Nawezaje kuiokoa familia yangu na mateso ya jini huyu?

Nawezaje kuiokoa familia yangu na mateso ya jini huyu?

Naitwa Ododi 35yrs Mkazi wa Kimara Korogwe. Nipo kwenye ndoa kwa muda wa miaka 6 nimebahatika kupata mtoto 1 ambae anafikisha mwaka mmoja tangu kuzaliwa na kuja kwenye hii dunia yetu ukiachana na wengine 7 ambao wapo kwenye ulimwengu mwingine.
Ilipoanzia fungua kiungo

Sehemu ya kwanza

---------

Baada ya kutoka hospital tulirejea nyumbani, na maisha yetu yakaendelea kama kawaida, nikaendelea kupigwa matukio kila siku, nikayumba sana kiuchumi. Alikuja mzee mmoja wa kisukuma huwa na fahamiana nae kwa muda akaniambia niende nyumbani Niliko zaliwa kweli nilifanya hivyo.

Nikiwa nyumbani nilipelekwa sehem na uncle wangu, nikakaa pale kwa muda wa siku nne nikiwa naendelea na visomo, kuna Bibi alikuja nakunambia mitihani yote inatokana na upande wa mwanamke ubabani kwao wanamambo mazito kidogo, Basi mimi nilimpa taarifa muhusika nikaomba aongee na wazazi wake wajue namna yakumsaidia.

Nilipo rejea tena nyumbani hakukua na afadhali mwanamke bado aliendelea kukabwa daily, siku moja wife alikua anaumwa ni kawanae home tumekaa sebuleni nikaona kabadilika anajaa kama kapuliziwa upepo, akaanza kuongea huku akisaga meno, akanishika mkono kwa nguvu nakunambia kama mimi jeuri atanigongesha nyoka, akasisitiza huyu mwanamke ana kiti chake kuzimu ni muache ambebe. (Pepo linaongea)

Kiukweli sikuwahi pata hofu kama siku hiyo, nikaanza kutafuta msaada sasa, ni kawa nawaza nikigongeshewa nyoka itakuwaje si ndo napotea mimi, nilikimbilia kwa shekh mmoja Ilala nikafanyiwa visomo akanipa na dawa zakutumia siku kadhaa upepo ukatulia kidogo.

Mungu akafanya wepesi nikajishikisha sehem tena kazi baada ya kukaa bench sana, baada ya mwezi mmoja kazini nikapata dili nono life likachenj nikafukia fukia mabonde yote, kama unavyoelewa ukikaa mtaani bila kazi kwa muda sana na maisha yetu ya Dar, kama ni thamani zako utajikuta umeuza kama si kuweka bondi ili maisha yasogee.

Ghafla kuna siku nilikuta wife kaandika ujumbe kwenye karatasi na kachora kile kitu ambacho huwa anakiona, nilipiga picha nikamtumia mkwe kwa Whatsp! Wiki jana usiku ule ule na kusema inatakiwa binti yao afanyiwe visomo, nilipo mpatia mama mkwe lile karatasi alilochora mwanae ghafla niliona kabadilika anaunguruma kama mdudu akajitupa chini kama vile gorikipa anadaka mpira, akaanza kujigeuza ile style mamba akiuma kitu Alikua nikama anapigana na kitu tusichoona ikawa taflani pale ndani.

Basi nikatulia nashangaa kama movie, mpaka baadae kulivyo tulia, ndugu wa mwanmke wote wako pale na Baba mkwe akadai kuna sehem tunaweza saidiwa kama najiweza nimpeleke mke wangu. Nikaona sawa, siku inayofuata nika tengeneza mazingira yakutoka kazini Ijumaa mapema ili ni safiri na Jpili nirejee mzigoni.

Ijumaa imewadia niko mzigoni napambana nikaomba kumuona HR nikamueleza nina mgonjwa nyumbani na hakuna mtu wa kunisaidia nimepigiwa simu kazidiwa alinielewa na kusema nimuone mtu anishikie kipengele changu, nikachomoka ilikua saa sita mchana nikaenda home fasta nikampitia wife tukaruka mkoani.

Tulifika pale jioni tuka tafuta sehem yakulala asubuhi tukawa kwa mwalimu akanipa mazoezi yake akasema tatzo dogo ni Jini mahaba akadai atampatia dawa litatoka fasta na mimba ata shika vizuri na itakua. "Waswahili wanasema uongo wa mganga nafuu kwa mgonjwa" Ila sisi kwetu ilikua tofauti.

Ratiba yetu kisomo ilikua saa 8 mchana lakini wife ghafla akaanza ku bleed, na masheikh hawafanyii mtu hilo zoezi akiwa kwenye siku zake. Nikamuelekeza sheikh akanambia ni hilo dudu linavuruga tiba nimuachie yeye atajua nini chakufanya, Basi alipambana awezavyo Jpili tukarejea usiku Dar.

Inaendelea......

Kusoma kilichoendelea fungua kiungo

Sehemu ya tatu
 
Mkuu hapo ni YESU YESU ndio suluhisho wa matatizo yenu! Kama upo tayari ni PM hapo Kimara mwisho kuna mtumishi wa kweli wa Mungu hiyo ni kazi ndogo kwa YESU.Huyo mtumishi kanisaidia sana na ni mtu wa MAOMBI sana! usikimbilie kwenye makanisa ya mafuta, mchanga, keki e.t.c Nenda kwa mtumishi wa Mungu atake kufundisha neno na Maombi Basi Bwana Yesu atawafungua.

Ukiwa tayari ni PM maana naona haukai mbali.
 
+255 718 216 553mtafute huyu anaitwa Lono Hamza huyu dogo alimtibia mwanangu Mimi niliyeteseka nae for 3yrs nahangaika kuanzia makanisani mpk sijui wapi!mateso aliyopitia mwanangu ni makubwa sana siwezi sema kaka Ila niliteseka nikafilisika nkarudi kua mzee ila kwanza yakupaswa kua na imani thabit juu ya Mola wako!!!usichanganye na waganga wa kienyeji sijui wapiga ramli utafeli!ukishindwa kwa Lono nambie nkusaidie tena kwa mzee mwingine yuko Chanika anaitwa sheikh Said sina namba yake ya simu!hao sio wapiga ramli na wala sio washirikina wa kutumia tunguli!
Shirki haiponeshi anaeponesha ni Mungu tu

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Baada ya kutoka hospital tulirejea nyumbani, na maisha yetu yakaendelea kama kawaida, nikaendelea kupigwa matukio kila siku, nikayumba sana kiuchumi. Alikuja mzee mmoja wa kisukuma huwa na fahamiana nae kwa muda akaniambia niende nyumbani Niliko zaliwa kweli nilifanya hivyo.

Nikiwa nyumbani nilipelekwa sehem na uncle wangu, nikakaa pale kwa muda wa siku nne nikiwa naendelea na visomo, kuna Bibi alikuja nakunambia mitihani yote inatokana na upande wa mwanamke ubabani kwao wanamambo mazito kidogo, Basi mimi nilimpa taarifa muhusika nikaomba aongee na
Nimekupa namba hyo mtafute huyo dogo na hana gharama ukitaka maelezo zaidi njoo PM maana najua atakuuliza umetoa wapi ila mmeweka hapo kwa maslahi ya wengine pia
 
Back
Top Bottom