pole sana kaka,

Dawa yake huyo mdudu ni ndogo sana. Itaisha moja kwa moja. MNATAKIWA KUOKOKA WEWE NA MKEO, MKIRI KAMA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO.

Ushauri:
1. Nenda Kanisa la Kilutheri lililopo hapo Kimara pamoja na familia yako yote. Omba kumuona Mchungaji mueleze shida unayopitia, ataomba nawe na kuwapa sala ya toba. Baada ya hapo hakikisha mnashiriki maombi mara kwa mara familia nzima ili kama hilo dudu lilikuwa linasumbua pia mtoto liondoke kabisa. Hii huduma ni bure kabisa.

2. Amka Usiku saa sita, omba mwambie Mungu shida yako kwa kumaanisha. Omba hata lisaa limoja kila siku usiku, fanya hivi mara kwa mara. Mungu aonaye haja ya moyo wako atakuponya kwa Jina la Yesu.

3. Mwamini Mungu, atakuponya.

Ngumu Sana kuamini haya! Dawa ni Yesu tu. Ila hawasikiagi.
 
Naitwa Ododi 35yrs Mkazi wa Kimara Korogwe. Nipo kwenye ndoa kwa muda wa miaka 6 nimebahatika kupata mtoto 1 ambae anafikisha mwaka mmoja tangu kuzaliwa na kuja kwenye hii dunia yetu ukiachana na wengine 7 ambao wapo kwenye ulimwengu mwingine.

Najua unaweza usinielewe nikisema ulimwengu mwingine kuna watoto 7, ndio ninao si uongo ila hili sijambo nataka mnisaidie mawazo kwa leo.
Muendelezo kaka
 
Pole aisee ila uliwezaje kung'ang'ana na manzi mwenye mapepo hadi ukafunganae ndoa kabsa wakati kitaani kuna mabinti kedekede wasio na vipengele
Mkuu, halafu hili jaribu lake nani angelipitia?Binti hakua na haki ya kuolewa?Na kama je kuna katabia kwa mkewe kalimsuit vizuri mleta mada na akaona mapepo si kikwazo! Hakuna mwanadamu anaejua ya mbeleni ni yapi,je!Angemkwepa huyu mkewe halafu akachukue hao ambao wewe umeona wako poa halafu waje wapate tatizo kubwa zaidi ya mapepo huku tayari wakiwa katika ndoa.Kwa mbaali nimeona kama una UBAGUZI.Hujawahi ona au kusikia kwa nguvu ya upendo tu mtu anaoa kipofu,muathirika wa ukimwi,n.K?
 
Naitwa Ododi 35yrs Mkazi wa Kimara Korogwe. Nipo kwenye ndoa kwa muda wa miaka 6 nimebahatika kupata mtoto 1 ambae anafikisha mwaka mmoja tangu kuzaliwa na kuja kwenye hii dunia yetu ukiachana na wengine 7 ambao wapo kwenye ulimwengu mwingine.

Najua unaweza usinielewe nikisema ulimwengu mwingine kuna watoto 7, ndio ninao si uongo ila hili sijambo nataka mnisaidie mawazo kwa leo.

Tuendelee na Mada tajwa.
Pole sana japokuwa kuna watu watakubeza na kukataa baadhi ya mambo kwa upopoma wao wa kutokujua ulimwengu wa pili upoje lakini kulingana na maelezo yako huyo ni jini mahaba,na jini mahaba ni jini ambaye ana nguvu sana hasa akiwa ndani ya ukoo au uliyewekeana maagano nae..Kama ni jini mahaba wa vipengele hivyo viwili huyo hawezi kutoka mzee hata ufanye nini utadanganywa tu nenda kwa yesu mara kwa masheik atatulia tu baada ya muda atarudi na makali mara mbili yake trust me!! Ni heri umuache tu huyo mwanamke ana maagano aliyoyaweka huko nyuma tayari hawezi kuishi na mwanaume so sad!! Hili jambo limewahi kuntokea hata mimi lakini si kwa namna ya mateso unayopata wewe tulifika na mke wangu hadi kwa paroko lakin mwisho wa siku hakuna kilichofanyika ikabidi niachane tu na yule binti...
Rakims
Pole sana kaka,

Dawa yake huyo mdudu ni ndogo sana. Itaisha moja kwa moja. MNATAKIWA KUOKOKA WEWE NA MKEO, MKIRI KAMA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO.

