Nawezaje kumwachisha mtoto kunyonya kidole?

NIMEONA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2019
Posts
3,862
Reaction score
5,693
Ni katoto ka mwaka mmoja na miezi kama mitatu hivi.

Kakiwa na usingizi tu basi ni lazima kanyonye kidole chake ndo kanalala vizuri, ukijaribu kukatoa tu anaamka na ugomvi (kilio) unakuwa mkubwa.

Hadi awe amelala sana (fofofo) ndo unaweza ukamtoa. Hii tabia imekuwa sugu hadi ukucha wa kidoleni unaanza kuharibika jambo ambalo si jema.

Mbinu gani nitumie wadau kumtoa huyu katika janga hili?
 
Huo umri muache tu aendelee kunyonya kidole, ndio muda wake wa kuenjoy hiyo kitu,

Kama issue ni ukucha kuharibika basi mnunulie vile viplastiki sijui vinaitwaje ambavyo watoto hunyonya ili asinyonye kidole.
 
Tafuta njia umdanganye kuhusu hicho kidole kama walivyosema wadau pia kama Una roho ngumu weka pilipili. Mbinu ya plasta inafanya kazi Sana hata kwenye kuachisha nyonyo.
Shukrani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…