Nawezaje kumwachisha mtoto kunyonya kidole?

Nawezaje kumwachisha mtoto kunyonya kidole?

Ungemuwahi tangu mchanga ukamvalisha soksi za mikono, angelia weeeh lakini angezoea na kuacha,

Na sasa hujachelewa, muweke plasta,

Sio kweli kua ataacha mwenyewe kwa sasa labda akishakua mkubwa level ya sekondari, lakini mtoto kunyonya kidole anakua mzembe sana wala sio poa.
 
Mtoto wangu ana miaka mitano na pointi lakini bado ana nyonya kidole. Nilitumia Kila njia nimefeli . Sasa nimebaki namcheki tu nikiamini ataacha mwenyewe.
 
Mpake upupu hatonyonya hata maziwa yko tena
 
Ni katoto ka mwaka mmoja na miezi kama mitatu hivi.

Kakiwa na usingizi tu basi ni lazima kanyonye kidole chake ndo kanalala vizuri, ukijaribu kukatoa tu anaamka na ugomvi (kilio) unakuwa mkubwa.

Hadi awe amelala sana (fofofo) ndo unaweza ukamtoa. Hii tabia imekuwa sugu hadi ukucha wa kidoleni unaanza kuharibika jambo ambalo si jema.

Mbinu gani nitumie wadau kumtoa huyu katika janga hili?
Usikubali kumfanyia mtoto wako mbinu za kinyama kama watu wanavyokushauri. Mwache ataacha mwenyewe baada ya kukua.
 
Back
Top Bottom