Ushauri:
1. Nenda Kanisa la Kilutheri lililopo hapo Kimara pamoja na familia yako yote. Omba kumuona Mchungaji mueleze shida unayopitia, ataomba nawe na kuwapa sala ya toba. Baada ya hapo hakikisha mnashiriki maombi mara kwa mara familia nzima ili kama hilo dudu lilikuwa linasumbua pia mtoto liondoke kabisa. Hii huduma ni bure kabisa.

2. Amka Usiku saa sita, omba mwambie Mungu shida yako kwa kumaanisha. Omba hata lisaa limoja kila siku usiku, fanya hivi mara kwa mara. Mungu aonaye haja ya moyo wako atakuponya kwa Jina la Yesu.

3. Mwamini Mungu, atakuponya.

KWANI HAYA MAMBO YA ULOZI YAPO KWELI?? TENA ZAMA HIZI ZA SAYANSI NA TEKNOLOJIA???
Upo dini gani mkuu?
 
Why mnarudi nyumba hiyo hiyo
Hebu Hama nyumba uone
 
Hujawahi kujihusisha na mambo ya kishirikina siku za nyuma? isije kuwa ni maagano uliyoingia na hao viumbe ukashindwa kuyatimiza ndio unaanza kuadhibiwa, hii ni either wewe au mkeo.

Kama mliwahi kwenda kwa waganga dawa ni moja tu; Maombi. Muanze kuomba wewe na familia yako kwa pamoja, mchague sehemu mtayoona ni sahihj kwenu kutimiza hilo, japo sijajua dini yako.

Ila kama ni mkristu hili sio tatizo, yapo makanisa mengi tafuta wachungaji uwaeleze shida zako huku nawe ukianza jitihada za dhati za kumtafuta na kumjua Yesu Kristu kupitia mafundisho yake kwa kusoma biblia. Hili ilifanye kwa pamoja mkiwa na familia yako sitting room kila siku amini matatizo yako yatakwisha.
Sijawahi Jihusisha na mambo hayo.
 
Naitwa Ododi 35yrs Mkazi wa Kimara Korogwe. Nipo kwenye ndoa kwa muda wa miaka 6 nimebahatika kupata mtoto 1 ambae anafikisha mwaka mmoja tangu kuzaliwa na kuja kwenye hii dunia yetu ukiachana na wengine 7 ambao wapo kwenye ulimwengu mwingine.

Najua unaweza usinielewe nikisema ulimwengu mwingine kuna watoto 7, ndio ninao si uongo ila hili sijambo nataka mnisaidie mawazo kwa leo.

Tuendelee na Mada tajwa.

Nia ya kuweka maandishi haya hapa chini ni vile nimekua nikipitia magumu mengi mimi pamoja na mke wangu na sasa naona mtoto pia anapitia shida nyingi, mke wangu amekua akiteswa sana na Kiumbe cha ajabu, amekua akikiona "fluently" Kikiwa na mapembe kama mbuzi kifupi ni kiumbe ambacho kina tisha sana, Ni kimekua kikimtesa, kumkaba, kumuingilia kivyovyote kikitaka, kinamfanya awe mgonjwa malanyingi, amekua hana nafasi ya kuwaza na kufikilia vyema.

Tatzo lilianza kabla ata sija funga nae ndoa, nakumbuka kuna siku nilimuacha nyumbani kwangu nikaenda kazini, ilipofika saa nane mchana alinipigia simu akilia sana, ikanibidi kurudi home. Nilipofika nilimkuta kalala chini hawezi ata kugeuka, alinambia kuna kiumbe cha ajabu kimemfata nakumbuluza nyumba nzima, amehangaika sana kuamka kashindwa lakini alikua macho anakiona na anasikia watu nje wakiongea nakupita ila pamoja na kupiga kelele hakuna alie sikia.

Mke wangu aliniita kwa majina yangu, na akasema alivyo kua akiona kipindi yule mdudu akimbuluza pale ndani ni kama amevunja vyombo vyote na TV, nikamjibu hakuna kitu chochote kilicho vunjika kila kitu kipo kama nilivyo acha asubuhi, Mke wangu aliinuka na kukaa kama dakika 20 bila kusema kitu, baadae akanambia anahisi maumivu makali sana kwenye mbavu, mgongoni, shingoni na mikononi.

Nilimvua nguo aliyo kuwa kaivaa juu kuangalia hizo sehemu anazopata maumivu, niliona mikwaluzo ya kucha alama za vidole, na zimevia damu sehem hizo zote, kiukweli sikuelewa nikamtafutia tu dawa za maumivu nikakaa kimya, ila cha ajabu usiku wake kile kiumbe kikaja tena, this time kilikua kinaongea ila mimi sikioni kikiniomba ni mpatie mwanamke wangu then chenyewe kinipe utajiri na mali nilikataa na nilisikia kikiondoka kinalia.

Ikapita muda maisha yakaendelea mpaka nikaja muoa huyu bibie, Safari ya ndoa haikua nyepesi nilipitia wakati mgumu sana kufanikisha zoezi la ndoa, matatizo ndo yakaanza mimba zinapotea juu kwa juu, Lile dudu likaanza mambo yake, mke akawa hawezi baki na nyumba itambidi akae nje mpaka nirudi na nikirudi hawezi enda kulala mpaka twende wote chumbani, nikama likawa linataka kumpa uchizi.

Siku moja kuna rafiki yangu akanipa wazo nijaribu kumtafutia Tiba kwa masheikh wa Pemba. Nikaomba likizo kazini ili niweze mtibia mke wangu, kazini nikapewa siku7 nikaona sawa, nikatafuta ndege mpaka Pemba mimi na mke wangu ili akafanyiwe visomo wamtoe huyo mdudu.. Mmh ndugu zangu ndo kama nikawa nimeenda kuwasha moto kwenye petrol station.

Visomo viliisha tuka rejea Dar es salam, Mambo yakawa mabaya zaidi, lile dudu ndo likaanza mkaba malanyingi kuliko mwanzo, sikukata tamaa nikaendelea kuhangaikia kwa mafundi mbali mbali ambao walidai wanaweza nisaidia mikoani huko bila mafanikio. Akiba yangu ikaanza kupungua kwa kasi sana sikumaliza mwezi kazini ni kapigwa chini.

Nikarejea sasa kukaa bila kazi hali ikawa mbaya sana, ilikua 2018 nilifedheeka sana kama mnavyoelewa maisha ya mjini ukiwa nacho alafu ghafla kikakata. Nikapata insomnia kwa muda maana nilikua silali usiku, mke wangu anaweza anza piga kelele anaona vitu mimi sioni usiku wamanane.

Usiku anapigakele za kuogopa vitu ambavyo mimi sioni, akidai amezungukwa na watu wa ajabu pale tulipo lala huku akijificha mgongoni kwangu, anadai kuna kitu wanamtoa tumboni anapiga kelele analia ni msaidie, imagine sioni chochote nabaki kama zuzu sielewi naanzia wapi, kuna muda alilia sana akasema wanamuuwa, alinistua sana kuangalia vizuri naona damu kitandani, nilipomwambia damu zina kutoka alipiga kelele moja na akazima.

Nilipata hofu nilipiga simu kwao nikawaelekeza juu ya yanayo endelea kwa mtoto wao, nilimkimbiza Botch Hospital alivyochekiwa Daktari akadai alikua na mimba inaonekana imeharibika.

ITAENDELEA
pole mkuu
 
Ndo narejea nyumbani taendeleza
Pole sana mkuu kwa mkasa unaopitia. Ninakushauri uende kwenye kanisa la walokole ujieleze kwa Mchungaji, ukubali kuokoka wewe na mkeo hayo mateso yataisha. Ukiombewa bila kuokoka, unakuwa huna ulinzi wa kimungu juu yako ukirudi nyumbani na majini yanawarudia. Pia kuhusu changamoto unazopitia zinasababishwa na mapepo aliyonayo mke wako kwa sababu umemuoa mtu ambaye ni mke wao katika ulimwengu wa Roho. Kwa msaada wa kiroho nitumie namba yako ya simu pm tuwasiliane.
 
Nawewe ulipata mental disorder?
Sio mental disorder.
Sio mm ila ni mtu niliyekuwa nae kwenye mahusiano aliwai kupoteza mimba mbili hiv hiv kwa style sawa na hio sema yeye alikuwa ananiambia tu niseme kama sipo tayari waitoe na kwel zinatoka pasipo kutumia dawa yeyote.

Je hio nayo ni mental disorder?
 
Back
Top Bottom